Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Rais Magufuli azindua Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Emmakulata Chamwino, Dodoma. Achangisha fedha kanisani kuchangia ujenzi wa Msikiti

Kwani aliyofanya Rais Magufuli kwa ajili ya waislamu yana tatizo gani? Mwaka 1990 Papa John Paul alitembelea Tanzania wakati Rais alikuwa Hassan Mwinyi, ambaye ni Muislamu. Kulikuwa na mkakati wa kuchangisha hela kwa ajili ya mapokezi hayo. Rais Mwinyi alijumuika katika kuhamasisha michango na kati ya vitu alivyofanya ni kunadi picha yake akiwa na mtu yo yote atakayetoa dau kubwa zaidi katika mnada huo. Picha hiyo ilinunuliwa na mtu ninayemfahamu kwa Shilingi milioni moja za wakati huo. Rais Mwinyi na yule aliyenunua picha hiyo bado wako hai. Unaweza kufuatilia habari hii kama unataka. Hiyo milioni moja haikuwa kwa ajili ya uzuri wa picha bali kwa kuwa tu mtu alitaka kuchangia katika shughuli hiyo. Sasa tuseme Rais Mwinyi aliharibu kama Muislamu kuingilia mambo ya Kikatoliki? Vivyo hivyo kwa Rais Magufuli. Tusilaumu kwa sababu ya kulaumu tu.
Ndio aliharibu na huwezi jua pengine ni miongoni mwa mambo anayajutia sana sasa hivi
 
NYIE NI WANAFIKI SANA.........NIMEAMINI HILO SABABU HAKUNA KIPINDI KIGUMU CHA BIASHARA YANGU YA KITIMOTO KAMA KIPINDI CHA MFUNGO WA RAMADHANI.....WAISLAMU NDIYO WATEJA WANGU WAKUBWA NA POMBE WANAPIGA KAMA KAWA.....ILA SASA HUKO PEMBENI WANANIITA KAFIRI.....INAWEZEKANA WEWE PIA NI MTEJA MKUBWA WA KITIMOTO.......MAKAFIRI TUNA RUN SHOW...KARIBU
Wewe kweli ni kafiri
 
We mtoa post umekosea sana na udini unakusumbua,nataka tu kukukumbusha kwamba Rais ni kiongozi wa nchi na nchi haina dini
Ndio ni raisi wa nchi hivyo ana nafasi nyingi za kutafuta mahari muafaka wa kuchangia huo msikiti. Ninacho ona ana nia nzuri lakini hakuusoma mchezo vizuri au hakupata ushauri muafaka hasa wakati huu wa uchaguzi.
 
Hakuna tofauti ya kupewa chuo cha kiislam na kisaidiwa kujenga msikiti: hapakuwa na chuo cha kiislam, mkristo akawapa chuo, hakuna msikiti, wakristu wanawachangia kujenga msikiti
Kwa sababu huna ujualo mkuu kuhusu uislam.

Sorry to say
 
Hoja yako ya kwamba eti kwa kuwa limefanywa ujerumani ndio sahihi na Sisi tufuate tu ndio ninalopinga hapa.
Hoja yangu hunaielewa, hoja yangu ni kuwa Mola wako unayemwabudu aliabudiwa katika sinagogi lilojengwa na wakristu. Ima kama wewe waabudu tofauti unijulishe niache kuchangia
 
Ndugu rais, wewe ni Rais siyo sheikh, wewe ni Mkiristu siyo Muislamu, mambo ya Waislamu waachie Waislamu wenyewe!

Una haki ya kuchangisha fedha kwa ajili ya matendo ya imani yako lakini huna haki ya kusimama ndani ya nyumba ya imani yako kudictate kipi kifanywe kwa niaba ya watu wa imani nyingine.

Waislamu wana taratibu zao za kujenga nyumba za Ibada zao, wanachangia wao wenyewe au wanatafuta mfadhili wa imani yao wao wenyewe, au wanafanya kwa kufuata taratibu za dini yao, kisha wanajenga msikiti wao!

Umewahi kusikia wapi Waislamu nchini wameendesha harambee makanisani kwa ajili ya kupata pesa kwa ajili ya kujenga misikiti yao? Au unafikiri Waislamu hawana marafiki Wakiristo wakiwemo maaskofu na mapadre ambao wangeweza kuwaomba wawafanyie harambee wajenge hizo nyumba?

Au lini umewahi kusikia maaskofu na mapadre wameomba michango kupitia misikitini ili Waislamu wachangie ujenzi wa makanisa?

Kuna mambo ni boundary ya kuheshimiana kiimani, nayo ni kutokuingiliana katika namna kila imani inavyoendesha mambo yake!

Najua pengine kibinadamu uliona aibu kutokana na mihela mirefu unayoimwaga makanisani siku hizi kwa jina la sadaka, ukahisi labda umma wa Waislamu utakuona kama mtu anayetumia mafungu yale ya urais yasiyokaguliwa na yeyote kwa ajili ya sadaka hizo, mimi nasema usihofu, maadamu wewe ni Mkatoliki na Mkiristu basi usiuonee haya Ukiristo wako wewe toa tu, Waislamu wanajiweza, wanaweza kujenga misikiti yao wao wenyewe na infact misikiti nchi hii ni mingi kwelikweli na imejengwa na Waislamu wao wenyewe!

Kuhusu misikiti iliyojengwa na Wafalme na marais, hiyo Waislamu tunajua huwa wanatafuta hao wafadhili wao wenyewe, ila sasa kwa kuwa Kiprotokali jambo linalofanywa na mfalme au rais wa Taifa moja katika jingine lazima mfalme au rais wa taifa husika awe na taarifa ndiyo maana taasisi za dini zinaweza kukujulisha ili usaidie kunyoosha mambo! Hii ni tofauti na kwenda kanisani ukaanzisha harambee ya kujenga misikiti! Ndugu Rais ulitumwa au kuombwa na Muislamu gani kutaka kujenga msikiti kupitia fedha za kanisani?

Wakati mwingine naangalia haya mambo na kuona kuwa yamekaa kisiasa. Hata hivyo mambo ya dini ni sensitive sana si vizuri kuchanganya dini na siasa! Mwalimu alionya sana kuhusu mambo haya!

Ipo namna mtu asiye muislamu anavyoweza kuguswa na kuamua kujenga msikiti, kwa mfano, Mwalimu aliguswa moyoni mwake baada ya kustaafu uraisi akaamua kutafuta fedha za kujenga Msikiti Butiama, Mwalimu alikuwa na connection za Vatican, Makanisa makubwa makubwa lakini hakwenda kutafuta fedha makanisani ili ajenge msikiti, Mwalimu alikwenda kwa Ghadafi ndiye aliyempa pesa za kujenga Msikiti huko Butiama!

Nimkumbushe tu ndugu Magufuli kuwa, dini ya Kiislamu pia imeweka misingi ya aina gani ya misikiti inafaa kuswaliwa ndani yake, Quran inasema ile misikiti iliyojengwa kwa dhamira safi ndiyo misikiti ya Mungu na ndiyo inayofaa kuswaliwa bali ile iliyojengwa kwa dhamira isiyo njema, yenye malengomalengo fulani hivi hiyo haina baraka za Mungu na haifai kuswaliwa ndani yake!

Nashauri Ndugu Rais awe makini sana na haya mambo ya dini, haya ni mazito sana, akiyakosea yataiweka heshima nzima ya taasisi ya urais rehani halafu kuja kurekebisha taswira hiyo inaweza kutumia gharama kubwa.

MAMBO YA WAISLAMU WAACHIWE WAISLAMU WENYEWE. NDUGU RAIS FANYA YALE YA IMANI YAKO AU YALE UTAKAYOOMBWA UFANYE KAMA UKIPENDA!
Tena hapo haujaanza muda wa push-ups sijui ukianza badae wiki hii tutaona nini!
 
Kuna sehemu kwenye Quoran inasema " Rafiki wa muislam ni mkristo" Urafiki katika shida na raha ikiwepo kuchangiana kama ilivyo kwenye Sherehe za harusi.
 
Ndio aliharibu na huwezi jua pengine ni miongoni mwa mambo anayajutia sana sasa hivi
Kwa nini tuandikie mate na wino upo? Nimesema wote wawili, mnunuaji na muuzaji bado wako hai. Kwa nini kama unadhani muuzaji unajutia kitendo chake usifuatilie na kuujua ukweli?
 
Hapo ni kama amewadharau waisilamu na kuwafanya Matonya. Kama alitaka kuchangia msikiti si ni bora angeenda huko huko msikitini aitishe harambee, kisha awapigie simu matajiri wachangie kwa kumuogopa? Na hela isipotosha akatoe hazina. Anasakwa kura kwa mbinu za kizee.
Basi wazikatae hizo pesa tujue
 
Nia ya Rais ni kufanya Chamwino iwe na nyumba za ibada nzuri. Ila kwa wenzetu wengine kila kitu ni makosa. Rais waache maana sidhani kama kuujenga msikiti kwa harambee ni dhambi mnayoisimulia. Iweje kujenga kwa kodi za umma sio tatizo?
 
NYIE NI WANAFIKI SANA.........NIMEAMINI HILO SABABU HAKUNA KIPINDI KIGUMU CHA BIASHARA YANGU YA KITIMOTO KAMA KIPINDI CHA MFUNGO WA RAMADHANI.....WAISLAMU NDIYO WATEJA WANGU WAKUBWA NA POMBE WANAPIGA KAMA KAWA.....ILA SASA HUKO PEMBENI WANANIITA KAFIRI.....INAWEZEKANA WEWE PIA NI MTEJA MKUBWA WA KITIMOTO.......MAKAFIRI TUNA RUN SHOW...KARIBU

Astakafirulah laana kuum
 
Ha
Ushoga muulize magufuli na maige aliekufa kama wanaukubali au hawaukubali pale makonda alipoanza kupambana nao
na tunafahamu kuwa risasi zilivuruga kabisa eneo lote la kiumeni huyo ni anisi ndio maana anataka kutuletea hizo habari.
 
Ila haina shida, mbona huku mtaani huwa tunachangia 200 za kujenga MASJID ambazo zitageuzwa sunday school kwa mujibu wa Gwajima!
Sisi wakristo hata akitokea sheikh kipozeo atuchangie kujenga kanisa hatuna shida kabisa ndio maana hata bakwata ilianzishwa na wakristo na mambo yanasonga tu.
Ila mambo tunayofanya sisi wakristo laiti angefanya muislamu!
 
Wakatoliki wamewachukia wapi waislam? na waislam wamewachukia wapi wakristo/wakatoliki?
Au mnapenda tu waanze kuchukiana?
Mkuu,

With all due respect, you won't be able to see it because that how you have been PROGRAMMED.

Nenda msome mtu anaitwa SULEIMAN TAKADIR.

Au nikikwambia tu kamsome mzee Mohamed Said na maandiko yake utasema hupendi because huyo ni mdini
 
BAKWATA ni kama taasisi ya serikali. Na Magu ni kiongozi mkuu wa serikali. Sio vibaya kiongozi wa serikali kuisaidia taasisi yake

Wale waislam wenyewe kabisa, wataiunga mkono hoja yako. Ila IslamCCM watakupiga madongo sana bwana mleta hoja...

Jaribu kupiga picha msikiti unajengwa na mchango wa mgalatia kwa fedha alizopata faida kwenye biashara ya kitimoto...
Aisee, hii kali

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom