Rais Magufuli awataka TRA kuwashughulikia wafanyabiashara wanaohujumu uchumi kwa kutoa risiti za uongo

Sababu wanaijua na wewe unaijua! Wafanyabiashara wanataka kupata faida kubwa sana.
 
Kuna kila dalili chungu (hazina) kimeishiwa. Mapato yamepungua sana, sasa anatafutwa mchawi.
 
kuna uwezekano wa Tanzania Kukusanya Kodi Kubwa Tu na wafanya Biashara na TRA wakawa na amani na furaha katika utendaji wa majukumu yao.Kuna matatizo Kwenye idara za Serikali pamoja na TRA,ambayo kama ayatofanyiwa kazi tutabaki na lawama kila kukicha,EFD ni chanzo cha mapato Kiduchu na Kila kukicha tutaendelea kukusanya Kodi ndogo ,atuwezi kuongeza mapato hapa nchini kwa mfumo uliopo sasa ndani ya TRA .kwa nyakati tofauti,tofauti nimejaribu kuonana na kushauri hili kwa wahusika,awasikilizi !Why China wanakozalisha 80% EFD machines awazitumii kukusanyia kodi? Why Kenya wana EFD lakini awana Songombingo kama TZ?,Why USA,UK na India no drama kwenye ukusanyaji wa kodi?kule Bandalini ile metered Fuel Pump ipo na inafanya kazi?au bado meli zinashusha mafuta kwa kukadiria??Mungu ibariki Tanzania🙏
 
Ila ukae ukijua hao hao wengi wanao kwepa kodi ndio wanao kimbiza mzunguko wa pesa mtaan kwa sababu ndio wanao fanya hata makontena bandarin haya kai sana. ila hili utaligundua ukiwa na jicho la kiuchumi.
 
Hivi wafanyabiasha kwanini hamtaki kutoa receipt za mashine ya EFD mfanyapo mauzo?
Sheria ya kodi inasema kuwa mfanyabiashara atatozwa kodi ya mwaka kutokana na mauzo yake ndani mwaka(siyo katika faida).
Mamlaka ya mapato inatambua mauzo yako ya mwaka kupitia rekodi ya risiti ulizotoa kwa kupitia hiyo mashine ya EFD.

Wafanyabiashara hawatoi risiti za EFD kupunguza hesabu za mauzo yao ya mwaka ili mwisho wa siku walipe kodi nafuu.
 

Nchi kama India kodi inakusanywa kabla bidhaa haijaingia sokoni. Bidhaa zote madukani zinakuwa na bei elekezi imeshachapwa katika bidhaa husika.
 
Wakati mwingine ni uhuni au ni serikali yenyewe inachangia hilo tatizo kuwepo, lkn wasomali wamezidi yuko tayari asikuuzie kisa umetaka risiti, hapo ndipo ninapofikiri serikali ilikosea au inahitaji marekebisho kila mfanyabiashara alipe VAT na ikifanya hivyo hilo tatizo litaisha, mara nyingi anayeitaji risti ni yule mlipaji wa VAT kama mfanyabiashara halipi VAT hana habari na mambo ya risti.
 
Serikali yenyewe kuna mahala inakwepa kodi utadhani katika nchi hii kuna nchi mbili au kuna mahala kuna msamaha, angalia; kwa jiji la dar es salaam hauwezi kufanya biashara na idara ya serikali kama wewe hujaasajiriwa na VAT lkn kwa mikoani hasa kwenye Halmashauri wewe uliyesajiriwa na VAT ukipereka bei zako zenye VAT unafukuzwa kama mbwa labda kwa kazi flanflan kubwa hizo wanakubali kulipa kodi/ VAT, sasa kwa mazingira kama hayo uoni serikali ndiyo inayoshawishi watu wakwepe kodi?
 
Bunge lipi linapanga na kupitisha sheria? Sheria zote zinapangwa na kupitishwa na wizara, huko bungeni ni rubber stamp tu.
Mkuu hufahamu sheria huwa zinatungwa bungeni?
Wizara huwa zinatoka mapendekezo ambayo huwenda Kama miswada na kujadiliwa na kuwa sheria .
Had we had smart bunge hii miswada mibovu ingekuwa inakwama bungeni kabla ya kuwa sheria ,
 
Atupatiege risiti ya ile 1.5T kwanza ili twendage sawa 😌 ~ aliskika mlevi mmoja toka kilabu cha pombe maeneo ya Mbalizi.
 
Mfanyabiashara kukwepa kukipa kodi eliwa kuna Tatizo sehem.

Ebu fikiria, bidhaa kuwa imported inalipiwa impotation tax n clearance, unapoisafirisha kuifikisha sokoni kuna transit tax, ukifika kwa wholesaler anauziwa na VAT inakatwa. Wholesalers naye kuja kumuuzia retailer VAT inakatwa. Retailer naye kumuuzia consumer VAT inakatwa apo bado hajalipa mapato na kodi ya jiji.

Mfanyabiashara anayefata njia zote hizi mwisho wa siku anayeumia ni final consumer ambao ni sisi wanyonge.

Ndyomaana bidhaa za supermarket bei huwa juu sababu jia zote za kulipa ushuru zinafatwa ila wanyonge wanakimbilia mmbidhaa za vichochoroni ila unakuta ni zile zile
 
Kodi kimantiki inamgusa zaidi mtu wa mwisho yaani mimi na wewe, kwa kiasi fulani mfanyabiashara kwanza lielewe hilo!
Wanachogoma wafanya biashara ni mazingira ya kufanya biashara na mteja ambaye hana uwezo wa kumudu ongezeko la kodi.,
Mfanyabiashara hata ukimtoza kodi kubwa ana uwezo wa ku bypass gharama zote zikaenda kwa mtu wa mwisho na yeye asiumie .
 
Biashara ni maelewano baina ya muuzaji na mnunuzi. Hivi ni mteja gani atakayekataa kupunguziwa bei kwa masharti ya kupewa risiti inayoficha kiwango halisi kilicholipwa? Serikali ni lazima waangalie upya utitiri na viwango vya kodi.
 
Naam..!! Kwa mantiki hii wafanyabiashara ndo watetezi bali serikali inawakamua walaji. Je, mlaji ana uwezo wa kubeba mzigo wa kodi?
 
Mwisho wa siku BEI ZA VITU ZITAPANDA..
hyo VAT utailipa wewe
Hajui !!! Vat ni kodi kwa mlaji wa mwisho, wafanyabiashara sio kwamba wanaiogopa Vat , bali huyo mlipaji mwenyewe ndio chokambaya.

Kodi kutolipika inaanza kwanza na umasikini wa mtanzania
 
We waache tu.
sisi wafanyabiashara tutapiga 18% zetu.tutakuongezea kwenye BEI.
tutakupa risiti yako.
KAAAAMILI.
Hajui !!! Vat ni kodi kwa mlaji wa mwisho, wafanyabiashara sio kwamba wanaiogopa Vat , bali huyo mlipaji mwenyewe ndio chokambaya.

Kodi kutolipika inaanza kwanza na umasikini wa mtanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…