Liliendeshwa zoezi la kufanya furmigation katika jiji la Dar na baadhi ya maeneo nchini, wataalam wa afya natumai walijua kinachofanyika ni kiini macho ila walikaa kimya.
Viongozi wa kisiasa nao wakaaa kimya, viongozi wa uponzani kimya na hata viongozi wa kitaifa nao hawakutoa neno.
Sasa yamkini baadhi ya cases zimetokana na watu kuweka imani kwenye farmigation na kuacha kuchukua taadhari nyingine ya yamkini zipo familia zinaendelea zinaendelea kujilinda kwa Farmington. Nani alaumiwe?
Zipo hasara zilizotokana na zoezi hilo na natumai hizi Ni fedha za umma zilizotumika vibaya, waliotumia vibaya wanajulikana wala hawakuna haja kuwaundia tume. Baadhi walizungumza adharani, je Hawa watu wasiofanya utafiti kabla ya kulisha jamii sumu wanasubiri Nini ofisini?
Kauli imetoka na ilipotoka wamesikia, natamani kila mmoja ajitafakari je anawatendea Watanzania wanachostahiki?
Lakini kwanini jukumu tusilikabidhi kwenye mamlaka ya Afya na kuliondoa kwenye kamati za ulinzi na usalama za mikoa? Vyombo vibaki kusaidia wataalamu wa afya kutimiza malengo tu?