Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA), Dkt. Irene Isaka

Kama unapata shida kuona kosa lake ngoja nikupe mfano huu: Umempa mkandarasi mkataba wa kujenga nyumba. Baadae ukakabidhiwa nyumba yako na kuichukua. Baada ya siku mbili nyumba ikapasuka ufa! Je mkandarasi hatawajibika kwa sababu tu wewe ulikubali kuipokea ile nyumba?
Inategemea. Kuna watu wakiwa wanajenga nyumba utasema wao ndo mafundi, wanaelekeza kila kitu. Ss Kama alikuambia tutumie cement, nondo na matofali ya aina flani ukamwambia No tumia ya aina ninayotaka mm na ukamnunulia ukapeleka, halafu ukampangia na ajenge kwa ratio gani ule Ufa Utakuwa unakuhusu wewe sema unaweza mlaumu tu sababu yeye Ndo mkandarasi.
Kuhusu huyu aliyesimamishwa kazi ni sawa, hata mm ningemsimamisha maana utetezi wa 25 to 20% kwe runinga sijui alitumia nn kufikiri.
 
ANGETENGUA NA WALIOFUTA FAO LA KUJITOA.
UNAACHISHWA/KUACHA KAZI LEO UKIWA UMECHANGIA MILLION 5,LAKINI KUICHUKUA UNAAMBIWA BAADA YA MIAKA 15 AU 20,HIVI MILLION TANO YA LEO BAADA YA MIAKA 10 ITAKUWA NA THAMANI ILEILE?MAANA HATA FAIDA HUPEWI!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Desemba, 2018 ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Dkt. Irene Isaka.

Mapema leo Rais Magufuli alifanya kikao cha wazi na Viongozi waTUCTA, watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSSF na NSSF) na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii(SSRA) kujadili masuala yahusuyo Mafao ya wafanyakazi hususani KIKOKOTOO na Rais Magufuli alifikia hitimisho kwamba Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika).
Pia soma
> Rais Magufuli aamuru Kikokotoo kilichokuwa kinatumiwa awali kiendelee hadi 2023 (kulingana na mfuko husika) - JamiiForums
Pole yake huyu mrembo , lakin naamini Ni kambuzi ka kafara tu haka , wahusika wakubwa wanapeta

Mfano , muhagama anasubiri nini
 
Labda wakurugenzi kwenye nchi za watu wenye akili zao ila sio hapa.Uyo kwa vyovyote vile katolewa kafara kufichania ovu iliyokuwepo kwasababu hili jambo sio laleo na kwasababu hata ingetokea toka mwanzo angegoma bado angeambiwa kakiuka maagizo halali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na ndiyo somo nalofundisha kwenye thread hii. Bora uweke legacy nzuri kuliko mbaya! Simama upande wenye haki hata kama utakufa kwa njaa kuliko upande wa dhuluma huku unashiba!
 
Huyu Dada masikini naona katolewa kafala kupitia komedi hii ambayo steering wake ana uwezo mdogo sana,

Eti baada ya stone kuzungumza na wahusika vyama vya wafanyakazi wanaimba na kushangilia.

Eti viongozi pamoja na wanachama Wa mifuko ya wafanyakazi huko mwanza wameandamana wakiwa na mabango makubwa yaliyochapishwa ya kumsifia stone dakika chache baada ya jiwe kutoa tamko lake. Mwenye akili anaweza kutambu ni nani ni teering Wa hii fake movie.
IMG_20181228_210009_991.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu anaangalia sura za kutumbua ,

Mfano ... Muhagama , makonda etc
 
Sasa irene alipaswa kujenga hoja na kuzuia hili hata kama angeshindwa ila at least angejaribu...hatutaki watu wa kufuata kila wanachoambiwa bila kutumia akili zao.. pale sio jeshini
Ivi unafikiri ni rahisi kihivyo kwenda tofauti na waliokuteua.au mabosi zako muulizeni mwanasheria wa Zanzibar wa kipindi kile ilikuwaje. Huyu ni mbuxi katolewa kafara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom