Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Wewe ndio unatatizo,bahati mzuri tumepata rais isiyependa blah blah, nyeupe iitwe nyeupe kadhalika nyekundu

Sasa kama mlizoea siasa kila kitu kwa JPM mtaugua presha, hotuba ilikuwa mzuri na nimeipenda sana
Huyu mzee ni kiongozi mbovu, wa hovyo. Kwa alichoongea leo ni kwamba ana tatizo kubwa kuliko tunavyomdhania. Mungu tusaidie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
By G Malisa:
"Hakuna virusi wanaokufa kwa fumigation. Kilichofanyika Dar es Salaam kupuliza dawa yenye kemikali ni upuuzi. Wanaokufa kwenye fumigation ni mende na si virusi ikiwemo virusi vya Corona.

Suala la kupuliza dawa ni upumbavu mtupu. Hakuna kirusi cha Corona kinachoweza kufa kwa Chlorine. Naomba IGP na Vyombo ulinzi mkachunguze walikuwa na lengo gani na nani alitoa hizo dawa” Rais JPM, 22/04/2020, Chato, Geita.

Nini maoni yako??
 
Jifukizeni mitishamba!
Mwenye picha ya kikombe babu atupie hapa tafazali
 
Kuna athari kubwa sana kwa mtu akijijengea fikira ya kupinga kila kitu,hebu fikiria kidogo makao makuu ya umoja wa mataifa yako Marekani,unataka kuniambia katibu mkuu wa umoja wa mataifa akitaka kutoa hotuba hadi aende Marekani,hawezi kuwa Tanzania na bado akahutubia mataifa yote?

Chato ni Tanzania,tupunguzeni manunguniko yasiyo tija

Sent using Jamii Forums mobile app
Chato anafanya nini? Tulimchagua akae ikulu, huko anafanya nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ndio unatatizo,bahati mzuri tumepata rais isiyependa blah blah,nyeupe iitwe nyeupe kadhalika nyekundu

Sasa kama mlizoea siasa kila kitu kwa jpm mtaugua presha ,hotuba ilikuwa mzuri na nimeipenda sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe kama unaona aliyoongea ni sahihi basi akili yako ina matatizo makubwa sana!
 
SALAAM ZA PONGEZI KWA MH RAIS MAGUFULI.

Na Elius Ndabila
0768239284


Leo Mh Rais amelihutubia Taifa alipokuwa akizungumza na wakuu wa vyombo vya usalama nchi. Hotuba ya Mh Rais imegusa mambo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa, kubwa likiwa ugonjwa wa Corona ambao unaiandama dunia kwa sasa. Nilipata wasaa wa kusikiliza vizuri sana hotuba ya Mh Rais.


Ninaomba nitumie wasaa huu kumpongeza Mh Rais kwa kuzungumza na Watanzania na kutoa ushauri wake kama amiri jeshi mkuu. Hotuba ya Mh Rais ni ya kutia matumaini na kuwapa ali kubwa Watanzania. Ninaimani kubwa Kama ushauri wa Mh Rais utazingatiwa ugonjwa wa corona hautakuwa tishio Bali utakuwa sawa na magonjwa mengine.


Nimpongeze Mh Rais kwa kuzumzia pia suala la kinga na tiba. Mh Rais amesema kwa kuwa bado hakuna dawa za kutibu corona ni vema WATANZANIA tukajiongeza kwa kutumia dawa za asili ikiwepo kujivukiza. Waafrika tumekuwa na tabia za kupuuza dawa za asili na kuamini dawa za magharibi. Wakati mwingine hata dini zetu zimekataza kutumia dawa za asili na kutushauri kutumia dawa za hospital. Tumedanganywa kwa kuwa watu hawajui hata hizo dawa za hospital ni dawa za kienyeji zilizoboreshwa zaidi. Ni vema tuwape furusa Wataalamu wetu wa asili kuonyesha juhudi zao ktk hili ambalo limewashinda wazungu. Hotuba ya Mh Rais inawapa nguvu madakitari wa asili kuonyesha vipaji vyao. Ugonjwa huu ni vita ya KIUCHUMI, hata dawa wakipata wazungu si rahisi kutufikia huku kwa kuwa maombi Yao ni afrika kufa ili wapate fursa ya kuja kuchukua Uchumi wetu.


Mh Rais ninampongeza pia kwa kutolea ufafanuzi suala la mask. Hivi tunategemea kama virus vya corona ni watu walitengeneza wanaweza kututengenezea maski za kuzuia? Ninaamini ile tathimini tuliyoambiwa Afrika kufikia mwezi wa nne itakuwa na wagonjwa wengi hupenda walikuwa wamepiga ni idadi ya mask zilizoingia Africa ambazo zinaweza kuwa na virus. Walitegemea kadiri tutakavyotumia maski ndivyo tutakavyoambukizwa. Mh Rais amesema kuna tetesi kuwa baadhi ya nchi hizi barakoa zimeonyesha kuwa na virus. Mh Rais amewapongeza wale wote wanaotumia mask za vitambaa vilivyotengenezwa hapa nchini. Hongera sana Mh Rais kwa kushauri viwanda vya hapa nchini vijiongeze na kuanza kutengeneza barakoa n.k


Mh Rais amesema uoga ni hatari kuliko ugonjwa wenyewe. Ameshauri tuchukue tahadhari zinazotolewa na Wataalamu lakini tusitishike. Rais ameonya pia wanaosambaza habari za uzushi kuwa watafutwe na washughulikiwe. Kwa hili ninampongeza mh Rais kwani kila mtu alikuwa anaandika anachokitaka.


Mwisho Rais amekemea vikali kufanya upuliziaji wa dawa kwenye miji na magari . Amesema hii haisaidii. Ameenda mbali kwa kusema hawezi kutangaza kuiweka lockdown DSM. Binafsi ninampongeza Mh Rais kwa kuwa amesaidia kuweka sawa suala la ubaguzi lililokuwa limeanza kujitokeza kwani ni wiki iliyopita tu moja ya wateule wake alionekana mbele ya camera akisema watu wa Dar Es salama muwakimbie na msiwakaribishe.


Mwisho ninampongeza mh Rais kwa kuonyesha msimamo wa kijasiri. Tutoke nje tukafanye kazi. Kukaa ndani ni hatari kuliko corona. Hivi Corona isipoisha wale wenzetu wa Kenya wataendelea kukaa ndani? Tupambane na corona tukiwa kazi ni na si kujifungia ndani. Ninaamini kwa kauli ya Mh Rais sasa vyuo na shule si MUDA mrefu masomo yataendelea.

#corona inaua chukua tahadhari
Kijijini Lali Ibaba.
Hongera sana mheshimiwa Rais kwa kutengeneza viumbe kama huyu mtoa mada ambao ni adimu sana kuwapata katika ulimwengu wa sasa. Ni aina fulani ya binadamu ambayo ilishatoweka siku nyingi na kuipata kwa urahisi labda umtumie DR Leakey

Sent using Jamii Forums mobile app
 
By G Malisa:
"Hakuna virusi wanaokufa kwa fumigation. Kilichofanyika Dar es Salaam kupuliza dawa yenye kemikali ni upuuzi. Wanaokufa kwenye fumigation ni mende na si virusi ikiwemo virusi vya Corona. Suala la kupuliza dawa ni upumbavu mtupu. Hakuna kirusi cha Corona kinachoweza kufa kwa Chlorine. Naomba IGP na Vyombo ulinzi mkachunguze walikuwa na lengo gani na nani alitoa hizo dawa” Rais JPM, 22/04/2020, Chato, Geita.

Nini maoni yako??
Duh uchunguzi tena ??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunaitaji tukope ili tuji jengee uwezo, kinachotakiwa fedha zinazo kopwa ziwe na riba yenye mantiki na fedha izo zitumike vizuri katika miradi husika.

Kwasasa tuna miradi mikubwa ya ma trilioni ya shilingi endapo itakamilika na ikaendelezwa vizuri taratibu kama nchi tuta anza ku ukimbia utegemezi na kuombaommba.

Mim nampongeza JPM kama kweli kila mwezi tunaweza kulipa bilioni miasaba za madeni tena mengine ameyarithi, uyu jamaa ni mwamba kwelikweli.Sasa naanza kumwelewa anaposema Nchi hii inaweza kuwa Donor country.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Raisi wa Tanzania JPM amesema Tanzania inalipa bilioni 700 katika taasis mbalimbali duniani zilizoikopesha nchi yetu kila mwezi ikiwemo benki ya dunia inayolipwa bilioni 200 kila mwezi. Hii ina maana kwa mwaka hulipwa zaidi ya trillion 8.4 fedha ambazo ni zaidi ya mishahara yote wanayolipwa watumishi wa umma.

Kwa hili nani anabisha kuwa Tanzania siyo koloni la mabeberu? Tuna safari ndefu ndugu Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ama kweli kukopa sherehe, kulipa matanga.
Kwani tulishikiwa fimbo kukopa?

Mimi naona tunalalama sana. Huwezi ukampangia mtu anaekudai kiwa akusamehe. Wewe ulivyokua unakopa ulikua umewehuka au?

Dawa ya deni ni kulipa tu.
 
Bado unategemea summary zinazofanywa na some members wa JF? Hotuba ipo hapo, huu uvivu mtaacha lini?
Unachekesha...yaani nitumie madakika kadhaa kumsikiliza Magufuli?! That will never happen!!

Btw, Magufuli aliyeita barakoa ni mavitambaa ya puani, atashindwa nini kusema barakoa zina coronavirus au ukijifukisha unaweza kuua coronavirus?! Ikiwa amesema
 
By G Malisa:
"Hakuna virusi wanaokufa kwa fumigation. Kilichofanyika Dar es Salaam kupuliza dawa yenye kemikali ni upuuzi. Wanaokufa kwenye fumigation ni mende na si virusi ikiwemo virusi vya Corona. Suala la kupuliza dawa ni upumbavu mtupu. Hakuna kirusi cha Corona kinachoweza kufa kwa Chlorine. Naomba IGP na Vyombo ulinzi mkachunguze walikuwa na lengo gani na nani alitoa hizo dawa” Rais JPM, 22/04/2020, Chato, Geita.

Nini maoni yako??
Rais Magufuli yuko sahihi kwa 100%
 
Sijakuambia kuwa iko USA yote hata hiyo NY mbona imeendelea kwa muda mrefu sana unataka kuniambia walikuwa wameambukizwa wote?. Kwa taarifa yako tangu juzi wamarekani hawataki tena lockdown wanaandamana mitaani. Bado hatujapata mwarobani wa kumaliza tatizo hili sana sana ni hali ya hewa na immune ya MTU husika. Utaona next month maambukizi US yatapungua kwa sababu ya mabadiriko ya hali ya hewa toka baridi kwenye kwenye joto. Hapa TZ tunatoka joto kwenda baridi hivyo maambukizi yanaweza ongezeka ingawaje sisi immune yetu iko juu kidogo ukilinganisha na watu weupe hivyo inaweza saidia sana.
Mkuu Marekani ni kubwa, Ina majimbo 52 na kila Jimbo linautawala wake, sema ni wamarekani wa Jimbo gani wameandamana?
 
..Chato ni kijijini kwa Magufuli.

..JK hakuwa kuzungumza toka Msoga.

..Mkapa hakuzungumza toka Lupaso.

..Mwinyi hakuzungumza toka Zanzibar au Mkuranga.

..Mwalimu Nyerere hakuwahi kuzungumza toka Butiama.

..Raisi anapaswa kuendesha shughuli zake toka IKULU, na siyo toka ktk nyumba yake binafsi. Serikali siyo KAMPUNI binafsi ya Raisi.
Usikalili kijana,rais ni higher authority anaweza endesha shughuri zake akiwa popote pale,rais ndio Ikulu ,Ikulu sio jengo.
 
Back
Top Bottom