Rais Magufuli ataja sababu kusitisha ujenzi bandari ya Bagamoyo kwa Mkopo wa Dola Bilioni 10

Rais Magufuli ataja sababu kusitisha ujenzi bandari ya Bagamoyo kwa Mkopo wa Dola Bilioni 10

Habara ya miaka ya nyuma imerudishwa leo.

Muwe mnafuatilia kwanza kabla ya kucopy na kupaste, ni vizuri kutuhabarisha ila haraka haraka mnaishia kuleta fake news.

Hii habari ni ile loan ya kujenga bandari aliyoigomea sababu walikua wanataka kuchukua control ya bandari nzima wajiamulie wanavyotaka, ni ushenzi na rais yeyote mwenye akili timamu angekataa, jakaya alikubali lakini kufuli alivyoingia tu akasema hapana
 
Habara ya miaka ya nyuma imerudishwa leo.
Muwe mnafuatilia kwanza kabla ya kucopy na kupaste, ni vizuri kutuhabarisha ila haraka haraka mnaishia kuleta fake news....
Hii sio ya bandari ya Bagamoyo dada.
 
Rais wetu na mpigania wanyonge amekataa kupokea mkopo wa dola 10 billion kutoka kwa China ili kupambana na corona,Rais amefikia uamzi huo baada ya kuona masharti ya mkopo huo ni magumu na yanaliweka taifa letu rehani.
Huu mkopo wa China umetangazwa wapi mbona hii habari ipo twitter tu ila haipo mainstream media?

Debt swapt for investment mbona ipo sana mkuu na inatambulika kisheria. Hata deni la Gadaffi mliposhindwa kulipa mliswap kwa uwekezaji kwenye social project ya chuo cha kiislamu!! Kwahyo sio kitu kigeni kma mnavyotaka potosha.

Pia Sri lanka hao walipewa mkopo as mkopo ila mradi wa Bagamoyo ingekuwa ni investment tu ila serikali inatoa guarantee basi.

Pia hiyo miaka 99 ni sera ya ardhi inatoa fursa kumililishwa ardhi mpka muda huo hivyo kuna taasisi nyingi tu zimepewa ardhi kwa miaka 99 na sio kwamba ni ufisadi kma mnavyotaka potosha.

Then faida za uwekezaji wa billion 10 dola, haupimwi kwa kodi ya direct ila multiplier effect. Ajira, indirect tax kwa bidhaa watakazonunua Tz, kuongeza mitaji kwa mabenki ya ndani, money supply pia ingepaa hivyo uchumi wa mtu mmoja mmoja ungepaa. Hta kma mkaendeleza bandari zote bado msingefikia robo ya mapato ya hapo Bagamoyo na huu ni ukweli lazima tuambiane hivyo sijaona opportunity cost hapo!

Kingine kwenye negotiation kuna fall back position so mtu anapoleta offer ya miaka 99 anajua mkinegotiate utamshusha mpka 33 so mtasettle kwenye 66 years hapo, kwahiyo mijadala yote huwa inaanza kwa figures za ajabu thrn counter offers zitaishusha mpka mfikie fallback ndio mnakua win win ila huwezi anza negotiation kwa ombi la hati ya 33 years? It's insanity.

Hata Magu aliingia kwenye negotiation na Barrick akidai Trillion 400!! Ila baada ya mjadala wakasushana hadi kufikia hizo minimal reforms.

Ni vizuri tupunguze ushabiki bila kutafiti. Sri Lanka ni tofauti na model ya Tz.
 
Magufuli alizungukwa na wezi, wanafiki na mafisadi wakubwa na ndio maana kuwa muda ilimbidi achukue vijana wazalendo kutoka upinzani ili ashirikiane nao kuendesha nchi.

Huu mradi ni kweli utagharamikiwa na China kwa asilimia zaidi ya 90.

Lakini kwanini wachina wajimikishe bandari yetu kwa miaka yote hiyo.

Tutawaambia nini wajukuu wetu na watoto wetu watakaokuwa watumwa kwenye nchi yao.

MagufuliLalaSalamaHakikaTutakukumbuka.
 
Kumekucha kumekucha, Yale Mashart ndani ya Mkataba wa bandari ya Bagamoyo ambayo hatujawai kuuona Mkataba zaidi ya kusimuliwa Sasa yanaelezwa hapa.

Mnakumbuka Hayati Magufuli akisema Ni kichaa pekee angeweza kuukubali Mkataba ule, lakin Ndugai akasema alipotoshwa.

Tuyapitie Mashart tuyaone.
 
Kumekucha kumekucha, Yale Mashart ndani ya Mkataba wa bandari ya Bagamoyo ambayo hatujawai kuuona Mkataba zaidi ya kusimuliwa Sasa yanaelezwa hapa,

Mnakumbuka Hayati Magufuli akisema Ni kichaa pekee angeweza kuukubali Mkataba ule, lakin Ndugai akasema alipotoshwa,

Tuyapitie Mashart tuyaone,

Kumbe bado iko kwenye mazungumzo? Mbona mwenda zake alitudanganya eti ulishasainiwa ili ionekane yeye ndie kaokoa?

Wao kama wawekezaji walikuja na masharti yao na sisi tunapaswa kutoa ya kwetu lakini sio kujifanya eti tumeukataa moja kwa moja kama Wazee wa Legacy wanavyotaka tuamini.
 
- Hao wachina wasanii sana, miaka 99 waendeshe huo mradi maana yake kuna kizazi cha watanzania kingepita bila kufaidi matunda ya huo mradi, wakati baada ya miaka 33 wangekuwa wameshapata faida.

- Bado wakataka wapunguziwe na bei ya baadhi ya vitu kwenye huo mradi kama maji, umeme, na gas, na zaidi biashara ikiwa mbaya wafidiwe.

- Kwenye ardhi badala ya mradi ndio upewe ardhi na ulipiwe land rent wachina wakata wasilipie, na bado wakata kuendesha biashara za hapo bandarini.

Kwa terms za aina hii ndio wakina Ndugai wanaupigia debe wanataka mradi urudishwe, kama sio wana maslahi binafsi hapa ni sababu gani nyingine waliyonayo? hawa wanasiasa hawana huruma kabisa na mtanzania, they are selfish more than the word itself.

Kama Kikwete angekuwa bado na muda wa kukaa madarakani angetekeleza huu mradi, bahati nzuri tu muda wake ulikwisha, lakini nia ya kutunyonya watanzania tayari alikuwa nayo, kwa hili hakwepi lawama.

Hili liwe fundisho sasa hii miradi mikubwa yote mikataba yake iwekwe wazi kila mtanzania aijue kabla haijaanza kutekelezwa, wanasiasa wasituamulie hatma yetu kwenye kila kitu watatuangamiza.
 
Hakusema hivyo mzee, alikataa kuupitisha kwa masharti yaliyokuwa yameletwa ili kuacha tathmini na makubaliano mengine! Hakufuta mradi huo, ulikuwa kama alivyosema jamaa huyo.
 
Walichotaka kukifanya wachina kwetu ni kama kile walichofanya uingereza kwa mchina kukodi mji wa hongkong uwe chini yao kwa muda wa miaka 99 kama sikosei.

Mataifa yanauza vipande vya ardhi so usishangae kusikia kuna mataifa wachina wanadominate eneo au bandari au airport, yale ni matokeo ya kukodi au kulinunua hilo eneo. Miaka 99 kukodi eneo ni investment nzuri sana ambayo inamfaidisha zaidi yule anaekodishwa na sie anaekodi.

Ni vema kabla ya kushabikia haya mambo basi tujifunze kwanza kwa kuingia maktaba na hata kutafiti kutoka kwa wenzetu yaliyowakuta tutaelewa.
 
Kumbe bado iko kwenye mazungumzo? Mbona mwenda zake alitudanganya eti ulishasainiwa ili ionekane yeye ndie kaokoa?

Wao kama wawekezaji walikuja na masharti yao na sisi tunapaswa kutoa ya kwetu lakini sio kujifanya eti tumeukataa moja kwa moja kama Wazee wa Legacy wanavyotaka tuamini.
Ninadhani ile interview ya kuongoza malaika ilkua ngumu sana maana mwendazake aliweka chumvi sehemu nyingi sana. Miradi yote inajengwa na pesa za ndani wakati tunakopa, awamu ya tano imezindua viwanda 2,400 siju vinafanyia kazi Madagascar!
 
Hakusema hivyo mzee, alikataa kuupitisha kwa masharti yaliyokuwa yameletwa ili kuacha tathmini na makubaliano mengine! Hakufuta mradi huo, ulikuwa kama alivyosema jamaa huyo.
Magu yeye alitaka Jk alaumiwe aonekane alikuwa anauza nchi. Wakati Jk hakuusaini kwa sababu ulikuwa kwenye mchakato. Ndio maana Deus anasema hatujaukataa bali tumewapa nasisi masharti yetu tunawasubiri.
 
- Hao wachina wasanii sana, miaka 99 waendeshe huo mradi maana yake kuna kizazi cha watanzania kingepita bila kufaidi matunda ya huo mradi, wakati baada ya miaka 33 wangekuwa wameshapata faida.

- Bado wakataka wapunguziwe na bei ya baadhi ya vitu kwenye huo mradi kama maji, umeme, na gas, na zaidi biashara ikiwa mbaya wafidiwe.

- Kwenye ardhi badala ya mradi ndio upewe ardhi na ulipiwe land rent wachina wakata wasilipie, na bado wakata kuendesha biashara za hapo bandarini.

Kwa terms za aina hii ndio wakina Ndugai wanaupigia debe wanataka mradi urudishwe, kama sio wana maslahi binafsi hapa ni sababu gani nyingine waliyonayo? hawa wanasiasa hawana huruma kabisa na mtanzania, they are selfish more than the word itself.

Kama Kikwete angekuwa bado na muda wa kukaa madarakani angetekeleza huu mradi, bahati nzuri tu muda wake ulikwisha, lakini nia ya kutunyonya watanzania tayari alikuwa nayo, kwa hili hakwepi lawama.

Hili liwe fundisho sasa hii miradi mikubwa yote mikataba yake iwekwe wazi kila mtanzania aijue kabla haijaanza kutekelezwa, wanasiasa wasituamulie hatma yetu kwenye kila kitu watatuangamiza.
Sio mradi ulejeshwe bali wawekezaji warudi tuendelee kubargain kwa terms zinazotufaidisha sote.
 
Walichotaka kukifanya wachina kwetu ni kama kile walichofanya uingereza kwa mchina kukodi mji wa hongkong uwe chini yao kwa muda wa miaka 99 kama sikosei.....

Mataifa yanauza vipande vya ardhi so usishangae kusikia kuna mataifa wachina wanadominate eneo au bandari au airport, yale ni matokeo ya kukodi au kulinunua hilo eneo. Miaka 99 kukodi eneo ni investment nzuri sana ambayo inamfaidisha zaidi yule anaekodishwa na sie anaekodi.....

Ni vema kabla ya kushabikia haya mambo basi tujifunze kwanza kwa kuingia maktaba na hata kutafiti kutoka kwa wenzetu yaliyowakuta tutaelewa.

You actually think that’s a good idea?

Mtu aje kujenga hotel kwenye kiwanja chako bila kukulipa ata senti moja,

Biashara ikianza wewe usipate chochote.

Anarudisha faida ya ujenzi ndani ya miaka 5 lakini hataki umdai chochote mpaka baada ya miaka 20.

Asilipe kidi yoyote kwa serikali ndani ya muda huo.

Sehemu ya kiwanja chako ulichomkatia baada ya kujenga kama kuna spare space huna say. Akitaka na yeye anaweza muuzia mtu mwingine afanye uwekezaji wowote kwa masharti kama uliyompa yeye?

Yote hayo kwa sababu kaajiri ndugu zako kwenye kazi za uhudumu (kutandika vitanda, usafi, kutunza maua, na nyingine zisizo na skills).

You actually think that is a good investment? Kama bado lazima utakuwa na matatizo.

Hao ni wa kwenda TIC tu serikali isipoteze muda na hao watu, useless kweli kweli.
 
Back
Top Bottom