Uchaguzi 2020 Rais Magufuli: Gambo sikumfukuza Ukuu wa Mkoa bali aliniomba akagombee Ubunge baada ya kuona Arusha inakwama

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli: Gambo sikumfukuza Ukuu wa Mkoa bali aliniomba akagombee Ubunge baada ya kuona Arusha inakwama

Ila kucheza na akili ya mpiga kura nguvu kidogo sana, sasa aliyeikwamisha arusha n nani sasa
 
Kama Mrisho Gambo atanyimwa kura na watu wa Arusha anapaswa kumlaumu Magufuli.

Kama kuna mtu anadhani Magufuli amemfanyia kampeni Gambo ukweli ni kwamba amemuharibia na wananchi wataamini hawa wote wawili ni waongo na matapeli watupu.

Lema anakwenda kuwamaliza na clip za nyuma halafu atawawekea hii ya leo, kura zitakapopigwa mtakumbuka maandishi yangu.

Huyu mzee sijui ana matatizo gani huwa sielewi kabisa.
Mwambie Lema.atafite kazi nyingine ubunge asahau!
 
Kwa hulka yake, hakupaswa kuwa rais. Na kwa bahati mbaya hakuwahi kuwa na ndoto ya urais hadi pale Jakaya alipolikoroga na hivyo huyu akasukumizwa. Kwa hivyo aliingia kwa nafasi hiyo bila kuwa hata na chembe ya vision. Ndio maana tumeshuhudia vituko lakini vituko ambavyo vinamtesa na kumyanyasa mwananchi wa kawaida. Njiani amelewa pombe ya madaraka kufikia kuona pesa za serikali ni zake na waTz ni vijakazi wake anaweza akawafanyia cho chote na wasimfanye kitu, asubuhi anaweza kutoa kauli hii, jioni akasema hajaisema. Hii yote ni kuamini waTz, yaani vijakazi wake, ni wajinga na mwenye akili na busara ni yeye peke yake. Ulevi wa madaraka. Jakaya na vizazi wako mlaaniwe milele!
Kwa upuuzi ulioandika unatikiwa ufungwe jiwe kichwani alafu uzamishwe baharini.
 
Rais Magufuli amesema kuna watu wanadai anamchukia Mrisho Gambo na kwamba alimfukuza kazi ya mkuu wa mkoa wa Arusha lakini hiyo siyo kweli.

Gambo alinifata akaniomba agombee ubunge ili aiokoe Arusha ambayo inaonekana kukwama, amesema Dr Magufuli.
Ningekuwa namchukia ningempitisha kugombea ubunge? ameuliza.

Nileteeni Mrisho Gambo kwa ajili ya maendeleo ya Arusha amesisitiza Dkt. Magufuli.







Maendeleo hayana vyama!

halafu keshokutwa jumapili utamwona kanisani mstari wa mbele tena na ekaristi takatifu anakomunika kabisa!!! hivi huyu baba huwa walau anaungama hayo mazambi yake ya kusema uongo mchana kweupe au ndo ekaristi anakulaga tu kaa andazi?!!! Rais mzima wa nchi unachapia mauongo kila siku?!!!

isitoshe angemwacha gambo ajaribu tu bahati yake peke yake kuliko kwenda kuwaambia watu eti wamchague sababu kamtuma yeye!! sasa mtu anatumwa na mkuu wa serikali kugombea ubunge ataweza kweli kuisimamia hiyo serikali kwa niaba ya wapiga kura wake au ndo atakuwa ndiyo mzee?!!!! kwanza huyo magu mwenyewe arachuga hatumsomi wala nini afu ndo aje kumwombea mtu kura!! nani ampe? za kwake keshapata kwanza mpaka aje kumwombea mtu?!! huyo gambo hata ccm wa r chuga hawampi kura.
 
..wewe una barua inayothibitisha kwamba hakufukuzwa?

..Raisi si alijitokeza kwenye TV na kutoa lawama kwa Mrisho Gambo, mpaka akamtuhumu kwa mambo ya udini?
Kujitokeza kwenye tv ni kwa mujibu wa sheria?
 
1. Elimu iongezeke, hususan elimu ya uraia kwa watu wengi zaidi. Mtaji wa CCM ni ujinga wa Watanzania wengi.

2.Watu waache utamaduni wa "hewala, hewala". Hata ukiwa na elimu, ukiwa mwoga hutaweza kuuondoa mfumo dhalimu.

3.Wanaotaka mabadiliko wamaanishe hilo kwa kweli. Wao wenyewe waanze kuishi kwa utamaduni wa kidemokrasia na kupenda mawazo mbadala. Siyo mtu analalamikia udhalimu wa CCM isivyo na demokrasia, wakati nyumbani yeye baba akishasema jambo halina mjadala. Au chama cha upinzani anakiendesha kama familia yake binafsi.

4. Vyama vya upinzani viache kuwa vyama vya msimu wa uchaguzi.Nimeshangaa sana upinzani umekubali kunyamazishwa na Magufuli miaka yote hii.Hususan katazo la kufanya mikutano ya hadhara ambalo liko kinyume na katiba. Kama wapinzani wameshindwa kupinga hili, nawaona bado sana hawajajizatiti kuiondoa CCM.

5. Tuandae watoto na vijana wanaokua sasa kukua katika utamaduni wa kuukata ujinga bila tahayari.Kwa sasa naona kama na wao tayari wanaondolewa kutoka kwenye "kizazi cha kuhoji" na kupelekwa kwenye "kizazi cha hewala hewala".

6. Vyama vya upinzani vijizatiti zaidi kimataifa kuchukua uzoefu sehemu nyingine na kutengeneza urafiki na network kubwa za kimataifa zitakazosaidia kuleta maendeleo chanya bila kuleta hofu ya siasa zetu kutawaliwa na watu wa nje. Kuna mitandao inayojulikana na kuheshimika kama vile Amnesty International, The Committee To Protect Journalists, Human Rights Watch etc inafanya kazi kubwa na nzuri kumulika serikali dhalimu, lakini sioni kama wapinzani wetu wanazitumia hizi taasisi vizuri.

7. Vyama vya upinzani bado sana havijatumia mitandao ya kijamii kujitangaza. Presence ya chama kama CHADEMA Youtube, Twitter, au hata JF ni ndogo sana kulinganisha na ukubwa wa chama. Mitandao inasaidia sana kupasha habari watu wengi kwa wakati mfupi sana. Upinzani bado unacheza kwenye hili.

8.Vyama vya upinzani vinatakiwa kuonesha mifano ya shughuli za kiuchumi. Sio kupiga siasa za midomo tu.Yako wapi mashamba ya vyama vya upinzani? Yako wapi maduka yao? Iko wapi miradi ya kusaidia ajira kwa vijana? Wapinzani wakianzisha vitu hivi, humo humo kwenye miradi kuna nafasi ya kuongeza wanachama na kutanua wigo wa kueneza sera kwa wananchi, tena kwa kuonesha mifano, si maneno tu.Waswahili wanasema "Maneno matupu hayavunji mfupa". Waingereza wanasema "Action speaks louder than words".

9. Wapinzani wanatakiwa kuwashawishi watumishi wa umma, hususan vyombo vya dola, kwamba wao hawana ugomvi nao, wanataka kuitoa serikali ya CCM tu. Vyombo vya dola vinatakiwa kufanya kazi pamoja na wapinzani, si kudhibiti wapinzani. Vikidhibiti wapinzani ushahidi uchukuliwe na washitakiwe.

10.Vuyama vya upinzani vijizatiti zaidi kupanga mkakati wa kisheria kuhakikisha haviibiwi kura. Hii ni pamoja na mabadiliko ya katiba, kuongeza teknolojia, kuongeza waangalizi wanaoheshimika kutoka nje, na kuongeza kujitambua miongoni mwa wananchi.

Kuna mengi sana, ila kwa leo niishie hapa.
Exquisite..
 
Yes, it is clear kwamba hakumfukuza - Gambo aliomba ili ashiriki uchaguzi wa kura za maoni - wanaAtown tumchague Mrisho Gambo akamsaidie JPM kupaisha nchi yetu
 
Ukwaju ebu pitia pande hii please....
Mkuu mm hili Jukwaa siliwezi, kwani kule kwetu bado?
hiyo 28 ifike maana baada ya uchaguzi kuna maisha, hata 2025 tunaiombea tuwe hai
1603464425060.png

1603464197806.png
 
Back
Top Bottom