Rais Magufuli ataja sababu kusitisha ujenzi bandari ya Bagamoyo kwa Mkopo wa Dola Bilioni 10

Rais Magufuli ataja sababu kusitisha ujenzi bandari ya Bagamoyo kwa Mkopo wa Dola Bilioni 10

Unakariri sana wewe kuhusu mifumo.

Mifumo inaleta maana kama watu wanatabia za kufuata taratibu, watanzania tulizoeshwa kuvunja sheria na kufanya mambo kiholela, angalia tuu barabarani ambapo tuna mifumo mizuri ya kuongozea magari lakini watu hawafuati sheria. Madereva wanapita kwenye taa nyekundu, hawasimami kwenye alama za pundamilia kupisha watembea kwa miguu, sasa huoni kuwa tabia zetu zinatakiwa kubadilishwa kwanza?

Anayebadilisha tabia za wenzake anaingia madarakani kwa mfumo wenye matatizo, na hayuko tayari mfumo huo ubadilike kwani anajua hata yeye hatakuwa na nafasi aliyonayo nayo. Kibaya zaidi yuko madarakani bado anatumia mbinu hizo hizo zenye mawaa, yeye na chama chake kuendelea kupata madaraka! Ajabu hili lipo Tanzania tu.
 
Jiwe ana mengi sana ya kumchana Jk..
Jk na ccm ni genge la wahuni na wapumbavu tushukulu mungu kumpata raisi magufuli angalau ananyoosha nchi ccm na jk walikuwa ni SHARI KAMILI BOLA JPM NI NUSU SHARI hivi unauzaje nchi na usalama wake hiyo bandari ingetumika kutorosha tembo na wanyama na madini yetu nakuingiza sumu za kutuangamiza waafrica kikwete ni raisi aliye staili kunyongwa hadharani
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Kwanza yakupasa uelewe bagamoyo ni homeland kwa huyo jk, hivyo chochote kinawezekana kabla hujaanza kuumiza kichwa sana.

Nafahamu huyo Mkwere alikua anajaribu kuvutia kwake, lakini sio kwa level ya kuuza nchi yote. Na hii imekua desturi kwenu maana jiwe naye kuna makubwa anazindua Chato, atakayekuja baada yake anaweza akayatumia kumchana kama anavyofanya kwa Mkwere.
 
Tatizo kubwa nchi yenu hiyo mumeingia kwenye ubepari kichwa nje nje bila hata kujua mfumo wenyewe unaendeshwa vipi, nyote mumekua na tamaa za kiajabu ajabu, hebu sikiliza hiyo hotuba ya rais, kwamba hata waliofidiwa kwenye ardhi ya Bagamoyo walikua makajanja wa Dar, sio wakazi wa Bagamoyo.
Ndiyo maana mimi napendelea mfumo wa kiuchumi wa nchi kama za Scandinavia kwa kuwa zina aina fulani ya usafi, hii mifumo ya kimagharibi ina madhambi mengi nyuma yake. Mfano watu wanaongelea maendeleo ya waingereza huku wakisahau jinsi walivyowazuia wahindi kutengeneza nguo ili wapeleke pamba UK, viwanda vyao viimarike. Uchumi huo wa dhulma hauwezi kutamalaki, siku wanaonyonywa wakijanjaruka, uchumi unaporomoka.

Umedokeza kuhusu sisi Kuingia kichwa kichwa wakati unasahau kuwa Kenya ndiyo mfalme wa kuingia kichwa kichwa Afrika mashariki.

Toka enzi zile za Mzee, mmekuwa mkiingia mazima na ubepari uchwara kwa kuruhusu watu wachache kujimilikia ardhi na hivyo kuleta matabaka yanayoondoa usalama wa nchi yenu. Umimi umekukaeni vichwani mnashindwa hata kuwa na usafiri wa umma Nairobi, kwa kuwa tuu wakina Sonko wanamiliki biashara matatu.

Uzuri Tanzania tunajifunza kutokana na makosa, watu wetu wa kazi wapo macho na walishaona tunakoelekea siko, wakauzima moto "professionally" (kama anavyopenda kusema Putin), tukapata Magufuli (aminia huyu mzee hakuja kwa bahati mbaya). Nyinyi bado mnaendelea kulishwa mavyakula msiyojua yamepikwaje, safisheni hiyo nchi kabla haijaharibika kama Somalia ya Siad barre.
 
Nafahamu huyo Mkwere alikua anajaribu kuvutia kwake, lakini sio kwa level ya kuuza nchi yote. Na hii imekua desturi kwenu maana jiwe naye kuna makubwa anazindua Chato, atakayekuja baada yake anaweza akayatumia kumchana kama anavyofanya kwa Mkwere.
Mtu kujenga kwao si dhambi maana kuna watz pia,ila isiwe kwa dhamna ya watz wote na rasilimali zao.

Sisi tunashukuru leo maana tumempata magu, na hivi ninavyokwambia, taa mpya ya matumaini imewaka.
 
Kikwete was a very diplomatic likeable guy who built the Tanzanian brand internationaly..But he was weak in making good contracts and dealing with corruption..For those who think JPM should have resigned from kikwete cabinet because the president was weak, they should know that parties with strong ideology are like families, you dont abandon your home because your father is a drunkard..You work with him untill he sobers up or leaves office then you select a sober leader..
Magufuli is sober, very sober and rejecting bagamoyo shows that he is not all talk and no action, he is a doer
 
Anayebadilisha tabia za wenzake anaingia madarakani kwa mfumo wenye matatizo, na hayuko tayari mfumo huo ubadilike kwani anajua hata yeye hatakuwa na nafasi aliyonayo nayo. Kibaya zaidi yuko madarakani bado anatumia mbinu hizo hizo zenye mawaa, yeye na chama chake kuendelea kupata madaraka! Ajabu hili lipo Tanzania tu.
Ukihamia nyumba iliyojaa uchafu utaanza kupanga makochi na kuweka mapambo ukutani au utaanza kuisafisha kwanza? Ngoja 2025 ifike ndio uanze hizo lawama.
 
Ndiyo maana mimi napendelea mfumo wa kiuchumi wa nchi kama za Scandinavia kwa kuwa zina aina fulani ya usafi, hii mifumo ya kimagharibi ina madhambi mengi nyuma yake. Mfano watu wanaongelea maendeleo ya waingereza huku wakisahau jinsi walivyowazuia wahindi kutengeneza nguo ili wapeleke pamba UK, viwanda vyao viimarike. Uchumi huo wa dhulma wauwezi kutamalaki, wanaonyonywa wakijanjaruka, uchumi unaporomoka.

Umedokeza kuhusu sisi Kuingia kichwa kichwa wakati unasahau kuwa Kenya ndiyo mfalme wa kuingia kichwa kichwa Afrika mashariki.

Toka enzi zile za Mzee, mmekuwa mkiingia mazima na ubepari uchwara kwa kuruhusu watu wachache kujumilikia ardhi na hivyo kuleta matabaka yanayoondoa usalama wa nchi yenu. Umimi umekukaeni kichwani mnashindwa hata kuwa na usafiri wa umma Nairobi kwa kuwa wakina Sonko wanamiliki biashara matatu.

Uzuri Tanzania tunajifunza kutokana na makosa, watu wetu wa kazi wapo macho na walishaona tunakoelekea siko, wakauzima moto "professionally" (kama anavyopenda kusema Putin), tukapata Magufuli (aminia huyu mzee hakuja kwa bahati mbaya). Nyinyi bado mnaendelea kulishwa mavyakula msiyojua yamepikwaje, safisheni hiyo nchi, itaharibika kama Somalia ya Siad barre.

Hamna kosa kwa nchi kuwa kwenye mfumo wa ubepari/captalism, sisi tulianza mapema hatukununa na umetusaidia pakubwa maana kila Mkenya amepewa fursa ya kutanua anavyoweza bila kulemazwa na mfumo. Hayo mliyokaririshwa na Nyerere kwamba Kenya imemilikiwa na wachache huwa sihangaiki kuyajibu maana hayana ukweli wowote, mlikaririshwa tu ili mfumbie macho mazuri ya ubepari na kubakia watumwa wa umaskini wa kijamaa, halafu cha kushangaza alikua anaachia waarabu na wahindi wamiliki kila kitu, leo hii Dar mjini utadhani yao.

Tatizo, mumechelewa sana hadi mumekuja kukumbatia ubepari kama hamna ujuzi nawo, ni kama mtu ajizuie hanywi pombe wala anasa miaka yote ya ujana halafu aje kushtuka kwenye umri wa miaka 50 ndio anaanza anasa, mtu kama huyo huwa kichaa kwa jamii maana hufanya vitu vya kiajabu ajabu.

Leo hii Watanzania mumejawa na tamaa mnafanya vitu ambavyo hata havijawahi kuskika kwenye nchi nyingine duniani, mnawachinja albino eti kutafuta utajiri, tamaa ya mali na utajiri inawafanya mnachinja hata watoto ili mtumie viungo vyao kwenye ushirikina wa kusaka utajiri, kipindi fulani mliua tembo hadi mkapigiwa makelele na dunia. Watu wenye roho kama hizo hata kuuza nchi wataiuza bila kupepesa macho, ndio maana utakuta nchi mumeingia mikataba ya ukichaa mtupu, mnaliwa kila kitu maana kila mtu ameingiwa na tamaa bila uzalendo wala huruma.
 
please my no 1,kipindi cha awamu ya nne wewe si ulikuwa waziri ?why hukuliona hili na kulizungumzia?njaa yako ilikupeleka usiyaseme haya?na please my no 1 tuelezee also kuhusu mauzo ya nyumba za serikali je yalikuwa above the board???
Hilo la kuuzwa kwa nyumba za serikali ni moja blunder kubwa kuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu, kwa bahati mbaya mkulu alihusika moja kwa moja kwenye hilo.
 
"If those were the terms they gave", there are always two(or even more than two) sides of the story.
That was the best decision if those were the terms they gave, burdening your country and enslaving your people for generations to come so that you can have a shiny new port that will not not be fully utilized unless you shut down the other port.

It's like telling me to cut my hand so that you give me food.

Africans should vigorously develop their own local capacity esp in TECH, so that we stop relying on these scam leeches.
 
Hamna kosa kwa nchi kuwa kwenye mfumo wa ubepari/captalism, sisi tulianza mapema hatukununa na umetusaidia pakubwa maana kila Mkenya amepewa fursa ya kutanua anavyoweza bila kulemazwa na mfumo. Hayo mliyokaririshwa na Nyerere kwamba Kenya imemilikiwa na wachache huwa sihangaiki kuyajibu maana hayana ukweli wowote, mlikaririshwa tu ili mfumbie macho mazuri ya ubepari na kubakia watumwa wa umaskini wa kijamaa, halafu cha kushangaza alikua anaachia waarabu na wahindi wamiliki kila kitu, leo hii Dar mjini utadhani yao.
Acha urongo wako... eti, "wakenya wote wamepewa fursa", unamaanisha wakikuyu? Mbona mpaka leo mmewawekea wajaluo kauzibe kwenye serikali kuu?
Tatizo, mumechelewa sana hadi mumekuja kukumbatia ubepari kama hamna ujuzi nawo, ni kama mtu ajizuie hanywi pombe wala anasa miaka yote ya ujana halafu aje kushtuka kwenye umri wa miaka 50 ndio anaanza anasa, mtu kama huyo huwa kichaa kwa jamii maana hufanya vitu vya kiajabu ajabu.
Nyinyi mlio wahi mko wapi? Mna nini cha kutuzidi zaidi ya madeni?
Leo hii Watanzania mumejawa na tamaa mnafanya vitu ambavyo hata havijawahi kuskika kwenye nchi nyingine duniani, mnawachinja albino eti kutafuta utajiri, tamaa ya mali na utajiri inawafanya mnachinja hata watoto ili mtumie viungo vyao kwenye ushirikina wa kusaka utajiri, kipindi fulani mliua tembo hadi mkapigiwa makelele na dunia. Watu wenye roho kama hizo hata kuuza nchi wataiuza bila kupepesa macho, ndio maana utakuta nchi mumeingia mikataba ya ukichaa mtupu, mnaliwa kila kitu maana kila mtu ameingiwa na tamaa bila uzalendo wala huruma.
Hiyo ya tamaa unayoisema kuna uwezekano ikawa ni 'sabotage'. kuna kamfumo kaliwekwa ili kuifanya Tanzania ije kuwa kama Kongo, ila tumewastukia.
 
Ukihamia nyumba iliyojaa uchafu utaanza kupanga makochi na kuweka mapambo ukutani au utaanza kuisafisha kwanza? Ngoja 2025 ifike ndio uanze hizo lawama.

Nyota njema huonekana asubuhi, tulitarajia kwenye huu utetezi wako tuone akiheshimu box la kura. Ukishaona kiongozi yoyote haheshimu box la kura na uwazi, hapo ujue harekebishi lolote zaidi ya kujenga himaya yake, na kutengeneza taifa la watu wanaomuabudu. Kwa bahati mbaya watanzania na dunia ilishapita huko, aliyefaidi hilo la kuabudiwa alikuwa ni Nyerere tu kutokana na uelewa mdogo ulikuwepo wakati huo. Mwaka wa nne huu bado hiyo nyumba inasafishwa tu, amejiandaa kutawala milele?
 
joto la jiwe si kitambo sana kakurupuka hapa akisema kuwa urafiki wa Tz na Uchina ni wa kutoka kitambo Sana na hautaisha hata sasa(CCM blind Mentality). Hii dunia hamna urafiki ni interests tu so Hii Mambo ya wafia chama ya kubwabwaja kuwa waliikomboa Afrika no upuzi mtupu...hope fools like mkorinto redeemer thisdayes have learnt a valuable lesson.
 
Mtoe magu ktka mambo ya kipuuzi kama hayo, labda kama umemjua baada ya kuwa rais 2015.

Huyu mtu mna chuki naye, lakini isiwe sababu ya kumpaka ubaya kwa gharama,
Wewe ni mfuata chama/ upepo, huna msimamo Magu ni Mungu kwako.
 
Ni juzi tu Geza Ulole alifungua Uzi wa Bagamoyo Port vs Lamu Port na wengi wenu mlichangia kea mihemko na kejeli, hivi hamkujua conditions za mkataba huo? Jiwe alikuwa wapi nyakati zile ati Sasa amekuwa ndiye mwokozi? Sasa wengi waliounga mkono ujenzi ule Sasa pia wanaupinga na kumuunga mkono mhusika mkuu katika mkataba wa Bagamoyo.
 
Mi nasema haya yote ni sababu ya udhaifu na unafiki wa wabunge wetu ,mambo ya hovyo yanapitishwa wao hawaoji wanabaki kusifia na kugonga meza na kushangilia na kupongeza,hatuwezi pata ufanisi wowote kwa bunge Kama la ndugai ambae hajui vipengele vya masharti ya mkataba wa bagamoyo,
 
Ameongea kwa uchungu mwingi hadi nimemhurumia mzee wa watu, sio kwa wawekezaji, sio kwa Watanzania, kila mtu mpigaji. Makajanja wa Dar walikwenda Bagamoyo wakatia kapuni mabilioni ya hela na kuwaacha wazawa na wakazi wa Bagamoyo mikono mitupu, nao wawekezaji wanaonekana kuja na masharti ya kiajabu ajabu.

Lakini tatizo hamsemi kimoja mueleweke nini sababu haswa za kusitishaa huo mradi, maana hapa rais amesema mengi ambayo hayajawahi kutajwa kati ya yote ambayo huwa mnayasema, halafu kama kweli hajaongeza chumvi, then ina maana rais Kikwete alikua anairubuni nchi yenu, kama kweli Kikwete alikubaliana na yote hayo yaliyotajwa humo, aisei nitamshangaa sana huyo rais wenu wa zamani, alikua ameipokeza nchi kwa watu mchana peupe.
Japo pia ni vigumu kuamini ukweli bila kuskliza upande wa pili, maana kila siku tunaskia ya nyie, hatujaskia naye muwekezaji kama kweli alikua na masharti kama hayo ya kuikoloni na kuifilisi nchi ya Tanzania.
Huo ndio ukweli aliepita kafanya mengi sana ambayo hata kutaja hapa aibu yaani... Kikubwa kilikuwa kikundi cha kibinafsi kisichojali watanzania wala future ya nchii..
So wakenya mkiona tunamtetea magu msiseme eti tunamwogopa si hatumwogopi ila tunajitahidi tusimvunje moyo maana hata kama anakosea vitu vidogo Dogo BT anachofanya kwa hii nchii acheni tu huyu jaama anauchungu na nchi hii
 
Back
Top Bottom