Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

Rais Magufuli: Hakuna lockdown Tanzania! Mwanangu amepona COVID-19 kwa kujifukiza (Mei 17, 2020)

“Kwa hali hii, kama wiki tunayoianza kesho itaendelea hivi nimepanga kufungua vyuo ili Wanafunzi wetu waendelee kusoma, lakini nimepanga pia kuruhusu michezo iendelee kwasababu michezo ni sehemu ya Burudani, maisha lazima yaendelee” -JPM #JPMChato millardayo on Twitter
 
Huyu mzee hajafahamishwa vizuri kuhusu huu ugonjwa,mbona analeta mzaha hivi
yeye mwache tu,mbona amejificha chato arudi dar tupige kazi na afanye ziara zake kama kawaida hapo ndio nitaamini maneno yake,kwaniini anatuambia sie tupige kazi tupukitike wakati yeye amejikarantini? Nadhani mzee ana target ya kuwaperish wagonjwa wenye magonjwa nyemelezi wote,watu wenye presha,sukari,overweight(obese),ngoma ndio watakaoumia.
 
Safiii Bora tugungue Mana kujifungia sio suluhisho ,@mh.Dr.John P Magufuli juu, Mwenyezi Mungu akulinde siku zote, more blessings 2 you
 
Na kuna watu laki kadhaa waliougua wakakaa tu nyumbani wakajifungia wakapona. Hahah zee jinga hili, mtu moja kupona haimaanishi ni dawa, ingekua hivyo watu milioni waliopona duniani kwa kukaa tu miili yao ikapambana na virusi tungesema hiyo ni dawa kwa hiyo tusifanye lolote.
PhD hivi aligawiwa bure? Au alifanyiwa research na mtu mwingine? Mbona jinga sana?
Hakuna kitu alishawahi kuongea ukakubali
 
Mhe. Rais Magufuli anatarajiwa kutuma salaam kwa Taifa leo Mei 17, 2020.

Hotuba yake inaaminika itajaa mambo mazito.

Kaa standby kwenye media zote na mitandao ya kijamii muda si mrefu ujao.

Inatarajiwa kuanzia mida ya saa sita na nusu mchana (12:30PM) ndipo atakuwa mubashara.

JF will cover it

======

View attachment 1452519

‪RAIS AMETOA SALAAM BAADA YA KUSHIRIKI KATIKA IBADA YA KANISA LA KKKT USHARIKA WA CHATO‬

Raisi Magufuli akiwa katika kanisa la KKKT Chato amepata nafasi ya kuzungumza mbapo ameongea mambo mbalimbali,

Katika hotuba hiyo Raisi ameanza kwa kumshukuru Mungu na viongozi wa dini wote nchini. Raisi magufuli amesema “Waimbaji wameimba hapa kwamba bila mungu huwezi kuongoza, bila kumtanguliza mungu huwezi ukafanya chochote. Kwahiyo napenda niwashukuru Watanzania wote, Viongozi wa dini mbalimbali ambao wameshiriki kuliombea taifa hili"

"Na ndio maana siku za nyuma wakati ugonjwa huu umeingia niliwaomba ndugu zangu watanzania angalau tutumie siku tatu za kuomba kwelikweli. Ninawashukuru sana kwa sababu wote tuliomba tulifunga na Mungu amejibu na Mungu ametusikia”

“Ndugu zangu mifano mingi imetolewa, hata katika mahubili yako leo Baba Mchungaji katika injili na katika matendo ya mitume umeeleza ni namna gani watu walivyoweza kumtegemea Mungu walivyoweza kufanikiwa”

“Yule kipofu alimlilia yesu, Mwana wa Daudi nirehemu, Yesu ambaye ni mtoto wa Mungu ambaye naye pia ni Mungu alimponya. Wakati wa dhoruba kula baharini wanafunzi walivyokuwa wamelala wakaona mtumbwi unataka kuzama walipiga kelele” Katika maandiko pia sehemu zingine Yesu aliwakemea kwanza mitume kwa kuwa na Imani ndogo na baadaye akaikemea pepo na mambo yakawa shwari kwahiyo sisi katika kipindi chochote kigumu cha aina yoyote tukimtanguliza Mungu tutafanikiwa”

“Kwahiyo ninawashukuru sana ndugu zangu, ninawashukuru sana Wachungaji, Masheikh, Mapadri, Maaskofu kila mmoja katika eneo lake ambao tulimtanguliza Mungu na Mungu ametusaidia sana”.

“Ndugu zangu katika mapambano ya aina yoyote ni vita. Ugonjwa huu wa Corona hauna tofauti na vita nyingine. Nilikwisha eleza na wataalamu pia wameahaeleza ni namna gani nzuri ya kuweza kupambana na ugonjwa huu hata Baba Mchungaji umezieleza mbinu zote”.

“Ni kweli sikutoa amri ya lockdown ya kuwafungia watu majumbani, ulikuwa ni utumwa wa ajabu. Imagine wewe Lyabange ufungiwe saa nyingine hata usionane na Mme wako Iseme au na watoto wako. Sisi hapa huwa tunaondoka asubuhi kwenda kuchukua chakula, ukachume viazi, maharage yako, uende ziwani ukavue hivyo vyote vingekuwa vimezuiliwa”.
.
Nimemsikia huyu mjamaa akisema eti watalii wanafunguliwa milango soon '"wakishapimwa temperature wakaonekana liko chini waende wacacoronise" huyu jamaa akapimwe upstairs aisee hayuko vyema
 
Mungu azidi kumlinda Rais JPM..
Hakika ni chaguo la Mungu

Leo naamini nikiwa kama Mkristu niliye na Imani tele maishani mwangu.. naamini wengi watakuwa wameondoa hofu kwa kumsikiliza.. kweli angekuwa Mchungaji tu.. ana upako..

Kama alivyosema.. endeleeni kuchukua tahadhari na kusali.. msiruhusu hofu iwaingie..

Magufuli oyeeeeeeeee
Mimi mtu asitmye mwelewa Rais Magufuli huwa nahesabu kama ni takataka tu.

Viba JPM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kuna watu laki kadhaa waliougua wakakaa tu nyumbani wakajifungia wakapona. Hahah zee jinga hili, mtu moja kupona haimaanishi ni dawa, ingekua hivyo watu milioni waliopona duniani kwa kukaa tu miili yao ikapambana na virusi tungesema hiyo ni dawa kwa hiyo tusifanye lolote.
PhD hivi aligawiwa bure? Au alifanyiwa research na mtu mwingine? Mbona jinga sana?
Uwiii nasoma comment yako huku naogopa
 
Nichukue fursa hii kumpongeza waziri wa Utalii Dr Kigwangalla kwa kuhakikisha watalii waliofanya booking wanalinda ahadi zao.

Nipo hapa Arusha kama mtalii wa ndani na nimefurahi sana kusikia kuwa watalii wa nje wataanza kumiminika tena soon.

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom