Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Acha kumuumbua mtukufu, alifanya hivyo kukusanya kura, anataka kujionyesha kua yeye habagui dini wala chama.
Alafu mkishampa kura atarudi kuwaambia mtajijua wenyewe
 
Ujinga tu..kwani ukienda kusali hapo utasali kwa kwa kuwa msikiti ukichangiwa na wakristo ama utasali kama muumini thabiti wa iman yako!?

Acha upopoma boss..
 
Hebu imagine haya anayofanya Rais Magufuli yangefanywa na rais Muislamu, hali ingekuwaje?
Kwani aliyofanya Rais Magufuli kwa ajili ya waislamu yana tatizo gani? Mwaka 1990 Papa John Paul alitembelea Tanzania wakati Rais alikuwa Hassan Mwinyi, ambaye ni Muislamu.

Kulikuwa na mkakati wa kuchangisha hela kwa ajili ya mapokezi hayo. Rais Mwinyi alijumuika katika kuhamasisha michango na kati ya vitu alivyofanya ni kunadi picha yake akiwa na mtu yo yote atakayetoa dau kubwa zaidi katika mnada huo. Picha hiyo ilinunuliwa na mtu ninayemfahamu kwa Shilingi milioni moja za wakati huo.

Rais Mwinyi na yule aliyenunua picha hiyo bado wako hai. Unaweza kufuatilia habari hii kama unataka. Hiyo milioni moja haikuwa kwa ajili ya uzuri wa picha bali kwa kuwa tu mtu alitaka kuchangia katika shughuli hiyo. Sasa tuseme Rais Mwinyi aliharibu kama Muislamu kuingilia mambo ya Kikatoliki? Vivyo hivyo kwa Rais Magufuli. Tusilaumu kwa sababu ya kulaumu tu.
 
Na wale tunaowakutaga had nje ya ma gate yetu na mabakuli wakiomba hela na kusema ya kujenga msikiti vip.tusiwe tunawapa au sio....

Muslim buana...
 
Msikiti haujengwi na pesa ya kafiri
NYIE NI WANAFIKI SANA.........NIMEAMINI HILO SABABU HAKUNA KIPINDI KIGUMU CHA BIASHARA YANGU YA KITIMOTO KAMA KIPINDI CHA MFUNGO WA RAMADHANI.....WAISLAMU NDIYO WATEJA WANGU WAKUBWA NA POMBE WANAPIGA KAMA KAWA.....ILA SASA HUKO PEMBENI WANANIITA KAFIRI.....INAWEZEKANA WEWE PIA NI MTEJA MKUBWA WA KITIMOTO.......MAKAFIRI TUNA RUN SHOW...KARIBU
 

Rais Mwinyi aliendesha hiyo harambee msikitini?
 
Kuna maeneo nmengi ambayo unaweza kukuta uislam hasa wa Tanzania haujiwezi, na umekuwa ukisaidiwa
Hakuna hiyo kitu.

Kule ni kujitoa kimasomaso tu, masheikh ambao ndio walimu wa kuwafundisha waislam kujua uislam wao wananyanyaswa na kuteswa kila Leo halafu tunazungumzia upendo????
 
Wengi wao wamereact kwa sababu ya udini walionao yani hawa watu wako sensitive na dini yao utadhani dini ndio tiketi ya kufika mbinguni wakati wataiacha hapa hapa duniani
 
Wakatoliki wamewachukia wapi waislam? na waislam wamewachukia wapi wakristo/wakatoliki?
Au mnapenda tu waanze kuchukiana?
 
Haya yote muhusika ni BAKWATA.
 
Nimesoma hadi mwisho sijaruka kipengele chochote, japo sikujua kinachoendelea lakini umeelezea vizuri nikapata mwanga,

Binafsi nakazia kwa msumari yote uliyoyaandika, Dini isichanganywe na Siasa.
Ni kweli. Si halali kabisa kufanya siasa madhabahuni
 
Masheikh?? Kama Alhadi? Au Maaskofu kama Gwajima???

Hivi nyie akili zenu zinafikiria ki namna gani??
Mimi huwa nasikiliza kile ambacho mtu anasema, huwa siangalii mtu kwanza halafu ndiyo niamue kumsikiliza au kutomsikiliza. Huwa nasikiliza kwanza bila kujali kimetoka kwa nani. Hata wewe pia naweza kukusikiliza. Hekima iko midomoni mwa watu, na si kwenye umardidadi wa maumbile yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…