Mimi nilikuwapo uwanjani Jana... Kuna shida sana pale katika logistics za kuingia uwanjani.. Yaani ili uingie ni mapambano.. Mashabiki, walinzi na polisi.. Inakosesha hata hamasa ya kwenda pale uwanjani. Huwezi kwenda na familia yenye watoto wadogo kwenye mechi za aina ile, ni hatari.
Nafikiri taratibu za namna za kuingia ziboreshwe ili kuondoa kero. Itafutwe namna nzuri ya mashabiki kuingia haraka bila kusababisha misururu mirefu isio na lazima, coz kwa maoni yangu ndio kitu kilichosababisha mageti kuharibiwa. Hili la viti nafikiri tukiwafungia mashabiki watajifunza. Kuzifungia timu sioni kama itasaidia, na vile vile ule uwanja utakuwa underutilised.. Kumbuka ni Yanga na Simba tu wanaweza kuujaza uwanja ule ukiondoa matamasha..