Wengi hamuwezi kumuelewa hii ni kutokana na kuzoea kumeza madesa,uvivu wa kufikiri na kutofuatilia mambo.
Jiulizeni maswali yafuatayo:-
1. Daktari wa kwanza kugundua jamii ya kirusi hiki kinachosababisha covid 19 alimgundua virus huyo mwezi November 2019 wakati virus huyo ameshafanya yake.
Swali la kujiuliza,ni lini alianza kushambulia watu?
2. China hawakukubali ugunduzi huo na kumwona daktari huyo kama mzushi,na alifungwa.Je ni watu wangapi waliokuwa free kusafiri muda huo kwani China hata hawakuchukua hatua yoyote wakati huo hadi hapo January?
3. Je mmefuatilia ni wageni wangapi kutoka nchi zilizokuwa zimeathirika walioingia nchini kuanzia mwezi October 2019 hadi March 2020?
4. Je kuna takwimu zozote za wagonjwa waliougua ugonjwa wenye dalili zinazofanana na covid 19 kabla ugonjwa haujatangazwa?Je mnadhani hakuna watu waliokuwa na ugonjwa wenye dalili kama hizo?
5. Tunaambiwa ugonjwa hauna tiba,je hata ukipima watu ambao hawaumwi,na ukawagundua,inasaidia nini?
6. Je kujitangaza kuwa mna wagonjwa wengi,kuna hasara yoyote kiuchumi?Na je wakiugua na kutibiwa hospitali bila kutangazwa kuna mtu atapata hasara?
7. Je ugonjwa huu usipoisha kabisa,unadhani nini kitaendelea?Unadhani maisha yatasimama?
Mwisho naunga mkono maamuzi ya Rais ni ya mtu mwenye hekima sana.Ni vigumu sana kama una akili nyepesi ya kuwaza saa ya kula ugali tu,kuelewa nia ya Mkuu wetu wa nchi.Wengi wanafuata maelezo ya wataalamu wanaokopi tu mambo kutoka kwa watu weupe bila hata kufikiria kwa kina kwa kuangalia mazingira yetu
Sent using
Jamii Forums mobile app