Rais Magufuli atengua uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dkt. Ave Maria Semakafu

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dkt. Ave Maria Semakafu

Naibu katibu mkuu anatenguliwa wanaachwa katibu mkuu na waziri wakati tangazo lilikuwa la kisera

Huyu Mama alikuwa mwanaharakati wa kwenye midahalo ya TVs enzi hizo Rais kasema lipuuzwe hao ni maadui zetu. Huwezi jua katumika kwa kuchomekea tu maneno twa hujuma katika tamko. Mbinu za kusabotage ziko nyingi hasa kipindi hiki amvacho wale wanao mhujumu JPM wanavyo jaribu kufurukuta.
 
Amezikumbuka sarakasi zake za kutatua tatizo baada ya kulitengeneza
Terrrible! kucheka kuko karibu na kulia. Kwa mkulu unacheka akigeuka unalia! Wengi walicheka ghafla wakalia waliolia kisha wakacheka kwa mkulu ni wachache. Ndio maana wengi wamechagua unafiki na kujikomba

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nilishaona kwamba huyu mama yuko hatarini tangia sera ilivyotenguliwa kwa simu mchana huu na kwenye uzi mwingine nikamshauri Dkt. Semakafu ajiuzulu kuliko kusubiri kutumbuliwa.
Ina maana waziri hahusiki, katibu mkuu hahisiki?

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Maamuzi mazito kama yale ni ngumu kuwa maamuzi bila Baraka toka juu, anawatumia wenzake kama mpira
Halafu kwenye ilani ya CCM wanayo hiyo sera ya kufuta astashahada kwa walimu wa shule za msingi.

Nakuwekea hapa kwa marejeo
IMG-20201005-WA0017.jpg


Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Huyu Mama alikuwa mwanaharakati wa kwenye midahalo ya TVs enzi hizo Rais kasema lipuuzwe hao ni maadui zetu. Huwezi jua katumika kwa kuchomekea tu maneno twa hujuma katika tamko. Mbinu za kusabotage ziko nyingi hasa kipindi hiki amvacho wale wanao mhujumu JPM wanavyo jaribu kufurukuta.
Na kwenye ilani kachomekewa na kina nani? Bashiru au Polepole?

Hizi conspiracy theories hazina mashiko hii issue ni kama tu ya kikokotoo mzee, huyu mzee akishinda itarudi tu kwa utekelezaji, just wait and see, timing tu labda ndio imekua mbaya.
 
Na kwenye ilani kachomekewa na kina nani? Bashiru au pole pole?

Hizi conspiracy theories hazina mashiko hii issue ni kama tu ya kikokotoo mzee, huyu mzee akishinda itarudi tu kwa utekelezaji, just wait and see, timing tu labda ndio imekua mbaya.

Wewe hujui ilani inachomekea mpaka 50M kila kijiji hesabu isiyo wezekana kutekelezeka kivitendo. Mkapa alikiri hadhara ilani haitekelezeki.

Hujui ilani inaandikwa na Watu, pengine katibu muhutasi namluki. Hujui Naibu jatibu huyu kama mtaalanu wa wizara anaweza kuombwa alete andiko kwa ajili ya matumizi ya ilani?
 
Pole mama, mambo ndiyo hivyo - yale yale ya Dr. Ndugulile.
 
Amezoea kutoa wenzake kafara wakati wakitekeleza wajibu wao kwa taratibu za kiserikali yule mama alikuwa anatangaza maamuzi kwa mambo yaliyokwisha amriwa.
 
Denmark ya tandale [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji625][emoji1241]
Hiyo hiyo endelea kula miguu ya kuku na utumbo wa kuku hapo bongo
Wivu utakuua wewe
 
Kabisa! Huyu mama katolewa kafara. Uamuzi wa kubadili sera usingeweza kufanyika bila ridhaa ya baraza la mawaziri ambapo Rais ni mwenyekiti, wizara inatekeleza tu.

Sasa hapa eti tunaaminishwa kwamba uamuzi huo ulifanya na NAIBU katibu mkuu? Wala sio katibu mkuu au naibu waziri au waziri? Hizi hadaa nyingine hapana..
Hivi kumbe tuko wengi nchi hii wenye kuona dizaini hizi za changa la macho eeh. Maana haiwezekani just naibu waziri aje na maamuzi mazito kama haya. Jamaa dizaini yake imekua ni hii hii ya kutengeneza tatizo na kuja hadharani kwa nguvu kubwa sana na kulitatua ili wale wanaoitwa "wanyonge" na watawala wajione wana mtetezi!!!!
 
Daah waraka wa Dkt Ave Maria umetoka tarehe 5 na taarifa ya utenguzi wake nao tarehe 5!! kazi ipo!!kwani huo waraka Dkt Ave kaibuka nao bila maridhiano na kurugenzi zinazohusika na elimu ya msingi? Hii kafara , POLE DKT
 
Kinachochanganya, amesema ni wapumbavu na wabaya wetu - wapuuzwe! Kila linaloonekana baya ni kusingizia wabaya wao? Nasikia kuna na mkuu wa wilaya fulani uteuzi wake umetenguliwa! Tutaona na kusikia mengi
 
Nimesikitishwa kweli kuona tabia zilezile, kufukuzana HOVYO. Naibu Katibu Mkuu, hakukurupuka nijambo ambalo lilijadiliwa na wizara mpaka kufika hayo maamuzi. Leo alieandika kwa kutoka taarifa ya maamuzi ya kikao anasulubiwa. Haki iko wapi kwa watumishi.

Kwaajiri yakutaguta kura, ndo haya yote yanatokea. Utafikiri walimu wanajaliwa sana hapa nchini, kumbe sivyo. Walimu wataseka miaka nenda rudi, vimishahara vuduchu na venyewe havijapandishwa miaka nenda rudi. Rais dili na maslahi ya watumumishi, kufukuza watu sio jawabu, na nie walimu, akiri kichwani mwenu, hizi sarakasi ni zakuwafariji tuu.

Huu ni uonevu wa hali ya juu kwa Naibu katibu mkuu wa wizara. Vipi mawaziri na Katibu mkuu wa wizara husika? Maana nao walijua na kulibariki hili. Haki itendeke kwa wote tafadhali. Lakini hata busara tuu ingetumika kwa watumishi husika. Wangeamuliwa kufuta barua ya awali na mambo yakaendelea.

Ila kwa sifa za Jiwe ndo tumbua tumbua yote hii bila huruma. Daa! Poleni sana watumishi, kazi munayo.
 
Aliahidi ajira 13,000 za walimu. Akajikuta uwezo wa kuwalipa na kampeni hizi ni mdogo. Aliamua kutoa kisingizio cha kutoajiri walimu wa vyeti baadae akaona itamharibia kisiasa ná uchaguzi huu.
Haiwezekani Dr. Ave Maria Semakafu akurupuke na kutoa tangazo aliloliotoa ambalo limemwingiza katika matatizo. Ni wazi kwamba suala hili lilijadiliwa kwizarani na azimio hilo kufikiwa.

Alichofanya Dr. Semakafu ni kutangaza tu. Ni wazi kwamba Waziri Joyce Ndalichalo analifahamu suala hili hata katibu Mkuu wa Wizara analifahamu. Kwa nini aliyechinjwa ni mmoja tu?
 
Elitwege anasemaje kuhusiana na hii mada??
 
Haiwezekani Dr. Ave Maria Semakafu akurupuke na kutoa tangazo aliloliotoa ambalo limemwingiza katika matatizo. Ni wazi kwamba suala hili lilijadiliwa kwizarani na azimio hilo kufikiwa. Alichofanya Dr. Semakafu ni kutangaza tu. Ni wazi kwamba Waziri Joyce Ndalichalo analifahamu suala hili hata katibu Mkuu wa Wizara analifahamu. Kwa nini aliyechinjwa ni mmoja tu?
Ni kweli kabisa Dr Ave Maria amekua mbuzi wa kafara.
 
Back
Top Bottom