Uchaguzi 2020 Rais Magufuli azungumzia wapinzani wanaohamia CCM na kupewa kipaumbele cha uongozi na kugombea

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli azungumzia wapinzani wanaohamia CCM na kupewa kipaumbele cha uongozi na kugombea

Mbona Lowassa alitoka CCM akahamia CHADEMA akawania na Urais kabisa. huyo Bwana mdogo hajafaham bado nini maana ya Siasa.
 
Hekima za mwenyekiti JPM ni kubwa sana kwa jinsi alivyojibu hilo swali ukizingatia kuwa ni swali la papo kwa papo. Maana ya jibu hili ni hivi:
  1. Amewakana wale wapinzani wahamiaji ambao wamekuwa wakijitapa kuwa wamehamia CCM kwa maelekezo kutoka juu au wametumwa na viongozi wa ngazi za juu. Maana yake ni kuwa kamati za huko wilayani na mkoani ndizo zenye maamuzi kuzingatia kanuni za chama
  2. Ametahadharisha kuwa kutokea upinzani sio dhambi, kama mhamiaji amekubaliana na itikadi ya CCM na akawa tayari kuwatumikia watanzania, hakuna ubaya maana hivi vyama ni njia tu lakini lengo ni kuwatumikia watanzania.

Hongera Mwenyekiti
 
Yule jamaa sijui akirudi tunduma au momba atajisikiaje kwa haya majibu ya dr president
 
Hii inawalenga kina Prof J, Sugu, Mdee, Bulaya etc.
 
Devid Silinde ndio ameleta Songombingo lote hilo.

Tunduma Kuna watu wamejiandaa miaka mingi na wametumia gharama kubwa kama unavyojua CCM na Rushwa.

Hata hivyo hongereni CCM Tunduma kwa kujitambua, 2010-2015 mlikuwa hamuwezi kuvaa kanga na kofia na kupita barabarani likuwa aibu lakini mlivumilia.

Bila shaka mmewasilisha maoni ya majimbo mengi Sana wanayopewa wageni kisa wameunga juhudi.
 
Hekima za mwenyekiti JPM ni kubwa sana kwa jinsi alivyojibu hilo swali ukizingatia kuwa ni swali la papo kwa papo. Maana ya jibu hili ni hivi:
  1. Amewakana wale wapinzani wahamiaji ambao wamekuwa wakijitapa kuwa wamehamia CCM kwa maelekezo kutoka juu au wametumwa na viongozi wa ngazi za juu. Maana yake ni kuwa kamati za huko wilayani na mkoani ndizo zenye maamuzi kuzingatia kanuni za chama...
Wakome na tamaa zao za madaraka. Lijualikali Oyeee! Subiri ka-uDC baada ya uchaguzi.
 
CCM imekua ikifanya maamuzi mengi sana ya hovyo lakini kwa hili nadhani itakua fake news.
 
Hekima za mwenyekiti JPM ni kubwa sana kwa jinsi alivyojibu hilo swali ukizingatia kuwa ni swali la papo kwa papo. Maana ya jibu hili ni hivi:
  1. Amewakana wale wapinzani wahamiaji ambao wamekuwa wakijitapa kuwa wamehamia CCM kwa maelekezo kutoka juu au wametumwa na viongozi wa ngazi za juu. Maana yake ni kuwa kamati za huko wilayani na mkoani ndizo zenye maamuzi kuzingatia kanuni za chama
  2. Ametahadharisha kuwa kutokea upinzani sio dhambi, kama mhamiaji amekubaliana na itikadi ya CCM na akawa tayari kuwatumikia watanzania, hakuna ubaya maana hivi vyama ni njia tu lakini lengo ni kuwatumikia watanzania.

Hongera Mwenyekiti
Magufuli hajajibu swali. Amekwepa swali.

Kwa sababu, hakutakiwa kulisukuma hilo swali vikao vya chini wakati hata yeye kapokea wapinzani na kuwapa vyeo vikubwa vya ukatibu muu na unaibu waziri wizarani.

Hakujibu swali.

Kalikwepa tu.
 
Kama ni kweli basi hii ni taarifa njema kwa Wapinzani wao. Mara nyingi Ccm imekuwa ikipoteza Majimbo mengi hasa yale ya Mjini kutokana na aina hii ya migawanyiko baina yao.
Kwa ajili ya Idd Azan na Mtemvu nasikia wameanza kampeni chinichini..hao madogo waliotoka upinzani hawatakiwi ndani ya CCM
 
Back
Top Bottom