Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Ni kweli unavyosema nadhani washauri wake ndio wanamuongoza vibaya, yote ni propaganda za kampeni wamuone kuwa anawajali na yuko pamoja naye huku akisahau kuwa si njia sahihi ya kuhamasisha michango ya ujenzi wa waislamu sasa sijui itakuwaje kama Masheikh wataupokea huo mchango au la maana tayari umehamasihwa kwa njia isiyo sahihi.
 
Mkuu ulikuwa unatakiwa utafakari kwa kina na kwa mapana kabla ya kuleta hili bandiko, Hakuna logic Kabisa kwenye bandiko lako, mwaka Jana nikiwa safarini kwenda Tanga kutokea Bagamoyo, tulipofika Handeni alipanda mtu mmoja kwenye gari yetu baada ya hapo akajitambulisha Kama kiongozi wa dini ya kisilaam kutoka eneo fulani huko handeni, akesema yeye anaomba mchango wa kusaidia kukamilisha ujenzi wa msikiti na kuanza ujenzi wa madrasa, je kwenye hizo hela alizopewa siku hiyo kwenye Basi, za wakrisito hazikuwemo???

Kingine fahamu kazi ya kiongozi ni kutatua changamoto na kero za raia wake rais alikuwa specific Kabisa kuelezea kuwa kuna watumishi anafanya nao kazi lkn sehemu yao ya ibada ni ndogo, kwahiyo inahitajika zaidi ya hiyo, halfu Mbona alisema pia Rostam alichangia ujenzi wa kanisa je hilo nalo watu waache kwenda kwenye hilo jengo kisa muisalamu katoa hela, pia kutoa ni moyo, Kama ni hivyo hiyo ni sadaka, sadaka yaweza kutumika kumsaidia yeyote yule.

Halfu mambo ya kutuambia sijui msikiti unajengwa kwa hela sijui Safi au chafu, riba imejaa na kutapakaa duniani, ni misikiti mingapi imejengwa kwa hela za riba? Au riba sio Haramu?
 
We mtoa post umekosea sana na udini unakusumbua,nataka tu kukukumbusha kwamba Rais ni kiongozi wa nchi na nchi haina dini
Unakumbuka mwaka 2011 mbowe alipochangisha pesa za kukarabati msikiti kule hai mlivyomshambulia mkiongozwa na bwakata mkoa wa kilimanjaro kuwa haikuwa sahihi mbowe kuchangisha pesa na kutangaza? Tena alichangisha kwenye swala ya ijumaa, huyu kachangisha kwenye misa kanisani tena TV ya taifa na channel 10 wakiwa live lakini mnashangilia.
 
Hakuna ubaya kuchangishana kujenga nyumba za ibada,,ili wakazi wa maeneo hayo nao wapate pa kuabudia
Unakumbuka mwaka 2011 mbowe alipochangisha pesa za kukarabati msikiti kule hai mlivyomshambulia mkiongozwa na bwakata mkoa wa kilimanjaro kuwa haikuwa sahihi mbowe kuchangisha pesa na kutangaza? Tena alichangisha kwenye swala ya ijumaa, huyu kachangisha kwenye misa kanisani tena TV ya taifa na channel 10 wakiwa live lakini mnashangilia.
 
Hahaha mkiachwana eneo bila kuchangiwa hamtajenga na eneo linaweza kuleta migogoro baadaye mkamsumbua sheikh Ponda kuanza kufuatilia mali za waislamu.

Jamani kuweni na shukrani kawaombea pesa huyo rais.

Hivi uliisha shuhudia ngumi msikitini wewe, kwamba moja ya viongozi wa msikiti anashutumiwa kula pesa za misaada?!

Binafsi naona ni jambo la kawaida kabisa na hajaanza yeye, hata Lowassa enzi zake kafanya sana hizi.

Juzi hapa Nakonda alikuwa anazunguka mchana na usiku kuwaomnbea pesa mjengewe msikiti na ofisi za bakwata.

Kusema asante tu hamuwezi?! Hahaha nyie kiboko.
 
Mimi sijawahi kumshambulia mbowe,kwa ishu hiyo,,mbowe ni mmoja wa wanasiasa wazuri kabisa,,kama kuna mtu alimshambulia kwa suala hilo,itakuwa vilikua vijembe vya kisiasa tu..
 

Kwahiyo kila atakae kwenda Ikulu atajenga kanisa lake why government inajichanganya hivi?.
Rais unachanganya watanzania . Kuruhusu Roman Catholic liwe na kanisa ikulu vipi waislam vipi mathehebu mengine? Ina maana kila Rais awe anajenga ikulu makanisa na misikiti? Hili umeharibu mzee wangu.
 
Azam Dewji achangia Milion 10. Kufanikisha ujenzi wa "Nyumba Yangu" katika Harambee aliyoianzisha Mh Rais Jumapili Agosti 23 huko Chamwino.
 
Tatizo unaongea katika perspective isiyo ya kiislam.

Uislam una taratibu zake za kuendesha mambo.

Na halafu mimi nikivaa suti yangu na nkipanda kwenye basi nkianza kuchangisha huku najiita John unakuwa na uthibitisho gani kwamba mimi siwapigi tu hiyo pesa abiria?? I am not saying huyo mtu hakuwa muislam laaaa, I am just trying kujenga hoja.

Katika uislam kuna aina mbali mbali za sadaka na kila moja inayo aina ya watu wanaoistahili.

Kuna hadithi nyingi sana za Mtume zinazozungumzia watu muflis, yaani mtu aliefilisika. Ni nani huyo?? Kwa mujibu wa uislam ni yule ambae itakuja siku ya kiama na yale yote aliyoyatenda dunia kuwa ni sawasawa na vumbi tu hayastahili malipo yoyote toka kwa Allah.

Kiufupi diamond hawezi kwenda janga msikiti kwa hela yake haramu halafu eti ategemee malipo na pepo. Labda pepo ya udongo.

Huyo rostam kuchangia kanisa anafanya huku akijua kwa Mungu hapati chochote atapata tu maslahi yake ya kidunia aliyokusudia kuyapata kupitia mchango huo.

Muda mchache mambo ni mengi mkuu
 

Amejenga kasehemu ka kumsalia bikira Maria ndani ya eneo la kanisa hilo la Ikulu huko Dodoma, Sijui kama Walutheri na Walokole watapenda hiyo move ya Magufuli, ngoja tuone kama nao atawapa eneo lao kujenga makanisa yao!
 
Mbona mi nishawahi kufatwa kuombwa nichangie mikeka ya kuswalia wakati mi mkristu.
Jamaa alikua anatembea na barua kuomba mchango huo toka msikiti husika.
 
Waislamu wana taratibu zao za kujenga nyumba za Ibada zao, wanachangia wao wenyewe au wanatafuta mfadhili wa imani yao wao wenyewe, au wanafanya kwa kufuata taratibu za dini yao, kisha wanajenga msikiti wao!
Mkuu hapa haupo sahihi.
Zaidi ya mara tano wanapita hapa nyumbani kwangu na kuomba mchango wetu watu wa kamati za kukusanya michango ya ujenzi wa msikiti.
Hawaulizi dini wala jina, hapa kwangu sisi sote ni wakristo. Na sidhani kama ukitoa mchango ukaandika jina la kikristo kwenye daftari lao watakurudishia mchango wako.

Tunawaona wanakaa barabarani wanakusanya michango na hawasemi wakristo wasichangie.

Usije ukasema hawa ni walaghai hawapeleki michango msikitini sitakuamini sababu wanakuja na vibali vya kukusanya michango na tunawajua kwa sura na majna ni kweli hao ni watu wa kutoka msikiti flani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…