Rais Magufuli ataja sababu kusitisha ujenzi bandari ya Bagamoyo kwa Mkopo wa Dola Bilioni 10

Mkuu Zitto Junior! Asante Kwa pointi hii!!

Unadhani ni kivipi mradi wa bagamoyo, ndio uwe suluhisho la kuubeba uchumi wetu mbali na Gas yetu pale Mtwara

Mimi nadhani, Wakati wa Miradi ya kinyonyaji kama huu tunaotaka kuuingia, Tufike mahali kama nchi tukatae

Mikataba Kwa mfano ya Madini, Nayo huwenda ilisainiwa Kwa lengo kama Hilo ambalo umebainisha, na ndio Maana mrahaba tukawa tunapata 2% Kwa mauzo yote, na Mkataba ukisoma ni miaka 💯

Ukimuuliza aliyesaini, naye atakwambia alitarajia kuona viwanja vya ndege vyetu vikiwa bize, Bandari zetu kuwa bize, Kwa hiyo kama ni mapato makubwa watayapata huko

Wazungu wanazijua Sana Hesabu, sio wa kwendea hivihivi, hawana Mkataba wa kukunufaisha wewe na Wala hawajawahi kupanga hivyo, Ila hulazimika Ikiwa watakuta viongozi wenye uwezo kichwani

Mradi wa bagamoyo Kwa masharti yake, usipojadiliwa ili kuondoa Baadhi ya masharti ya kinyonyaji, hauna Tija, ni Bora tudili na bomba letu kutoka Hoima, Hilo ndilo litazifanya Bandari zetu kuwa bize
 
Semantics tu za kutokukukubali facts; ni mapendekezo ya kuweka mkataba! Magufuli hakufuta mkataba bali alikaa kuingia mkataba huo kwa mapendekezo hayo.
Atakataaje kuingia mkataba usiokuwepo; huoni kwamba unajichanganya?

Ili pawepo na mkataba ni lazima pawe na mapendekezo na majadiliano kati ya pande mbili. Haya ni mapendekezo ya mchina ndiyo aliyoyakataa Magufuli na sio mkataba.
Hakuna cha 'semantics hapa, labda uwe hujui maana halisi ya neno hilo.
 
Hapa ni swala la Tanzania na hao wawekezaji; Tanzania ndiyo iliyokataa mapendekezo ya wawezekezaji kuwa hayakulingana na interest za Tanzania, je kuna upande gani mwingine ambao Tanzania ilitakiwa kusikiliza tena kabla ya kutoa uamuzi?
Unauliza swali la kitoto.
Huoni kuna pande mbili hapo? China na Tanzania?

Kama Tanzania imekataa mapendekezo aliyotoa mchina, yenyewe haiwezi kutoa mapendekezo ya upande wake kulinda 'interests' zake?
 
Mkuu unaweza kushare upya hiyo clip
 
Nimeelewa concern yako lakini tukubaliane kabisa hata serikali ina justify Stendi ya Magufuli, ATCL, kutopandisha mishahara kwa hoja ya hiyo hiyo ya "uchumi ni mtambuka". Kwamba faida ya ATCL sio kuingiza mabilion kupitia mauzo ya ndege ila utalii, ku ease logistics, n.k. kwahiyo tukubaliane kabisa kwamba hiyo justification ipo kwa miradi yote ya kiserikali sasa kivp kwa bagamoyo ndio iwe mutual exclusive?

Mimi nadhani kuliko kuvutana sana kati ya serikali, wananchi,spika, AZAKI n.k huo mkataba (at least draft) upelekwe kwa kamati ya bunge ya uwekezaji walau waishauri serikali na pia kuruhusu maoni ya stake holders ikiwemo sisi wananchi.

Mwisho wa siku mradi ufanyike kwa Win Win situation.... Hata ile vurumai ya ACACIA tulikua tuna demand trillion 400 lakini tukasettle for less kwa kuanzisha subsidiary bila kuvunja kabisa mkataba.

So kikubwa mradi uungwe mkono (pending amendment chache kwenye makubaliano) kuliko mawazo ya kufutilia mbali hiko kitu ndio nachopinga. Maana kuna watu hawataki hata mazungumzo wanataka ufutwe outright sasa kwa staili hiyo tutafika kweli?
 
Ubarikiwe Sana mkuu!!
 
Unauliza swali la kitoto.
Huoni kuna pande mbili hapo? China na Tanzania?

Kama Tanzania imekataa mapendekezo aliyotoa mchina, yenyewe haiwezi kutoa mapendekezo ya upande wake kulinda 'interests' zake?
Haya sawa mzee; wewe umejibu kikubwa kwa kujua kuna kuna pande mbili yaani Tanzania na China lakini Tanzania imekataa mapendekezo ya China halafu unauliza kwa nini ilikataa mapendekezo ya upande mmoja tu- sijui ulitaka ikate na mapendekezo ya upande upi tena. Counter offer unataka ndiyo ambayo Kakoko anasema wanaendelea na majadiliano. Serikali ilikuwa haijaingia nao mkataba wowote, ila kwa upande wao wawekekezaji hao walitaka mkataba ambao serikali itawapa concessions hizo ambazo serikali ilikataa.
 
Counter offer unataka ndiyo ambayo Kakoko anasema wanaendelea na majadiliano. Serikali ilikuwa haijaingia nao mkataba wowote, ila kwa upande wao wawekekezaji hao walitaka mkataba ambao serikali itawapa concessions hizo ambazo serikali ilikataa.
'Full circle', unarudi pale pale nilipoanzia, sasa sijui unabishia kitu gani?
 
Mkuu unaweza kushare upya hiyo clip



Clip iliyowekwa jana ilikuwa ☝️ ndio premise ya mchango wangu. Mkurugenzi katoa maelezo mazuri ya areas of negotiation ambazo awazikubali.

Past concerns on the same areas.

Unaweza kupitia na hiyo mada nyingine uangalie na michango ya wengine.

In terms of financial appraisal ya mradi concerns za mkurugenzi mtu mwingine yoyote makini will come to the same conclusion with logic alone bila ya hata kuona huo mkataba.

Ukisikiliza anachosema huyo Kakoko ni confirmation of their fears kwa watu ambao walishatafakari kwa makini hiyo $10 billion inaenda wapi na mkurugenzi gave an honest opinion in financial terms.

Uwekezaji mwingine wachina wanatakiwa kwenda TIC kwa sababu TPA hawana shida nao. Ndio maana nikakuuliza why wanataka na viwanda vyao viwe sehemu ya uwekezaji wa bandari?

Ni mkataba mmbovu.
 
Umenisoma vema lakini au umekurupuka.... Sasa mbona ni kama unaongea kile kile ninachokikemea mimi?! Hebu nisome upya kisha ucomment vema kama mtu anesoma na kuelewa alichosoma.
 
Mradi unaanza tena.Je Jiwe alitudanganya?
Jiwe alidanganya sababu mradi hakuubuni yeye ndio maana kaenda kujenga uwanja wa Ndege huko kwao.... kwenye Biashara meza ya mazungumzo ndio inaamua Kila kitu unategemea mtu aingize mahela yake Kisha aje kibwege kama mchina alikuja na terms zake ilitakiwa nasisi twende na zetu kisha tunakubaliana Sasa sisi tunategemea tuletewe dhahabu kwenye sahani ni ujinga kwakweli
 
Bila shaka sasa hivyo vipengele vya ovyo watakuwa wameshaviondoa vyote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…