Rais Magufuli ataja sababu kusitisha ujenzi bandari ya Bagamoyo kwa Mkopo wa Dola Bilioni 10

Rais Magufuli ataja sababu kusitisha ujenzi bandari ya Bagamoyo kwa Mkopo wa Dola Bilioni 10

Ni Tanzania tu ambapo kiongozi aliyekuwa kimya mpaka mkataba wa kinyonyaji ukapita anakuja kusema huo mkataba ulikuwa mbovu! Wakati huo huo hata yeye huo Mkataba hataki kuonyesha nini kiko ndani ya huo mkataba alipokubali upite, kisha akaukataa.
Unaelewa fika jinsi katiba ya Tanzania ilivyo na kuwa Rais ndiyo mwisho wa kila kitu, ulitaka Magu kama waziri afanyeje?
Kichekesho ni pale rais huyo huyo anapogomea katiba mpya ili mambo yaendeshwe kwa uwazi zaidi na watu wanashangilia na kusema ni kiongozi sahihi!
Hivi ukimfunamia mzee wako na dada wa kazi utapiga tarumbeta kuwaambia majirani?
 
Unaelewa fika jinsi katiba ya Tanzania ilivyo na kuwa Rais ndiyo mwisho wa kila kitu, ulitaka Magu kama waziri afanyeje?

Hivi ukimfunamia mzee wako na dada wa kazi utapiga tarumbeta kuwaambia majirani?

Katiba ya Tanzania inasema kila mwananchi ni mlinzi wa rasilimali ya umma, au yeye anasoma katiba ipi?

Unaifananisha nchi na ngono ya mzazi wako?
 
Huna utetezi wenye mashiko zaidi ya kuleta mipasho.
Kama Magufuli angepayuka na kupiga kelele, leo hii asingeweza kuwa na nafasi ya kubadilisha mikataba ya madini, kuzuia leseni ya IPTL na kufufua mashirika ya uchukuzi.
 
Kama Magufuli angepayuka na kupiga kelele, leo hii asingeweza kuwa na nafasi ya kubadilisha mikataba ya madini, kuzuia leseni ya ITPL na Kufufua mashirika ya uchukuzi.

Kwa hiyo kubadilisha jambo nchi hii ni mpaka uwe rais? Sasa mnapotaka watu wawe wazalendo kabla hawajawa maraisi mnaamaanisha nini? Hamjui mpaka uonyeshe uzalendo ni lazima uwe rais?
 
Kwa hiyo kubadilisha jambo nchi hii ni mpaka uwe rais? Sasa mnapotaka watu wawe wazalendo kabla hawajawa maraisi mnaamaanisha nini? Hamjui mpaka uonyeshe uzalendo ni lazima uwe rais?
Hapana, hata wewe unayehoji unaweza kuwa mzalendo ila kufanya jambo kubwa nchi nzima lazima uwe na dhamana na hakuna mwenye hiyo dhamana zaidi ya rais.
 
Hapana, hata wewe unayehoji unaweza kuwa mzalendo ila kufanya jambo kubwa nchi nzima lazima uwe na dhamana na hakuna mwenye hiyo dhamana zaidi ya rais.

Mkuu jamaa amekuuliza nani mwenye dhamana ya kulinda rasirimali za nchi?
Nafikiri kuwa mzalendo ni pamoja na kuweka misingi imara itakayozuia mambo mabaya yasitokee siku za usoni, sasa misingi ni pamoja na kubadili katiba na baadhi ya sheria ili ziweze kuilinda nchi kila penye mwanya wa kutuingiza kwenye shida.. Huwezi kuwa mzalendo au kujiita mzalendo halafu ukashindwa kuweka misingi imara ya siku za usoni.
 
Hapana, hata wewe unayehoji unaweza kuwa mzalendo ila kufanya jambo kubwa nchi nzima lazima uwe na dhamana na hakuna mwenye hiyo dhamana zaidi ya rais.

Huo ujinga wa kwamba rais ndio mwenye dhamana ya kufanya jambo kubwa la nchi ndio hapo kama nchi tumejikuta tunaendeshwa kwa utashi wa rais, akiamua kutupiga anatupiga kisha genge lake linamtetea. Sisi tunaoamini kwenye nguvu za mtu tunaamini mifumo ndio sahihi kwa kuendesha nchi kwani mustakabali wa nchi hautapimwa kwa utashi wa rais.
 
View attachment 1123438

RAIS John Magufuli amesema sababu kubwa ya kusitishwa kwa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ni masharti magumu yaliyomo katika mkataba wa utekelezaji wa kazi hiyo.

Jiwe la msingi la ujenzi wa bandari hiyo liliwekwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2015 na ulitarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 10. Bandari hiyo endapo ingejengwa ingekuwa kubwa zaidi Afrika Mashariki ikiwa na ukubwa wa ekari 3,000 na viwanda 190 vingejengwa.

Akizungumza jana kwenye mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliowashirikisha wafanyabishara kutoka wilaya 139 nchini, Rais Magufuli aliweka wazi sababu za kusitishwa kwa ujenzi wa bandari hiyo. Rais Magufuli alisema “kwenye mkataba wa ujenzi wa bandari hiyo kulikuwa na vipengele vya ovyo”. Rais Magufuli alisema mojawapo ya masharti ni kutojengwa wala kuendelezwa kwa bandari yoyote kuanzia eneo la Tanga hadi Mtwara.

"Yaani kwenye eneo lote kuanzia Tanga hadi Mtwara kusijengwe bandari yoyote. Bandari ya Kilwa tusiiendeleze, Bandari ya Mtwara ambayo itawezesha mikoa ya kusini kupokea mafuta badala yake Dar es Salaam kisha yarudi huko, hatutakiwi kuiendeleza, Barabara kutoka Mtwara hadi Bamba Bay ambayo itatuwezesha kusafirisha mizigo hadi Msumbiji tusiijenge," alisema Rais Magufuli

Pia alisema wawekezaji hao wangeweza kumiliki ardhi kwa hati ya miaka 99 pamoja na kutoruhusiwa kuuliza nani anamiliki eneo hilo. Rais Magufuli alisema sharti lingine ni gharama zitakazotumiwa na mwekezaji huyo katika ujenzi wa bandari hiyo kutakiwa kurejeshwa.
Salaam hizi ziwafikie wakaazi wa msoga wote kuwa kila masika na mbu wake
 
Shamba la bibi, kuna mambo lazima tukubali Rais wetu anajitahidi sana kuyaweka vizuri na tumpe heko. Katika kulinda uridhi wetu kwa kweli nampa heko, anajitahidi sana.

Mikataba ya hovyo kama hii ni wizi wa mchana kabisa. Hamna maslahi kwetu kama watanzania. Hii mikataba kama ya mangungo ifutiliwe mbali.

Natamani aingilie mikataba ya gasi pia, kule nako sijui kama tupo salama.

Kama watakubaliana na mkataba ambao ni win win wajenge ila mkataba ambao hatufaidi chochote, hatuhoji chochote yaani tumeuza uridhi wetu kwa miaka 99 bila chochote watu wanachuma tu, tena bado turejeshe gharama na hatuna uwezo wa kufanya chochote mbadala, hapana kwa kweli..khaaa

Heko Rais, tuliendie urithi wetu tutakukumbuka kwa hilo.
Hayo maneno yako nakumbuka uliwahi kuyasema enzi za kikwete
 
Mikatabba ya Kiwanja cha ndege cha Chato, ya Stiegler's Gorge, ya ununuzi wa ndege pia viwekwe hadharani, ili watanzania wafanye comparisons!!!
Tutashukuru sana tukiwekewa hiyo mikataba
 
Ngoja tusikie mabobezi ya ukosowaji toka ufipani yakija na taarifa ya madhara tutakayopata kuukataa mradi huu usiendelee niko pembeni mwa smartphone yangu nasubiria mapovu kwa makamanda
Tuna mpa pole mzee mswahili wa msoga
 
Hiyi ilikuwa kazi kuu ya serikali ya awamu ya nne na watendaji wake wakuu!! Halafu unaona watu wanakenua!! Hata mababu zetu ambao hawakuwa wamepata elimu ya hata kindergarten ya Kimangaribi(Western education) hawakuwa na akili finyo kama za wasomi wa vyuo vikuu wenye Masters na PhDs!!!! Kudos Rais Dr Magufuli.
Hiyo yote inafanyika chini ya ccm
 
Back
Top Bottom