Rais Magufuli awatumbua Kitila Mkumbo, Ole Sendeka na Katambi, awateua Jumanne Fhika, Dr. Aloyce Nzuki, Allan Kijazi, Josephat Paulo, Kemikimba

Rais Magufuli awatumbua Kitila Mkumbo, Ole Sendeka na Katambi, awateua Jumanne Fhika, Dr. Aloyce Nzuki, Allan Kijazi, Josephat Paulo, Kemikimba

serikalini hata ukiwa unafanyakazi ofisi kumi huwa unalipwa mshahara mmoja tu. Mfano, waziri huwa ni mbunge, angeweza kulipwa mshahara Wa ubunge na Wa uwaziri Ila ukishakuwa waziri unaondolewa kwenye payroll ya bunge, unabaki kulipwa wizarani tu. Bungeni atakuwa analipwa posho za vikao tu. Kwa ishu ya kijazi itaangaliwa kati ya wizarani na Tanapa wapi analipwa mshahara mkubwa, kama ni Tanapa ataendelea na mshahara Wa huko, kama Wa wizara ni mkubwa atalipwa Wa wizara.
Apo nimekupata sawa sawa Shukrani sana 🤝
 
Magufuli aache watu wawe huru kufanya watakalo muhimu wasimuharibie kazi, huwezi kumfungia mtu ndani kama mbuzi, sio siku zote mtu afanye unalotaka wewe tu, huu nao ni udikteta.

Kwa muendelezo huu ataendelea kuteua wapya kila siku, vyema ajifunze kuheshimu taratibu alizozikuta, asitake kubadilisha kila kitu.
Mbona hajawakataza, alichofanya ni kutoa angalizo kwamba ukitaka ubunge lazima uachie nafasi uliyonayo. lakini pia kwa utitiri wa watia nia ilikuwa ni busara kwa hawa wateuliwa kubaki na nafasi zao kwa sababu wao siyo bora kuliko watia nia wengine.

Tegemea ulichokishika mkononi, usitegemee utakachotafuta. Unaweza kufanya vizuri kwenye nafasi uliyopewa na ikaonekana na baadaye ukawa promoted to the next level.
 
Ni matumizi tu mabaya ya kodi zetu. Badala ya kuteua Wataalamu, unawateua Wanasiasa wenzako! Unategemea nini muda wa kufanya hiyo siasa utakapofika/utakapowadia? Ni lazima tu wakukimbie ili wakatafute malisho ya uhakika.

Na tutamshangaa sana Rais iwapo atawateua tena watu wa aina hii iwapo watashindwa kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya chama au hata kushindwa kabisa kwenye huo uchaguzi mkuu ujao.
umeshaambiwa vigezo ni kujua kusoma na kuandika zaidi sana kuwa ccm

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Katambi hana base yoyoye Shinyanga mjini na hajulikani maana 2015 alibebwa tu na nguvu ya Chadema.
Pale mjini GAKI, Fresho na Kwilasa ndio wanaamua mbunge awe nani

Na utamu zaidi GAK(Gaspar Kileo) nae anagombea mwaka huu hataki kunwaga hela zake tu anaona bora ajimwagie mwenyewe.

Chupi zinabana🤣🤣
 
Huu ni uonevu nadhani kuanzia ngazi fulani,mbona kuna baadhi ya mawaziri kabisa tena ngazi za juu wao hatengii uwaziri wao sasa kama ni hivyo
watu wanachanganya.. Uwaziri siyo sehemu ya utumishi wa Umma. Uwaziri ni Cheo cha kisiasa, ndo maana mtu asipokuwa mbunge Rais akitaka amchague kuwa waziri lazima amchague kwanza kuwa mbunge.. lakini Ukurugenzi, ukuu wa wilaya, ukuu wa mkoa n.k ni utumishi wa Umma moja kwa moja Mhusika kama siyo likizo anapaswa awepo kazini kila siku za kazi, Rais akijisikia anaweza kupangua wizara na kuzipunguza kutoka 40 zikabaki hata 20.. lakini wilaya ikizhaundwa au mkoa Rais hawezi kuamka na kusema leo Amefuta mikoa 10, hivyo waziri yeyote ni Mwanasiasa automatically, hivyo kugombea ubunge ni sehemu ya sifa ya kwanza..

JamiiForums mobile app
 
Ni matumizi tu mabaya ya kodi zetu. Badala ya kuteua Wataalamu, unawateua Wanasiasa wenzako! Unategemea nini muda wa kufanya hiyo siasa utakapofika/utakapowadia? Ni lazima tu wakukimbie ili wakatafute malisho ya uhakika.

Na tutamshangaa sana Rais iwapo atawateua tena watu wa aina hii iwapo watashindwa kwenye mchakato wa kura za maoni ndani ya chama au hata kushindwa kabisa kwenye huo uchaguzi mkuu ujao.
Na ndio upungufu ninao uona. Hajaacha kuteua wana siasa. Kateua makada kibao wa CCM kuwa DED, DAS na RC. Acha maisha yaendelee
 
Magufuli aache watu wawe huru kufanya watakalo muhimu wasimuharibie kazi, huwezi kumfungia mtu ndani kama mbuzi, sio siku zote mtu afanye unalotaka wewe tu, huu nao ni udikteta.

Kwa muendelezo huu ataendelea kuteua wapya kila siku, vyema ajifunze kuheshimu taratibu alizozikuta, asitake kubadilisha kila kitu.
Wewe fikiria Hadi Jana walioomba kupitia CCM Ni elfu nane Kati Yao elfu 6 ni watumishi wa umma hivi unataka ofisi za serikali afanye kazi Nani? Magufuli Yuko sahihi ku replace angeruhusu ungekuta wafanyakazi wa umma laki mbili wanataka ubunge ofisi wameacha tupu hazina wa kuhudumia wako foleni ya kuchukua fomu za uteuzi
 
Wewe fikiria Hadi Jana walioomba kupitia CCM Ni elfu themanini Kati Yao elfu 60 ni watumishi wa umma hivi unataka ofisi za serikali afanye kazi Nani? Magufuli Yuko sahihi ku replace angeruhusu ungekuta wafanyakazi wa umma laki mbili wanataka ubunge ofisi wameacha tupu hazina wa kuhudumia wako foleni ya kuchukua fomu za uteuzi
Kwa uongo uko vizuri,watu elfu themanini unawajua wewe lkn?
 
Wao ktk teuzi siwaoni kabisa au wapo Kenya siku hizi
Be dynamic.. wakibana huku unatokea kwingine.

Ona sasa Msukuma mwenzako anasema Gaspar Kileo na Fred Shoo ndio wanaamua Mbunge wa Shinyanga Mjini awe nani hahahaha...
 
Kijazi wa TANAPA ameteuliwa kua Naibu katibu Mkuu Wizara ya Mali asili huku akiendelea pia na u-boss wake pale TANAPA.

Hao ndio wenye nchi sasa,wanyonge walie na umaskini wao tu.
Prof. Mkenda Ina maana naye kaenda kugombea ubunge au katumbuliwa?
 
watu wanachanganya.. Uwaziri siyo sehemu ya utumishi wa Umma. Uwaziri ni Cheo cha kisiasa, ndo maana mtu asipokuwa mbunge Rais akitaka amchague kuwa waziri lazima amchague kwanza kuwa mbunge.. lakini Ukurugenzi, ukuu wa wilaya, ukuu wa mkoa n.k ni utumishi wa Umma moja kwa moja Mhusika kama siyo likizo anapaswa awepo kazini kila siku za kazi, Rais akijisikia anaweza kupangua wizara na kuzipunguza kutoka 40 zikabaki hata 20.. lakini wilaya ikizhaundwa au mkoa Rais hawezi kuamka na kusema leo Amefuta mikoa 10, hivyo waziri yeyote ni Mwanasiasa automatically, hivyo kugombea ubunge ni sehemu ya sifa ya kwanza..

JamiiForums mobile app
Ahaa sawa
 
Hizi Ni dharau kwa mwenyekiti wao, kwamba pamoja na angalizo alilolitoa bado wanamuona si lolote si chochote.

Ngoja tuone Kama Mwenyekiti wao atawalamba miguu kwa kuruhusu uteuzi wao, maana alishawapiga ban wasithubutu
Kujua hii game inahitaji uwaze nje ya box,kama unawaza ndani ya box comment ni kama ulivyoileta
 
Mimi naona mwenyekiti na yeye wangemzuia kugombea mimi naisi asingefika hapo alipo hii ni kuzuia demokrasia.
Angekuwa mwl huko kwao sengerema hadi muda huu.. anasubiri mafao yake nssf na kadi yake ya benki kwa wakopeshaji wa mtaani.
 
Kumbe wana mdharau Mwenyekiti kiwango hiki, yaani ingekuwa mimi ni Mh. Mwenyekiti JPM, wote walioacha kazi serikalini kuanzia Katibu Mkuu, PS, RC, RAS, DC, DAS, DED, CEO, MD, DPS, wotee wenye vyeo vikubwa na wakaachia ni tamaa kubwa, majina yakija kwangu nakata yote, itakuwa funzo kubwa kwa wengine. Yaani naamini Mh. Rais alilisema sana hili, wenye tamaa kama Mwananzila atawakata wote. Tusubiri tuone, hii ni dharau kubwa ya wazi wanafanya kwa Mwenyekiti
 
Kumbe wana mdharau Mwenyekiti kiwango hiki, yaani ingekuwa mimi ni Mh. Mwenyekiti JPM, wote walioacha kazi serikalini majina yakija kwangu nakata yote, itakuwa funzo kubwa kwa wengine. Yaani naamini Mh. Rais alilisema sana hili, wenye tamaa kama Mwananzila atawakata wote. Tusubiri tuone, hii ni dharau kubwa ya wazi wanafanya kwa Mwenyekiti
Yeye alipokua mwalimu mbona hakuridhika na cheo chake akaenda kugombea ubunge?Ni tamaa au?
 
Back
Top Bottom