Hii sio ya bandari ya Bagamoyo dada.Habara ya miaka ya nyuma imerudishwa leo.
Muwe mnafuatilia kwanza kabla ya kucopy na kupaste, ni vizuri kutuhabarisha ila haraka haraka mnaishia kuleta fake news....
Hii habari huenda ikawa ni version nyengine ya ilee ya bandari ya Bagamoyo.Hii habari Ni ya mwaka gani?
Huu mkopo wa China umetangazwa wapi mbona hii habari ipo twitter tu ila haipo mainstream media?Rais wetu na mpigania wanyonge amekataa kupokea mkopo wa dola 10 billion kutoka kwa China ili kupambana na corona,Rais amefikia uamzi huo baada ya kuona masharti ya mkopo huo ni magumu na yanaliweka taifa letu rehani.
Kumbe bado iko kwenye mazungumzo? Mbona mwenda zake alitudanganya eti ulishasainiwa ili ionekane yeye ndie kaokoa?Kumekucha kumekucha, Yale Mashart ndani ya Mkataba wa bandari ya Bagamoyo ambayo hatujawai kuuona Mkataba zaidi ya kusimuliwa Sasa yanaelezwa hapa,
Mnakumbuka Hayati Magufuli akisema Ni kichaa pekee angeweza kuukubali Mkataba ule, lakin Ndugai akasema alipotoshwa,
Tuyapitie Mashart tuyaone,
Kumbe bado iko kwenye mazungumzo? Mbona mwenda zake alitudanganya eti ulishasainiwa ili ionekane yeye ndie kaokoa?
Wao kama wawekezaji walikuja na masharti yao na sisi tunapaswa kutoa ya kwetu lakini sio kujifanya eti tumeukataa moja kwa moja kama Wazee wa Legacy wanavyotaka tuamini.
Ninadhani ile interview ya kuongoza malaika ilkua ngumu sana maana mwendazake aliweka chumvi sehemu nyingi sana. Miradi yote inajengwa na pesa za ndani wakati tunakopa, awamu ya tano imezindua viwanda 2,400 siju vinafanyia kazi Madagascar!Kumbe bado iko kwenye mazungumzo? Mbona mwenda zake alitudanganya eti ulishasainiwa ili ionekane yeye ndie kaokoa?
Wao kama wawekezaji walikuja na masharti yao na sisi tunapaswa kutoa ya kwetu lakini sio kujifanya eti tumeukataa moja kwa moja kama Wazee wa Legacy wanavyotaka tuamini.
Magu yeye alitaka Jk alaumiwe aonekane alikuwa anauza nchi. Wakati Jk hakuusaini kwa sababu ulikuwa kwenye mchakato. Ndio maana Deus anasema hatujaukataa bali tumewapa nasisi masharti yetu tunawasubiri.Hakusema hivyo mzee, alikataa kuupitisha kwa masharti yaliyokuwa yameletwa ili kuacha tathmini na makubaliano mengine! Hakufuta mradi huo, ulikuwa kama alivyosema jamaa huyo.
Sio mradi ulejeshwe bali wawekezaji warudi tuendelee kubargain kwa terms zinazotufaidisha sote.- Hao wachina wasanii sana, miaka 99 waendeshe huo mradi maana yake kuna kizazi cha watanzania kingepita bila kufaidi matunda ya huo mradi, wakati baada ya miaka 33 wangekuwa wameshapata faida.
- Bado wakataka wapunguziwe na bei ya baadhi ya vitu kwenye huo mradi kama maji, umeme, na gas, na zaidi biashara ikiwa mbaya wafidiwe.
- Kwenye ardhi badala ya mradi ndio upewe ardhi na ulipiwe land rent wachina wakata wasilipie, na bado wakata kuendesha biashara za hapo bandarini.
Kwa terms za aina hii ndio wakina Ndugai wanaupigia debe wanataka mradi urudishwe, kama sio wana maslahi binafsi hapa ni sababu gani nyingine waliyonayo? hawa wanasiasa hawana huruma kabisa na mtanzania, they are selfish more than the word itself.
Kama Kikwete angekuwa bado na muda wa kukaa madarakani angetekeleza huu mradi, bahati nzuri tu muda wake ulikwisha, lakini nia ya kutunyonya watanzania tayari alikuwa nayo, kwa hili hakwepi lawama.
Hili liwe fundisho sasa hii miradi mikubwa yote mikataba yake iwekwe wazi kila mtanzania aijue kabla haijaanza kutekelezwa, wanasiasa wasituamulie hatma yetu kwenye kila kitu watatuangamiza.
Walichotaka kukifanya wachina kwetu ni kama kile walichofanya uingereza kwa mchina kukodi mji wa hongkong uwe chini yao kwa muda wa miaka 99 kama sikosei.....
Mataifa yanauza vipande vya ardhi so usishangae kusikia kuna mataifa wachina wanadominate eneo au bandari au airport, yale ni matokeo ya kukodi au kulinunua hilo eneo. Miaka 99 kukodi eneo ni investment nzuri sana ambayo inamfaidisha zaidi yule anaekodishwa na sie anaekodi.....
Ni vema kabla ya kushabikia haya mambo basi tujifunze kwanza kwa kuingia maktaba na hata kutafiti kutoka kwa wenzetu yaliyowakuta tutaelewa.