Sawa Sheikh! Nimekupata. Ila kuna jambo unatakiwa pia kuwashukuru hao Wakatoliki. Wamewachangia mzigo wa kutosha tu na ahadi kedekede kupitia ile harambee kwa ajili ya ujenzi wa msikiti wenu kule Chamwino.
Siku ukitembelea maeneo hayo na kuswali kwenye huo msikiti, basi usije ukasahau na Waumini wa Kikatoliki nao walishiriki kuchangia chochote ili ndugu zao Waislamu nao wapate sehemu nzuri ya ibada.
Watanzania siku zote ni wamoja. Ni hawa wanasiasa tu uchwara ndiyo wanajitahidi kutufarakanisha. Ingawa nina imani hawatafanikiwa kamwe.
NB: Usiseme tena 'kwani tuliwaomba' si kiherehere chenu tu na huyo mkatoliki mwenzenu!