Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Acha kumuumbua mtukufu, alifanya hivyo kukusanya kura, anataka kujionyesha kua yeye habagui dini wala chama.
Alafu mkishampa kura atarudi kuwaambia mtajijua wenyewe
 
Ujinga tu..kwani ukienda kusali hapo utasali kwa kwa kuwa msikiti ukichangiwa na wakristo ama utasali kama muumini thabiti wa iman yako!?

Acha upopoma boss..
 
Hebu imagine haya anayofanya Rais Magufuli yangefanywa na rais Muislamu, hali ingekuwaje?
Kwani aliyofanya Rais Magufuli kwa ajili ya waislamu yana tatizo gani? Mwaka 1990 Papa John Paul alitembelea Tanzania wakati Rais alikuwa Hassan Mwinyi, ambaye ni Muislamu.

Kulikuwa na mkakati wa kuchangisha hela kwa ajili ya mapokezi hayo. Rais Mwinyi alijumuika katika kuhamasisha michango na kati ya vitu alivyofanya ni kunadi picha yake akiwa na mtu yo yote atakayetoa dau kubwa zaidi katika mnada huo. Picha hiyo ilinunuliwa na mtu ninayemfahamu kwa Shilingi milioni moja za wakati huo.

Rais Mwinyi na yule aliyenunua picha hiyo bado wako hai. Unaweza kufuatilia habari hii kama unataka. Hiyo milioni moja haikuwa kwa ajili ya uzuri wa picha bali kwa kuwa tu mtu alitaka kuchangia katika shughuli hiyo. Sasa tuseme Rais Mwinyi aliharibu kama Muislamu kuingilia mambo ya Kikatoliki? Vivyo hivyo kwa Rais Magufuli. Tusilaumu kwa sababu ya kulaumu tu.
 
Na wale tunaowakutaga had nje ya ma gate yetu na mabakuli wakiomba hela na kusema ya kujenga msikiti vip.tusiwe tunawapa au sio....

Muslim buana...
 
Msikiti haujengwi na pesa ya kafiri
NYIE NI WANAFIKI SANA.........NIMEAMINI HILO SABABU HAKUNA KIPINDI KIGUMU CHA BIASHARA YANGU YA KITIMOTO KAMA KIPINDI CHA MFUNGO WA RAMADHANI.....WAISLAMU NDIYO WATEJA WANGU WAKUBWA NA POMBE WANAPIGA KAMA KAWA.....ILA SASA HUKO PEMBENI WANANIITA KAFIRI.....INAWEZEKANA WEWE PIA NI MTEJA MKUBWA WA KITIMOTO.......MAKAFIRI TUNA RUN SHOW...KARIBU
 
Kwani aliyofanya Rais Magufuli kwa ajili ya waislamu yana tatizo gani? Mwaka 1990 Papa John Paul alitembelea Tanzania wakati Rais alikuwa Hassan Mwinyi, ambaye ni Muislamu. Kulikuwa na mkakati wa kuchangisha hela kwa ajili ya mapokezi hayo. Rais Mwinyi alijumuika katika kuhamasisha michango na kati ya vitu alivyofanya ni kunadi picha yake akiwa na mtu yo yote atakayetoa dau kubwa zaidi katika mnada huo. Picha hiyo ilinunuliwa na mtu ninayemfahamu kwa Shilingi milioni moja za wakati huo. Rais Mwinyi na yule aliyenunua picha hiyo bado wako hai. Unaweza kufuatilia habari hii kama unataka. Hiyo milioni moja haikuwa kwa ajili ya uzuri wa picha bali kwa kuwa tu mtu alitaka kuchangia katika shughuli hiyo. Sasa tuseme Rais Mwinyi aliharibu kama Muislamu kuingilia mambo ya Kikatoliki? Vivyo hivyo kwa Rais Magufuli. Tusilaumu kwa sababu ya kulaumu tu.

Rais Mwinyi aliendesha hiyo harambee msikitini?
 
Kuna maeneo nmengi ambayo unaweza kukuta uislam hasa wa Tanzania haujiwezi, na umekuwa ukisaidiwa
Hakuna hiyo kitu.

Kule ni kujitoa kimasomaso tu, masheikh ambao ndio walimu wa kuwafundisha waislam kujua uislam wao wananyanyaswa na kuteswa kila Leo halafu tunazungumzia upendo????
 
Mungu akubariki ndugu, nchi hii Kwa udini haijambo, ukiona dini yako imeweka mbele ubaguzi jiulize mara mia je haya ni mapenzi ya Mungu. Ubaguzi unaleta laana mbaya sana ndio maana wabaguzi wengi huwa hawastawi, Tazama mazingira yako kati ya wabaguzi na wabaguliwa ni wangapi wamefanikiwa zaidi Kwa idadi, jibu baki nalo mwenyewe, kuanzia uongozi Wa nchi, idadi ya watu, wasomi, wenye pesa.
Wengi wao wamereact kwa sababu ya udini walionao yani hawa watu wako sensitive na dini yao utadhani dini ndio tiketi ya kufika mbinguni wakati wataiacha hapa hapa duniani
 
There is no way, again there is no way and never there will be mapenzi ya wakristo kwa waislam

Qur an imeshasema zamani sana mambo haya.

Walipofikia waislam wa Tanzania moja ya chanzo ni chuki ya wakristo hususan wakatoliki dhidi ya waislam.

Mengi sana yashasemwa juu ya hili na hakuna na hakutokuwepo mapenzi haya yanayoonyeshwa isipokuwa ni jambo/mambo tu yanafanywa kwa maslahi flani
Wakatoliki wamewachukia wapi waislam? na waislam wamewachukia wapi wakristo/wakatoliki?
Au mnapenda tu waanze kuchukiana?
 
Ndugu rais, wewe ni Rais siyo sheikh, wewe ni Mkiristu siyo Muislamu, mambo ya Waislamu waachie Waislamu wenyewe!

Una haki ya kuchangisha fedha kwa ajili ya matendo ya imani yako lakini huna haki ya kusimama ndani ya nyumba ya imani yako kudictate kipi kifanywe kwa niaba ya watu wa imani nyingine.

Waislamu wana taratibu zao za kujenga nyumba za Ibada zao, wanachangia wao wenyewe au wanatafuta mfadhili wa imani yao wao wenyewe, au wanafanya kwa kufuata taratibu za dini yao, kisha wanajenga msikiti wao!

Umewahi kusikia wapi Waislamu nchini wameendesha harambee makanisani kwa ajili ya kupata pesa kwa ajili ya kujenga misikiti yao? Au unafikiri Waislamu hawana marafiki Wakiristo wakiwemo maaskofu na mapadre ambao wangeweza kuwaomba wawafanyie harambee wajenge hizo nyumba?

Au lini umewahi kusikia maaskofu na mapadre wameomba michango kupitia misikitini ili Waislamu wachangie ujenzi wa makanisa?

Kuna mambo ni boundary ya kuheshimiana kiimani, nayo ni kutokuingiliana katika namna kila imani inavyoendesha mambo yake!

Najua pengine kibinadamu uliona aibu kutokana na mihela mirefu unayoimwaga makanisani siku hizi kwa jina la sadaka, ukahisi labda umma wa Waislamu utakuona kama mtu anayetumia mafungu yale ya urais yasiyokaguliwa na yeyote kwa ajili ya sadaka hizo, mimi nasema usihofu, maadamu wewe ni Mkatoliki na Mkiristu basi usiuonee haya Ukiristo wako wewe toa tu, Waislamu wanajiweza, wanaweza kujenga misikiti yao wao wenyewe na infact misikiti nchi hii ni mingi kwelikweli na imejengwa na Waislamu wao wenyewe!

Kuhusu misikiti iliyojengwa na Wafalme na marais, hiyo Waislamu tunajua huwa wanatafuta hao wafadhili wao wenyewe, ila sasa kwa kuwa Kiprotokali jambo linalofanywa na mfalme au rais wa Taifa moja katika jingine lazima mfalme au rais wa taifa husika awe na taarifa ndiyo maana taasisi za dini zinaweza kukujulisha ili usaidie kunyoosha mambo! Hii ni tofauti na kwenda kanisani ukaanzisha harambee ya kujenga misikiti! Ndugu Rais ulitumwa au kuombwa na Muislamu gani kutaka kujenga msikiti kupitia fedha za kanisani?

Wakati mwingine naangalia haya mambo na kuona kuwa yamekaa kisiasa. Hata hivyo mambo ya dini ni sensitive sana si vizuri kuchanganya dini na siasa! Mwalimu alionya sana kuhusu mambo haya!

Ipo namna mtu asiye muislamu anavyoweza kuguswa na kuamua kujenga msikiti, kwa mfano, Mwalimu aliguswa moyoni mwake baada ya kustaafu uraisi akaamua kutafuta fedha za kujenga Msikiti Butiama, Mwalimu alikuwa na connection za Vatican, Makanisa makubwa makubwa lakini hakwenda kutafuta fedha makanisani ili ajenge msikiti, Mwalimu alikwenda kwa Ghadafi ndiye aliyempa pesa za kujenga Msikiti huko Butiama!

Nimkumbushe tu ndugu Magufuli kuwa, dini ya Kiislamu pia imeweka misingi ya aina gani ya misikiti inafaa kuswaliwa ndani yake, Quran inasema ile misikiti iliyojengwa kwa dhamira safi ndiyo misikiti ya Mungu na ndiyo inayofaa kuswaliwa bali ile iliyojengwa kwa dhamira isiyo njema, yenye malengomalengo fulani hivi hiyo haina baraka za Mungu na haifai kuswaliwa ndani yake!

Nashauri Ndugu Rais awe makini sana na haya mambo ya dini, haya ni mazito sana, akiyakosea yataiweka heshima nzima ya taasisi ya urais rehani halafu kuja kurekebisha taswira hiyo inaweza kutumia gharama kubwa.

MAMBO YA WAISLAMU WAACHIWE WAISLAMU WENYEWE. NDUGU RAIS FANYA YALE YA IMANI YAKO AU YALE UTAKAYOOMBWA UFANYE KAMA UKIPENDA!
Haya yote muhusika ni BAKWATA.
 
Nimesoma hadi mwisho sijaruka kipengele chochote, japo sikujua kinachoendelea lakini umeelezea vizuri nikapata mwanga,

Binafsi nakazia kwa msumari yote uliyoyaandika, Dini isichanganywe na Siasa.
Ni kweli. Si halali kabisa kufanya siasa madhabahuni
 
Masheikh?? Kama Alhadi? Au Maaskofu kama Gwajima???

Hivi nyie akili zenu zinafikiria ki namna gani??
Mimi huwa nasikiliza kile ambacho mtu anasema, huwa siangalii mtu kwanza halafu ndiyo niamue kumsikiliza au kutomsikiliza. Huwa nasikiliza kwanza bila kujali kimetoka kwa nani. Hata wewe pia naweza kukusikiliza. Hekima iko midomoni mwa watu, na si kwenye umardidadi wa maumbile yao
 
Back
Top Bottom