barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,378
- 29,739
Ni kweli. Sindano hii sasa hivi bavicha wamelala chali ganzi mwili mzima. Bora asingeongea wapate ahueni.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni kweli. Sindano hii sasa hivi bavicha wamelala chali ganzi mwili mzima. Bora asingeongea wapate ahueni.
wamesahau kama kuna mdudu yuko nje anasambaa kwa kasi hahahaaKaenda kugawa pesa kanisa meno nje vigelegele Kama vyote
Wewe endelea kujifungia ndaniLeo ameongea huku ametulia. Ila suala la kusema tuchape kazi ndo nawaza tuu hapa au za kuambiwa nichanganye na zangu?
yeye mwache tu,mbona amejificha chato arudi dar tupige kazi na afanye ziara zake kama kawaida hapo ndio nitaamini maneno yake,kwaniini anatuambia sie tupige kazi tupukitike wakati yeye amejikarantini? Nadhani mzee ana target ya kuwaperish wagonjwa wenye magonjwa nyemelezi wote,watu wenye presha,sukari,overweight(obese),ngoma ndio watakaoumia.Huyu mzee hajafahamishwa vizuri kuhusu huu ugonjwa,mbona analeta mzaha hivi
Hakuna kitu alishawahi kuongea ukakubaliNa kuna watu laki kadhaa waliougua wakakaa tu nyumbani wakajifungia wakapona. Hahah zee jinga hili, mtu moja kupona haimaanishi ni dawa, ingekua hivyo watu milioni waliopona duniani kwa kukaa tu miili yao ikapambana na virusi tungesema hiyo ni dawa kwa hiyo tusifanye lolote.
PhD hivi aligawiwa bure? Au alifanyiwa research na mtu mwingine? Mbona jinga sana?
Nimemsikia huyu mjamaa akisema eti watalii wanafunguliwa milango soon '"wakishapimwa temperature wakaonekana liko chini waende wacacoronise" huyu jamaa akapimwe upstairs aisee hayuko vyemaMhe. Rais Magufuli anatarajiwa kutuma salaam kwa Taifa leo Mei 17, 2020.
Hotuba yake inaaminika itajaa mambo mazito.
Kaa standby kwenye media zote na mitandao ya kijamii muda si mrefu ujao.
Inatarajiwa kuanzia mida ya saa sita na nusu mchana (12:30PM) ndipo atakuwa mubashara.
JF will cover it
======
View attachment 1452519
RAIS AMETOA SALAAM BAADA YA KUSHIRIKI KATIKA IBADA YA KANISA LA KKKT USHARIKA WA CHATO
Raisi Magufuli akiwa katika kanisa la KKKT Chato amepata nafasi ya kuzungumza mbapo ameongea mambo mbalimbali,
Katika hotuba hiyo Raisi ameanza kwa kumshukuru Mungu na viongozi wa dini wote nchini. Raisi magufuli amesema “Waimbaji wameimba hapa kwamba bila mungu huwezi kuongoza, bila kumtanguliza mungu huwezi ukafanya chochote. Kwahiyo napenda niwashukuru Watanzania wote, Viongozi wa dini mbalimbali ambao wameshiriki kuliombea taifa hili"
"Na ndio maana siku za nyuma wakati ugonjwa huu umeingia niliwaomba ndugu zangu watanzania angalau tutumie siku tatu za kuomba kwelikweli. Ninawashukuru sana kwa sababu wote tuliomba tulifunga na Mungu amejibu na Mungu ametusikia”
“Ndugu zangu mifano mingi imetolewa, hata katika mahubili yako leo Baba Mchungaji katika injili na katika matendo ya mitume umeeleza ni namna gani watu walivyoweza kumtegemea Mungu walivyoweza kufanikiwa”
“Yule kipofu alimlilia yesu, Mwana wa Daudi nirehemu, Yesu ambaye ni mtoto wa Mungu ambaye naye pia ni Mungu alimponya. Wakati wa dhoruba kula baharini wanafunzi walivyokuwa wamelala wakaona mtumbwi unataka kuzama walipiga kelele” Katika maandiko pia sehemu zingine Yesu aliwakemea kwanza mitume kwa kuwa na Imani ndogo na baadaye akaikemea pepo na mambo yakawa shwari kwahiyo sisi katika kipindi chochote kigumu cha aina yoyote tukimtanguliza Mungu tutafanikiwa”
“Kwahiyo ninawashukuru sana ndugu zangu, ninawashukuru sana Wachungaji, Masheikh, Mapadri, Maaskofu kila mmoja katika eneo lake ambao tulimtanguliza Mungu na Mungu ametusaidia sana”.
“Ndugu zangu katika mapambano ya aina yoyote ni vita. Ugonjwa huu wa Corona hauna tofauti na vita nyingine. Nilikwisha eleza na wataalamu pia wameahaeleza ni namna gani nzuri ya kuweza kupambana na ugonjwa huu hata Baba Mchungaji umezieleza mbinu zote”.
“Ni kweli sikutoa amri ya lockdown ya kuwafungia watu majumbani, ulikuwa ni utumwa wa ajabu. Imagine wewe Lyabange ufungiwe saa nyingine hata usionane na Mme wako Iseme au na watoto wako. Sisi hapa huwa tunaondoka asubuhi kwenda kuchukua chakula, ukachume viazi, maharage yako, uende ziwani ukavue hivyo vyote vingekuwa vimezuiliwa”.
.
Mimi mtu asitmye mwelewa Rais Magufuli huwa nahesabu kama ni takataka tu.Mungu azidi kumlinda Rais JPM..
Hakika ni chaguo la Mungu
Leo naamini nikiwa kama Mkristu niliye na Imani tele maishani mwangu.. naamini wengi watakuwa wameondoa hofu kwa kumsikiliza.. kweli angekuwa Mchungaji tu.. ana upako..
Kama alivyosema.. endeleeni kuchukua tahadhari na kusali.. msiruhusu hofu iwaingie..
Magufuli oyeeeeeeeee
Uwiii nasoma comment yako huku naogopaNa kuna watu laki kadhaa waliougua wakakaa tu nyumbani wakajifungia wakapona. Hahah zee jinga hili, mtu moja kupona haimaanishi ni dawa, ingekua hivyo watu milioni waliopona duniani kwa kukaa tu miili yao ikapambana na virusi tungesema hiyo ni dawa kwa hiyo tusifanye lolote.
PhD hivi aligawiwa bure? Au alifanyiwa research na mtu mwingine? Mbona jinga sana?
Mwamba huyu.“Kwa hali hii, kama wiki tunayoianza kesho itaendelea hivi nimepanga kufungua vyuo ili Wanafunzi wetu waendelee kusoma, lakini nimepanga pia kuruhusu michezo iendelee kwasababu michezo ni sehemu ya Burudani, maisha lazima yaendelee” -JPM #JPMChato millardayo on Twitter
Hapa duniani kuna yeyote anayeweza kumuambia lolote kinyume na kumsifia?Unataka kumwambia nini ?