Rais Magufuli awatumbua Kitila Mkumbo, Ole Sendeka na Katambi, awateua Jumanne Fhika, Dr. Aloyce Nzuki, Allan Kijazi, Josephat Paulo, Kemikimba

Rais Magufuli awatumbua Kitila Mkumbo, Ole Sendeka na Katambi, awateua Jumanne Fhika, Dr. Aloyce Nzuki, Allan Kijazi, Josephat Paulo, Kemikimba

Magufuli aache watu wawe huru kufanya watakalo muhimu wasimuharibie kazi, huwezi kumfungia mtu ndani kama mbuzi, sio siku zote mtu afanye unalotaka wewe tu, huu nao ni udikteta.

Kwa muendelezo huu ataendelea kuteua wapya kila siku, vyema ajifunze kuheshimu taratibu alizozikuta, asitake kubadilisha kila kitu.
Jifunzeni kuridhika.
 
Siwezi kushangaa, kampeni zake 2015 alisema kwny serikali yake mtu akiharibu sehemu moja kamwe hatahamishiwa sehemu nyingine atamfukuza tu.

Lakini tumeona kwa Mwigulu, Simbachawene, Kamishina Andengenye aliwaponda balaa wkt wa kuwatumbua ila baadae akawarudisha serikalini na kuwapa vyeo huku akisema ni wazalendo haswaa.
Hili ni suala la kutunza kumbukumbu tu...
Wengi tumeshasahau hayo tunasonga mbere...
Maendeleo hayana chama!!
 
Ualimu ni cheo kidogo sana serikalini, hivyo sio tamaa kugombea, ila PS, DPS, RC, RAS, DC, DAS, DED ni tamaa kabisa, na mm najua Mh. Rais akisema hageuki, alisema anawasubiri, uzuri majina yatamfikia, subiri tuone, sbb wameonyesha dharau kubwa sana aisee
Hageuki?Mbona alisema kwny serikali yake mtu akiharibu sehemu moja atamtumbua tu,mambo ya kumhamishia sehemu nyingine marufuku.

Akawatumbua Mwigulu,Simbachawene,Kamishina Andengenye akiwaponda balaa lkn akawarudisha tena akisema wao ni wazalendo sana na wachapa kazi.

Achana na maneno ya wanasiasa mzee baba.
 
Ukitumia akili vizuri, ubunge miaka 5 tu unatosha kutoka kimaisha. Mambo mengine ni stress tupu ndiyo maana watu wanaona isiwe tabu.
Wasipopitishwa je?
Ile kauli "...heri kenda chukua kuliko kumi nenda rudi!!" Ikatimia.
Ni WALAFI NA WANA TAMAA YA FISI...
AIDHA KUNA UDHAIFU KATIKA UTENDAJI WAO "HAWATUFAI" Na katika hili namuunga mkono Namba moja wetu.
 
Kumbe hawamuogopi tena
Uncle haaaaa umenikasirisha sana , jamaa mwaka wa 20 anendelea kuwa mbunge wetu, anafikia record ya Babu Msuya. Yaani sisi wana Mwanga kama mazezeta. Suburi uone LINARUDI. Bado nipo kijijini Kirongwe. Kuna sehemu jamaa ikipigwa kampeni anaenda, kama kata ya Msangeni, Mwaniko, Ngujini na Kifula. sehemu zingine linakubalika.
 
Wasipopitishwa je?
Ile kauli "...heri kenda chukua kuliko kumi nenda rudi!!" Ikatimia.
Ni WALAFI NA WANA TAMAA YA FISI...
AIDHA KUNA UDHAIFU KATIKA UTENDAJI WAO "HAWATUFAI" Na katika hili namuunga mkono Namba moja wetu.
Wasipopitishwa si basi.
Bado dhana ipo palepale kuwa ubunge unalipa.
 
Haya yaliwahi kutokea tawala zilizopita, mtu ni mbunge, mkuu wa mkoa nk
Enzi za JK Engineer Stella Manyanya alishakamata vyeo hivyo vyote alikua ni Mbunge,Naibu waziri na RC hapohapo.
 
Uncle haaaaa umenikasirisha sana , jamaa mwaka wa 20 anendelea kuwa mbunge wetu, anafikia record ya Msuya. Yaani sisi wana Mwanga kama mazezeta. Suburi uone LINARUDI. Bado nipo kijijini Kirongwe. Kuna sehemu jama ikipigwa kampeni anaenda kama kata ya Msangeni, Mwaniko, Ngujini na Kifula. sehemu zingine anakubalika.
Tulia, tulia, tulia, tutaongea kwa kirefu
 
Ni usanii tu, anatuzuga kuwa hajawapa baadhi ya wateule wake baraka za kugombea wakati wana go ahead yake.

Siamini kama Kitila anaweza kugombea bila kupewa go ahead!
Mbona alishasema atakayeomba ruhusa atapewa na kumnyima ruhusa ni kutenda dhambi kubwa
 
Magufuli aache watu wawe huru kufanya watakalo muhimu wasimuharibie kazi, huwezi kumfungia mtu ndani kama mbuzi, sio siku zote mtu afanye unalotaka wewe tu, huu nao ni udikteta.

Kwa muendelezo huu ataendelea kuteua wapya kila siku, vyema ajifunze kuheshimu taratibu alizozikuta, asitake kubadilisha kila kitu.
Nakuona pinga pinga kila kitu.

Wahenga walisema'MSHIKA MAWILI MOJA UMPORONYOKA". Hii misemo ya WAHENGA haikuja kwa bahati mbaya yakheee.
 
Back
Top Bottom