Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Misri katika ule mtaa mkuu kutoka uwanja wa ndege kuna msikiti upo karibu kabisa na kanisa na hali imekuwa hivyo miaka na miaka.

Mada yako imekosa mizania inayotokana na tafiti za kiulimwengu.

Msikiti kuwa karibu na kanisa siyo tatizo hata kidogo, ipo misikiti mingi tu duniani imejengwa na inapakana na makanisa

Tatizo ni Rais wa nchi, tena wa imani nyingine, kwenda katika nyumba yake ya ibada na kisha kutaka sadaka za waumini wenzie kanisani zikajenge msikiti.

Kama waislamu wenyewe wangemuomba aendeshe harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wangeweza kumualika msikitini au kwenye uwanja wa wazi akapewa muongozo na waislamu wa namna ya kuendesha zoezi hilo!

La sivyo alivyofanya Magufuli ni kujivisha jambo ambalo si la dini yake kwa malengo yake binafsi (naamini ni ya kisiasa)
 
Ndio. allah sio Yehova. allah ni mmoja wa miungu tulioambiwa. " msiabudu miungu mingine ila Mimi."
 
Una ushahidi gani kama Rais hajaamua kufanya tukio lile kwa maombi ya hao hao waislam?.

Kwa taarifa yako wasaidizi muhimu wa Rais ni waislam, kazungukwa na waislam hivyo wanamwambia umuhimu wa Chamwino kuwa na msikiti.

Kumbuka kuwa Marehemu Mkapa na Nyerere hawakuwahi kuhudhuria zile shughuli za kuhifadhi Quran lakini JPM amehudhuria.
 
Hahaha mleta mada anasagau tu su anajisahaulisha, misikiti mingi sana imejengwa kwa kuchangiwa na waumiju wa madhehebu ya kikristo.

Faiza Foxy alisema eti ikulu ya magogoni ilijengwa na waislam, nikacheka sans.
Waislamu hawahawa wanaojengewa misikiti?!
 
Mnampaisha Tundu Lisu kwa lipi? Jamaa ni failure hata kabla ya uchaguzi kuanza rasmi.

Lissu ni Mwanaharakati makini, Ni Mwanasheria Nguli, ni Wakili Msomi, alikuwa ni Mbunge Machachari, Ni kiumbe jasiri! Hastahili kupaishwa na mtu yoyote yule! Anajipaisha mwenyewe.
 
Misri katika ule mtaa mkuu kutoka uwanja wa ndege kuna msikiti upo karibu kabisa na kanisa na hali imekuwa hivyo miaka na miaka.

Mada yako imekosa mizania inayotokana na tafiti za kiulimwengu.
Mkuu katika hili umesoma vizuri? Au mimi kuna sentensi sikuziona? Sijaona akizungumzia suala la kanisa kuwa karibu na msikiti. Hii ipo hata Daslama pale Magomeni ambapo upande wa pili kuna kanisa. Nilichokiona anzungumzia Magufuli, rais wa jamhuri, kuwaombea waislamu mchango wa kujenga msikiti. Maombi yenyewe yaliyofanywa kwa wakristo ndani au katika maeneo ya nyumba yao ya ibada na zaidi wakati huu tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu.
 

Msikiti upi hapa nchini ulijengwa kwa michango ya wakiristo ukiachilia mbali huu ambao Magufuli anataka kiki za kisiasa?
 
Ni kweli hata wakristo wanawaita waislamu ni wapagani kwamba hawana dini.
Kila dini inajiona wao ndo wako sawa,,iwe walokole,budha,hindu etc,,wala haipaswi kuwa mjadala,kwasisi tunaoabudu imani za jadi,huwa tunawachora tu na kubaki kuwasikitikia jinsi mnavyopoteza mda.
 
Kama mnakosoa harambee iliyofanyika baada ya mkuu wa nchi kuona kuna hitaji hilo, mbona pia alishafanya harambee kwa kumuomba mfalme wa Morocco kujenga msikiti mkubwa Afrika Mashariki na msikiti unaendelea kujenga na kama sikosei mwaka huu unafunguliwa?? Acheni roho za kichadema muwe wakweli msiwe wanafiki. Waislamu hawana tatizo na hilo isipokuwa wale wenye chuki binafsi na jemedali JPM. Yaani ni hivi hamtashinda kwa uovu huu
 
Kwani hicho chuo kabla ya kupewa waislamu kilikuwa ni taasisi ya dini gani?
Tanesco Morogoro, achana na hii dhana ya kibaguzi JPM hajaanza jana wala juzi kuwa karibu na waislam.

Bashiru Ali Kakurwa
Kassim Majaliwa
Samia Suluhu Hassan

Hao ni wasaidizi wake tena wa karibu sana, ni lazima nafsi imsukume ili na wao wakiwa Chamwino wawezwe kuswali.

Miaka ile ya Mwalimu Nyerere pengine halikuwepo wazo la kujenga msikiti lakini kumbuka ni miaka ya 1970 na 80 leo ni karne tofauti kabisa.
 
Kweny Uislam Sadaka haimtazami mtoaji bali dhamira na uhalali wa umiliki kile ulichotoa

Hata uwe Sheikh au Mufti kama Sadaka yako ina malengo labda ya kisiasa au kuleta zahma kwny Jamii au mali hiyo ya sadaka imetokana na dhulma basi sadaka hiyo ni Void

Wakati wa Bwana Mtume kuna Msikiti uliamriwa uvunjwe baada ya kujengwa kwa kuwa tu dhamira haikuwa njema ya Wajenzi

So kwny Uislam hata unapotoa Sadaka kwa Asie Muislam kwa dhamira safi ya kumsaidia kuondokana na shida zake unapata thawabu
Kwahiyo asiye muislamu kuchangia msikiti ni dhambi bwashee?
 
Mi naona rais hajakosea kitu maana anapofanya harambee za ghafla iwe kumsaidia kwa mfano yule mama kilema pale ubungo flyover kila msaidizi wake anachangia. Akichangisha kanisani wote wasaidizi wake bila kujali dini wanatoa. Kama rais amejihusisha kujengwa kanisa eneo la ikulu hivyohivyo amejihusisha kuchangisha kwa msikiti wa eneo la ikulu. Utamaduni wa watanzania kuchangiana kwa ujenzi nyumba za ibada umeanza siku nyingi na hii ni moja ya sifa za watanzania.
 
Ukisoma between lines - mwandishi - Ana chuki isiyopimika dhidi ya wakatoliki.
Mwandishi anaumia sana kumuona Rais anatoa sadaka kanisani.

Hili la kuchangiana si hoja yake ya msingi. Ila imempa upenyo tu kuventi chuki yake dhidi ya wakatoliki.

Rais ni kiongozi wa nchi. Anaongoza wakristo, waislam na hata wasio na dini.
Ana jukumu la kuwaunganisha wote waishi kindugu, kuthaminiana, kuheshimiana na kusaidiana.

Mwandishi asingetumia chuki yake dhidi ya ukatoliki angeweza kuiona dhamira njema ya Rais kutuunganisha na kutufanya tuishi kitanzania - tukipendana na kushirikiana bila kujali tofauti zetu kiimani, kikabila nk.
Sisi ni WATANZANIA na ni NDUGU.
 
Ndugu zangu, Amani iwe juu yenu pamekuwepo na madai na majitapo mengi kutoka kwa baadhi ya political laymen tangu jana baada ya baba mwenye nyumba kutembeza bakuli kanisani kuomba fedhwa za kujenga msikiti.

Hapo nina maswali mawili matatu.

Moja, Baba mwenye nyumba alitumwa na masheikh kuwaombea michango kanisani, bila shaka mamlaka za waislamu zitatujulisha.

Pili, Je ni upendo wa baba mwenye nyumba kwa wapangaji wake kutaka kuonesha religious equilibrium katika kipindi hiki cha kutafuta political pasture?, sina hakika sana kama iko hivyo.

Tatu, Ni uumini na uchamungu wa kiwango cha juu cha baba mwenye nyumba?, nadhani hili ni jibu sahihi.

Nne, Ni ipi hukumu ya kisheria katika dini ya uislamu kujenga msikiti kwa fedhwa ambazo yakinani zimetokea kanisani bila wasiwasi wowote?

Hapo maulama watatusaidia

Tano, Je hili halina athari yoyote kisiasa khasa wakati huu wa uchaguzi?

Sita, Ni lini msikiti wa mfalme wa Moroko utazinduliwa nao waislamu wachangie kanisa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…