Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Rais Magufuli akijibu swali la Sojo, MNEC kutoka Songwe aliyesema kwamba ametumwa na wanasongwe kuwasemea kuwa wanasononeka pale ambapo wapinzani wanapohamia CCM na kupewa kipaumbele cha uongozi na kuwaacha wanachama ambao walikipigania chama kufa na kupona 2010-2015, wanavunjika moyo wanapoona wageni wanapita bila mbadala.Sojo ameyataja majimbo ya Momba na Tunduma.
Pia soma > Rais Magufuli: Cecil Mwambe moyo wake uko CCM, Chama kilifanya makosa makubwa kumfanyia figisu 2015
Rais Magufuli amesema hilo lilipaswa kuzungumziwa kwenye kamati ya vikao vya CCM Wilaya au Mkoa kwamba wanaokuja kule huwahitaji. Lakini chama hiki ni cha watu, kina misingi yake, kinameza watu wote. Suala hilo lizungumziwe kwenye kamati za wilaya na mikoa na mlitafutie ufumbuzi.
Rais ameongeza kuwa CCM ina watu wengi ambao walikuwa vyama vingine kama Makongoro Nyerere na Mzee Wassira ambao walikuwa NCCR Mageuzi lakini sasa hivi ni CCM damu damu. Amewataka wanaccm kuwa na mioyo ya kuvumiliana ya kumtanguliza Mungu.
Amesema labda wana wasiwasi huyu aliyekuja huenda akawashinda na ndiyo maana amekuwa aliwashinda kila mara, otherwise mngekuwa mnamshinda, sasa kwa sababu anawatandika na mlikuwa mmejiandaa na akipigiwa kura za maoni atachaguliwa na wananchi.
Rais Magufuli ameendelea kusema kuwa Tatizo moja la siasa zetu tunajiwekea vizingiti kwamba akija huyu atashinda lakini mkiachiwa ninyi hamshindi. Nafikiri meseji umenipata.
Lakini Chama hiki kinapokea watu wote ilimradi wanazingatia masharti ya chama. Sasa mkiingia kwenye grupu zenu za kuanza kubishana mbona amerudishwa huyu! Amerudishwa kwa misingi kwamba mlimzuia njia akapitia dirishani, amerudi sasa apitie mlangoni mnataka tena mumzuie!! Muwe na uvumilivu. Ningependa huyo aliyeingia aendelee kushinda ili siku moja aingie kuwa mjumbe wa NEC.
Kwani mwanamke au mme wako akikosea, siku nyingine akaja kukuomba msamaha kwani utakataa? Siyo ajabu akaja na mapenzi mazuri mazuri kuliko ya zamani amejifunza huko mbinu nyingi na mbadala, Sasa unakataa uhondo huo?. Rais amemaliza kwa kusema CCM oyeee