Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Wiaslamu tumechelewa katika hilo.Hatuna jeuri wala ujasiri wa kulikemea hilo leo.Reginald Mengi alifuatwa na akachangia misikiti mingi wakati wa Mwinyi.Juzi Kigoma Diamond Platinum,mwanamuziki (haramu katika Uislamu,Mzinzi (kwa ushahidi wa kuwa na watoto nje ya ndoa)kajenga msikiti n akaukabidhi huku akiambatana na kimada.
Hospitali za Misheni zinatibia watu wote bila kubagua.
Kwa hili,msimlaumu JPM amefanya kile kilichomsukuma kukifanya.
Waislamu tujitafakari.
Wajitafakari kwa lipi sasa?,waislamu ndo jamii zenye nyumba za ibada zenye haliya kiwango kikubwa,,kuna jamii bado wanasali kwenye vibanda vya trubai na salfeti.

Kuchangia ujenzi msikiti,au kanisa sio ishu ya ajabu kiasi cha kuhitaji mjadala
 
Fact
Kama Yesu Kristo wakati wa mateso yake alianguka mara tatu, basi huyo Askofu Mkuu, Paroko na Katibu wa Baraza la Maaskofu, walianguka pia kuchangisha fedha ya kujenga/ kukarabati msikiti ndani ya Kanisa kwa sababu zisizo za msingi kabisa. Sasa sijui kama wamekwisha inuka.
Michango ya msikiti ilibidi ifanyike kwenye eneo la msikiti na wao kualikwa.
 
Rais ni wa wote wewe acha majungu,Rais angekua muislam na akachangisha hivi msikitini dhidi ya waKristo wala usingesema na usingesikia waKristo wanaongea maneno,mmekaa kiukorofi korofi tu,hilo siyo tendo la kudharauliwa isipokua ni tendo la kuunganisha ummoja wa wananchi na kuondoa udini au ukabila

Tumia akili
 
Jiwe kachanga karata zake vibaya. Kwa tafsiri nyepesi Waumini wa Imani nyingine wataona ni udhalilishaji wa Imani yao kwani matamshi yale yalitolewa Kanisani na siyo Msikitini wala kwenye Mkutano wa Hadhara.
 
Rais ni wa wote wewe acha majungu,Rais angekua muislam na akachangisha hivi msikitini dhidi ya waKristo wala usingesema na usingesikia waKristo wanaongea maneno,mmekaa kiukorofi korofi tu,hilo siyo tendo la kudharauliwa isipokua ni tendo la kuunganisha ummoja wa wananchi na kuondoa udini au ukabila

Tumia akili

Hakuna mtu anaweza kuja msikitini kuomba waislamu watoe mchango wa ujenzi wa kanisa akifanya hivyo ataombwa kwa heshima zote aache kulizungumzia hilo msikitini.
 
Maoni yako ni sahihi ila jitahidi kupanua uelewa wako. Few months ago huko ujerumani waislam waliwaomba wakristu wawaruhusu waislam kufanya ibada ya ijumaa kanisani kwakuwa misikiti ilikuwa midogo kuruhusu social distancing because of covid. Waislam waliswalia kanisani
 
Nadhani hapo alianza kurekebisha makosa ya gwajiboy kule kawe! kumbe nae kalikoroga?
 
Maoni yako ni sahihi ila jitahidi kupanua uelewa wako. Few months ago huko ujerumani waislam waliwaomba wakristu wawaruhusu waislam kufanya ibada ya ijumaa kanisani kwakuwa misikiti ilikuwa midogo kuruhusu social distancing because of covid. Waislam waliswalia kanisani

Huko Ulaya, waislamu wenyewe waliomba!

It came from the muslims themselves for what they thought is better for them, not otherway around!
 
Msaidizi wake ni Alhaj na kiubinadamu anajisikia vibaya kuwa na waislam kadhaa kanisani halafu wasiwe na msikiti katika eneo lao la kazi.

Samia Suluhu, Kassim Majaliwa na wengine wasaidizi wa karibu ni waislam hivyo mkumbuke umuhimu wao kwake kimaisha.

Msiongozwe na chuki mpaka mkapoteza uwezo wa kuyatafakari masuala ya kawaida kabisa ya kiubinadamu.

Hapo Chamwino ni sehemu ya Dodoma na ni makao makuu kutakuwa na ongezeko la waislam miaka ijayo.
 
Missile of the Nation,

Rais, Askofu Mkuu na Katibu wao TEC ni full maigizo. Wameleta kinyaa. Watumie hizo fedha sasa kununua vifaa vyao kanisani Kama kinanda kikubwa, viti, mabenchi na hata Noah ya Paroko kuliko kuharibu Sunnah ya misikiti wa Kiislamu.
Ni kampeni kabisa ile siku! hata alimnadi mteuliwa wa ubunge!! sasa hao wa huo msikiti watapokea au sheikh mkuu atapokea na kuikabidhi!!
 
Mnisaidie, kuna papa mmoja aliombwa vipaza sauti na waislamu na aliwapa kupitia kwa mwakilishi wake hapa Tz.

Kifupi kama waliomba wanastahili kusaidiwa. Hujenga umoja wa kitaifa na kudumishs mshikamano.

Haijalishi mkusanyaji ni mwislamu au mkristo. Wakatae wao waislam kama hawahitaji. Lengo ni msikiti wa makao makuu ujengwe, tuabudu kila mmoja kwa imani yake.
 
Waislamu waliomba!

It came from the muslims themselves for what they thought is better for them, not otherway around!

Misri katika ule mtaa mkuu kutoka uwanja wa ndege kuna msikiti upo karibu kabisa na kanisa na hali imekuwa hivyo miaka na miaka.

Mada yako imekosa mizania inayotokana na tafiti za kiulimwengu.
 
Mnisaidie, kuna papa mmoja aliombwa vipaza sauti na waislamu na aliwapa kupitia kwa mwakilishi wake hapa Tz.

Kifupi kama waliomba wanastahili kusaidiwa. Hujenga umoja wa kitaifa na kudumishs mshikamano.

Haijalishi mkusanyaji ni mwislamu au mkristo. Wakatae wao waislam kama hawahitaji. Lengo ni msikiti wa makao makuu ujengwe, tuabudu kila mmoja kwa imani yake.

Mleta mada kasahau kuwa upande wa pili wa mada yake unaweza kumuonyesha yeye kama ni mtu mbaguzi asiyetambua kuwa utanzania msingi wake mkuu ni kuvumiliana kati ya dini mbili kongwe.
 
Magufuli analeta dhana za Church Supremacy nchini, ana portray kuwa waislamu hawawezi kufanya mambo yao wenyewe mpaka huruma ya kanisa!

Ile kitu waislamu wanaita Mfumo Kristo baadhi ya dalili za kukomaa kwake ndiyo hizi!

Fikra zako ni potofu na ni za hatari. Mkapa aliyebadili matumizi ya chuo Morogoro ili waislam wawe na chuo kikuu cha kwao alikuwa ana portray church supremacy?.
 
Back
Top Bottom