Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

Rais Magufuli: Hakuna Lockdown kwa Dar wala Tanzania, NEVER! Tusiwatishe watanzania, hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko Corona

"Hofu ni ugonjwa mkubwa kuliko corona"..., au hofu juu ya tishio jingine lolote.

Manufaa ya 'Lockdown' popote Tanzania katika hatua hii iliyofikiwa na ugonjwa haipo tena. Kwa hiyo kinachowezekana, na kinachppaswa kuwekewa nguvu zaidi ni hizo njia za kinga, kuvaa barakoa, kuepuka mikusanyiko ya watu, kunawa, kutumia sanitizer, n.k., haya ndiyo yanayohitaji kuwekewa nguvu zaidi ili kuzuia kuendelea kusambaa kwa ugonjwa ndani ya jamii kwa kasi kubwa.

Haya yakifanyika kwa ufanisi na bila ya vitisho, Tanzania tutapata ahueni hata kama hatutaweza kuukomesha ugonjwa moja kwa moja.

Baada ya kuunga mkono aliyosema rais juu ya ugonjwa huo, napenda pia kuwakumbusha waTanzania juu ya mapana ya "Hofu kuwa ugonjwa mbaya" juu ya jambo lolote lile.

Inatubidi waTanzania tuachane na hofu wakati tunapofanya maamuzi mhimu yanayotuhusi sisi na maslahi ya nchi yetu nzima.

Tunapopata fursa ya kuwachagua viongozi wetu watakaotuongoza, tusisukumwe na hofu na kulazimika kupoteza haki yetu ya msingi ya kuwachagua viongozi bila ya shinikizo lolote na wala vitisho vyovyote.

Na akitokea kiongozi anayetaka kupora haki yetu hiyo kwa kutumia mabavu ya vyombo tulivyomkabidhi ili nchi yetu iwe salama, lakini yeye anavigeuza viwe ndio kinga yake na kuvitumia kutunyanyasa, inabidi pia tuachane na hofu na kukabiliana naye na kumkataa.

Tukifikia hatua hiyo, kwa hakika tutakuwa tumeyasikia na kuyaheshimu maneno ya busara aliyotuambia kiongozi wetu juu ya ugonjwa wa coronavirus.

Nitoe wito kwa waTanzania wenzangu. Uchaguzi mkuu utakapokuja, ni lazima tuondoe hofu (ugonjwa mbaya).
Tujitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura kwa mtu yeyote tunayeona kuwa anafaa kutuongoza bila ya hofu, na hata bila ya kuogopa vitisho kama vitakuwepo.

Tukishafanya hivyo, ni wajibu wetu pia kuhakikisha kuwa hatutasita na kuwa nahofu namtu yeyote atakayetaka kufanya hila na kuzifanya kura zetu zisihesabike na kutulazimisha tukubali viongozi ambao hatukuwapa kura hizo.

Hii ndio kuondoa hofu inayoweza kutufanya kuwa wagonjwa.

MTanzania, hustahili kuwa na hofu. Rais wetu amekwishaeleza hiyo ni hatari zaidi kuliko gonjwa baya hata kuzidi coronavirus.
Kweli mkuu watu wasiwe na hofu si unaona Uganda eti nao waliweka lockdown sasa angalia madhara makubwa waliyo pata
Cases 58 ,Deaths 0 na recovered 38 ...Wamepigwa ...alisema Think Tanker Gwajima
 
Kaka hivi unajua idadi ya watanzania wote wenye dalili za Malaria, TB, kichocho, fungus, cancer ya titi, shingo ya Uzazi, tezi dume, HIV. Je, unajuwa idadi ya vitanda vya kujifungulia vinavyohitajika na vilivyopo Sasa na wakunga wanaohitajika nchini?

Why CORONA? And not malaria?
Nitajaribu kukuelewesha kwa mara ya mwisho.

Kila ugonjwa una visababishi tofauti, dalili tofauti, na kwa yanayo ambukizwa - njia za maambukizi tofauti - na hata kwenye kutibu au kukinga kuna utofauti.

Why Corona and not malaria? Because malaria has yet to cripple an entire health system..because malaria can be prevented easily compared to the Corona virus..because malaria can actually be prevented and treated and until now, COVID-19 has neither vaccine nor cure...because malaria does not require respirators or ventilators- which we are short of - when cases get worse...because the Corona virus exasperates the immunity system which makes room for some of the diseases you listed even more lethal...the list is long!

Hakuna aliyesema kuwa tuache kushughulika na magonjwa mengine, ila kufumbia macho au kupuuza COVID-19 doesn't make it any less serious; quite the opposite!
 
Mhe. rais km mpambanaji namba 1 kwenye taifa letu la tanzania lenye kila aina ya maliasili tulizobarikiwa na mungu. tunahitaji kusikia kitu kutoka kwako tunahitaji kufahamu hapa tulipo tuna fanyaje na huko mbele tunaenande.

Katika kipindi hiki kigumu mno kwa dunia na sisi tukiwemo janga hili limesha tunyoosha,

Secta nyingi kwa sasa zipo hoi na nyingine zinachechema, tunahitaji kujua na utupe muelekeo na muongozo juu ya...

1. Nchi yetu imeathirika vipi kiuchumi na kiafya uchumi umedororo kwa asilimia ngapi ipi mikakati ya serikali kwa sasa tunafanyaje?

2. Vipi hali yetu ya secta ya afya tunaweza kumudu kuhudumia washukiwa na wagonjwa wa corona kwa kiwango kipi serikali imejipanga vipi. vipi hali ya magonjwa mengine km malaria , hiv na n.k vipi bajeti ya afya itabaki ileile au itaongezwa kwa kiwango gani na itatoka wapi hizo pesa za kuongezea..?

Je vikinga maambukizi barakoa, sanitizer na n.k vinapatikana mitaani kwa wingi na gharama nafuu maana tumeamua kuto kulockdown nchi je serikali inamikakati gani kuhakikisha raia wake wapo salama ktk shughuli zao za kila siku?

3. Mhe. rais corana imesimamisha uchumi wa mamilioni ya watanzania mfano, kwa mujibu wa wizara ya maliasili na utalii secto hii pekee ilitoa ajira za direct laki 6 na zile za indirect zaidi ya milioni 2 sasa kwa sasa secta hii ipo kwenye coma watu wote hao hawapo kwenye ajira tena,

Hiyo ni secta moja bado elimu zaidi ya walimu 89,000 elfu walikuwa wanafundisha private schools sasa wapo likizo zisizo na malipo achilia mbali hilo hapo hatujagusia michezo mbalimbali imesimama ziii, vikundi vya catering services kuanzia wapambaji, wapishi, mc na n.k zipo athari kubwa sana.

Hakika hali si nzuri ila ni serikali pekee inaweza kutufariji maelfu hawa kwa kusema mikakati mliyonayo na msaada wenu juu ya watanzania hawa.

4. Kwa vyovyote vile bajeti yetu 2019- 2020 na ya 2020-2021 zimeshaathirika kwa janga hili serikali ituambie tunafanyaje sasa..? km tutakopa wapi au itakuwaje..

5. Ukweli utatuweka huru km serikali yako mhe. mara nyingi umekuwa ukisema wewe ni mkweli na unapenda watu wakweli naomba taarifa ambazo tumekuwa tukipewa ziwe za kweli.

Mkanganyiko mwingi unajitokeza na kutuacha njia panda. mfano taarifa za watu waliopna mara 100 mara 11 tumuamini nani? sisi km watanzania hatutaki kuhoji uhaminifu wa serikali yk kwa raia ila tunaamini wahusika watajirekebisha ukweli muhimu hata km unaumiza ila ndio ukweli.

Mwisho tanzania ni moja na sisi pia tuwe wamoja na wenye nia ya dhati ktk kupambana na corona ktk kipindi hiki kigumu.

#Chukua taadhari kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya corona.
 
SueIsmael,
Hapo namba 4 utafiti umeufanya lini kujuwa kuwa hakuna tofauti ya fatality rate kati ya mtu mweupe na mtu mweusi? Kati ya tropical and template Climate/Weather kwenye CORONA?

Kuambukizwa sio issue kwetu issue yetu ni mortality ratio sio morbidity
 
Mkuu na hiyo ndo sababu kuu ya kuitwa pandemic.Sasa huyo matanga mkuu kakariri tu chapa kazi,unachapaje kazi wakati upo hospital au unaugulia ndani?
Matokeo ya kuambukizwa ni kuugua au kutokuugua hata baada ya kuambukizwa. Na matokeo ya kuugua ni kupona kabisa, kufa au kupona na kubaki na disability. Hivyo hakuna mgonjwa ambaye atabaki ndani au hospital milele.

Lazima atapona au kufa ndani ya muda mfupi usiozidi siku 10. Ukipona utarudi kazini na ukifa utakwenda kuzikwa na watu wasiozidi 10.

Lakini kujifungia (lockdown) inaweza kuendelea zaidi ya siku 100 hufanyi kazi ya aina yoyote hadi hapo usikie kuwa hakuna mgonjwa hata mmoja mwenye COVID-19 huko nje. Huo ni uchizi sawa na uchizi mwingine.

Ni heri uugue uugue upone au ufe maisha yaendelee kuliko kujifungia endlessly. Survival of the fittest
 
Return Of Undertaker, Hujaelewa...

Raisi kaongelea FUMIGATION MASHINES (huvaliwa mgongoni) na hutoa aidha maji (liquid) au vapour.

na zile za ROSTAM ni SANITIZING MASHINES hutoa vapour tuu.

#YNWA

Wrote from Anfield...!!!
 
Yaani kiongozi mkuu wa Nchi Kuja kwa raia kutoa ushuhuda was Jambo ambalo liko chini ya uwezo wake nikuonesha kiasi gani hana mawasiliano mazuri na wataalam wake. Chukulia mfano hizo kemikali zingekuwa na madharaa kwa binadam nani alipswa kuwajibika??, Ilihali haya yanafanyika chini ya kijana wake mpendwa. Tuache kusifu mambo yakipuuzi
Hujaelewa...

Raisi kaongelea FUMIGATION MASHINES (huvaliwa mgongoni) na hutoa aidha maji (liquid) au vapour.

na zile za ROSTAM ni SANITIZING MASHINES hutoa vapour tuu.

#YNWA

Wrote from Anfield...!!!
 
Nafanya kazi mochwari

Jr[emoji769]
Hao walioko mortuary labda wametoka kwenye familia yenu, maana mtaani kwetu wote tupo na ndugu zangu wote wapo na wafanyakazi wenzangu wote wapo Sasa hayo mafuriko huko mortuary wametoka mtaa gani?
 
Waliofanya fumigation siyo wajinga. Utafiti uliofanywa na Marekani, unaonesha mabwawa ya kuogelea yaliyowekwa chlorine, virus au wanakufa au wanakuwa inactive.

Na wanaoogelea kwenye mabwawa wamehakimishiwa kuwa kama maji ya kwenye bwawa yamewekwa chlorine, hata kama mmojawapo wa wanaoogelea akawa ana virus vya corona, hawezi kuwaambukiza wengine kwa kupitia maji.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujaelewa...

Raisi kaongelea FUMIGATION MASHINES (huvaliwa mgongoni) na hutoa aidha maji (liquid) au vapour.

na zile za ROSTAM ni SANITIZING MASHINES hutoa vapour tuu.

#YNWA


Wrote from Anfield...!!!
 
Vipi Spain, Italy, France, USA wanafanya fumigation?
Hujaelewa...

Raisi kaongelea FUMIGATION MASHINES (huvaliwa mgongoni) na hutoa aidha maji (liquid) au vapour.

na zile za ROSTAM ni SANITIZING MASHINES hutoa vapour tuu.

#YNWA

Wrote from Anfield...!!!
 
Sijaona Marekani wakifanya fumigation mitaani
Hujaelewa...

Raisi kaongelea FUMIGATION MASHINES (huvaliwa mgongoni) na hutoa aidha maji (liquid) au vapour.

na zile za ROSTAM ni SANITIZING MASHINES hutoa vapour tuu.

#YNWA

Wrote from Anfield...!!!
 
Sawa bhana! Rostam Aziz akamatwe sio?
Dah! Na tunasisitizwa tuchangie
Raisi kaongelea FUMIGATION MASHINES (huvaliwa mgongoni) na hutoa aidha maji (liquid) au vapour.

na zile za ROSTAM ni SANITIZING MASHINES hutoa vapour tuu.

#YNWA

Wrote from Anfield...!!!
 
  • Thanks
Reactions: Mj1
Back
Top Bottom