Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Kwaiyo Taarifa ya ummy ya kesho itakua waliopona 123 wagonjwa 285 yani kutufanya sie kama wanae mzee huyu.Wakati hayo mamia yameanza kutangazwa juzi tu. We toka chatto bwana uje tupambane usituchoshe hapa.Ummy angekua bold enougu angejiuzulu lin ndio hvo tena atakula wapi mana pale ni kama amewatusi kina ummy
 
(Ikulu Chato). Only in Tanzania.
Ikulu ni nini? Nielewavyo ni mahali Rais wa nchi anakaa, iwe kwa muda, au pa kudumu. Kwa hiyo, kila nyumba ya mkuu wa mkoa wa Tanzania ilikuwa pia ni ikulu kwa kuwa ndiyo nyumba ambayo mkuu wa nchi anaweza kulala akiwa huko. Nakumbuka pia Msoga ilikuwa ikulu at some point.
 
Jiwe umejua kunifurahisha leo, kuna wapumbavu wanatamani fungafunga oh funga masoko funga maduka funga baa mara zuia kile ohh zuia watu wasisafiri, nawaambia hawajui wanachokitamani wangejua adha na tabu za lockdown na fungafunga ni zaidi, afadhali mara elfu kumi ya corona wasingekaa wakathubutu kupayuka habari za lockdown na funga hiki fungia kile.
Mkuu wanaoshadadia lockdown wala siyo wananchi wa kawaida, ni wanasiasa na wanaharakati uchwara wanaotaka nchi ivurugike kwa maslahi yao. Na ndio wanaosambaza taharuki kwenye mitandao ya kijamii.

Uzuri ni kwamba Magufuli aliwashtukia mapema.
 
..Chato ni kijijini kwa Magufuli.

..JK hakuwa kuzungumza toka Msoga.

..Mkapa hakuzungumza toka Lupaso.

..Mwinyi hakuzungumza toka Zanzibar au Mkuranga.

..Mwalimu Nyerere hakuwahi kuzungumza toka Butiama.

..Raisi anapaswa kuendesha shughuli zake toka IKULU, na siyo toka ktk nyumba yake binafsi. Serikali siyo KAMPUNI binafsi ya Raisi.
upinzani ni kazi sana..
 
Wengi hamuwezi kumuelewa hii ni kutokana na kuzoea kumeza madesa,uvivu wa kufikiri na kutofuatilia mambo.
Jiulizeni maswali yafuatayo:-

1. Daktari wa kwanza kugundua jamii ya kirusi hiki kinachosababisha covid 19 alimgundua virus huyo mwezi November 2019 wakati virus huyo ameshafanya yake.
Swali la kujiuliza,ni lini alianza kushambulia watu?

2. China hawakukubali ugunduzi huo na kumwona daktari huyo kama mzushi,na alifungwa.Je ni watu wangapi waliokuwa free kusafiri muda huo kwani China hata hawakuchukua hatua yoyote wakati huo hadi hapo January?

3. Je mmefuatilia ni wageni wangapi kutoka nchi zilizokuwa zimeathirika walioingia nchini kuanzia mwezi October 2019 hadi March 2020?

4. Je kuna takwimu zozote za wagonjwa waliougua ugonjwa wenye dalili zinazofanana na covid 19 kabla ugonjwa haujatangazwa?Je mnadhani hakuna watu waliokuwa na ugonjwa wenye dalili kama hizo?

5. Tunaambiwa ugonjwa hauna tiba,je hata ukipima watu ambao hawaumwi,na ukawagundua,inasaidia nini?

6. Je kujitangaza kuwa mna wagonjwa wengi,kuna hasara yoyote kiuchumi?Na je wakiugua na kutibiwa hospitali bila kutangazwa kuna mtu atapata hasara?

7. Je ugonjwa huu usipoisha kabisa,unadhani nini kitaendelea?Unadhani maisha yatasimama?

Mwisho naunga mkono maamuzi ya Rais ni ya mtu mwenye hekima sana.Ni vigumu sana kama una akili nyepesi ya kuwaza saa ya kula ugali tu,kuelewa nia ya Mkuu wetu wa nchi.Wengi wanafuata maelezo ya wataalamu wanaokopi tu mambo kutoka kwa watu weupe bila hata kufikiria kwa kina kwa kuangalia mazingira yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jilockdown wewe mwenyewe...
Wiki ya nne sasa,kazini sienda na duka la mke wangu nimefunga,mwisho wa kupokea wageni home kwangu ilikuwa Jana, dogo I know what am doing so sijasubitia mtu aniambie kwa kuwa najua,mwenzio akinyolewa wewe tia maji.wewe kadevelop imunity ya corona mkuu,chapa kazi
 
Bottomline ya Rais ni kuwa let nature take its course. Natural selection take its course, survival for the fittest! atakayebaki basi anatosha mimi kutawala! Lakini no lockdown, economic activities to continue as normal. Vinginevyo huwezi kusema maneno kama hayo!
Na kweli tutapukutika vilivyo in the world history! Kinachoonekana kuzisaidia Europe na USA ni kockdown. South Amrica walifanya kama Jiwe, maiti zinaokotwa barabarani!.. Equador Pascal Mayalla au unasemaje rafiki

Wafanyakazi wa afya akili kichwani mwenu,,,,... kuishi au kufia kazini
 
Ikulu ni nini? Nielewavyo ni mahali Rais wa nchi anakaa, iwe kwa muda, au pa kudumu. Kwa hiyo, kila nyumba ya mkuu wa mkoa wa Tanzania ilikuwa pia ni ikulu kwa kuwa ndiyo nyumba ambayo mkuu wa nchi anaweza kulala akiwa huko. Nakumbuka pia Msoga ilikuwa ikulu at some point.
Yaah ata akiwa kwenye gari anakua Ikulu..endelea kuwapa elimu
 
JK alinifundisha msemo sitousahau, ZA KWAKO CHANGANYA NA ZA MBAYUWAYU....tuzingatie hili.

Anayesema hayo yote, anakuja na spin stories za mask zina CORONA, na mjifukize 100°C, na kakimbia ofisi yake iliyo ktk EPICENTER ya infection..kamuachia naibu..
Naye ni Fa Fa Fa Fa, hajui tofauti ya P wala Z katika hili...

Everyday is Saturday.......................😎
 
Wiki ya nne sasa,kazini sienda na duka la mke wangu nimefunga,mwisho wa kupokea wageni home kwangu ilikuwa Jana, dogo I know what am doing so sijasubitia mtu aniambie kwa kuwa najua,mwenzio akinyolewa wewe tia maji.wewe kadevelop imunity ya corona mkuu,chapa kazi
Sasa povu la nini kama na wewe umejilockdown pia?
Hopeless
 
Ujinga bado ni tatizo kubwa Tanzania. Stupidity is still common in Tanzania.

Mtu anatoka kule ameshiba utumbo wa bata anaandika mambo ya hovyo hovyo na ajabu unakuta ni mzazi ana watoto wanamtegemea kujifunza kutoka kwake.

Hizi nchi zetu kuendelea bado sana kwa sababu ujinga bado ni tatizo kubwa kiliko hata magonjwa.
 
Ahsante sana Mh.Rais wa JMT..wanaosema lock down niwasaliti kabisa awataki tuendelee kupokea kodi. Kweli 2015 sikupoteza muda wa kupiga kura...TUSITISHANE
 
Duuuh kweli matarumbeta akili mmeweka mfukoni!Hamuangalii USA wanavyoteketea?Eri hakuna haja ya kupima,seriously?Sasa si mtangaze tu maisha yaendelee kama kawaida na haya mambo yaishe ya kuambiana kuhusu Corona na sijui tahadhari!Kichwa maji mkubwa!
 
Back
Top Bottom