Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka

Nyie watu mkoje? Hivi hili swali si lilitetewa bungeni? Yaani sijui hamna akili ama huwa mnajitoa akili. Irene kwani alikuwa anapanga mwenyewe bila ya kupitisha kwa wenye mamlaka ya kutunga kanuni?

Kikokotoo hutengenezwa na Waziri mwenye dhamana, mkurugenzi wa SSRA hausiki!
Sasa irene alipaswa kujenga hoja na kuzuia hili hata kama angeshindwa ila at least angejaribu...hatutaki watu wa kufuata kila wanachoambiwa bila kutumia akili zao.. pale sio jeshini
 
[emoji23]
[emoji23]
[emoji23]
[emoji23]
[emoji23]
mbuzi wa kafara
 
Kama unapata shida kuona kosa lake ngoja nikupe mfano huu: Umempa mkandarasi mkataba wa kujenga nyumba. Baadae ukakabidhiwa nyumba yako na kuichukua. Baada ya siku mbili nyumba ikapasuka ufa! Je mkandarasi hatawajibika kwa sababu tu wewe ulikubali kuipokea ile nyumba?
Mfano wako haufanani na hali halisi hata kidogo!
 
Hivi ndugu mbona unajitoa ufahamu. Unajua kazi ya mkurugenzi? Kwa kifupi mkurugenzi anakuwa ndiyo injini ya shirika.. kwa kutumia wataalam wake anawajibika kutoa maamuzi sahihi. Haijalishi kama aliyapitisha kwa rais au nani lakini baadae yakionekana hayana manufaa YEYE ndiye mwajibikaji!

Umesema vizuri sana kumpotosha Rais. Wako wengi sana wanao save 5th government with the spirit of the 4th goverment na ni janga kwa taifa hili.
 
Mapema leo Rais Magufuli alifanya kikao cha wazi na Viongozi waTUCTA, watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSSF na NSSF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA) kujadili masuala yahusuyo Mafao ya wafanyakazi hususani KIKOKOTOO na Rais Magufuli alifikia hitimisho kwamba Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika).
Pia soma
> Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika) - JamiiForums
Ni fundisho kwa watendaji wengine wenye roho mbaya za kuwakandamiza watumishi wa umaa maana bado ktk baadhi ya taasisi za serikali kuna viongozi wanawakatisha tamaa watumishi watiifu kwa nchi yao.
Hakika Rais Magufuli ni muokozi wa wanyonge wote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom