Rais Magufuli: Hali kwa sasa ipo vizuri na Corona inapungua. Wanafunzi wa Form VI na Vyuo vyote kufunguliwa 01 Juni 2020

Rais Magufuli: Hali kwa sasa ipo vizuri na Corona inapungua. Wanafunzi wa Form VI na Vyuo vyote kufunguliwa 01 Juni 2020

Tupatie sababu za kisayansi kwanini huamini kwamba nyungu ni kinga mojawapo ya Corona...wenzako wameshatoa sababu za kisayansi kwamba virus huyo hawezi kustahi mili kwenye heat...kwa hiyo kujifukiza kunaleta heat kwa hiyo huyo virus anapukutika...
mkuu kuwa serious, jamaa amesema kuwa hao viongozi hawajavaa barakoa kwasababu wamepiga nyungu,
inamaana mtu akipiga nyungu ndiyo inakua kinga means nyungu ni chanjo ya korona??
 
mkuu kuwa serious, jamaa amesema kuwa hao viongozi hawajavaa barakoa kwasababu wamepiga nyungu,
inamaana mtu akipiga nyungu ndiyo inakua kinga means nyungu ni chanjo ya korona??
Haiwezi kuwa chanjo,Ni watu wanakinga zao tu
 
Karibu

Wageni wameshawasili katika sherehe hii ambayo wateule kadhaa wataapishwa akiwemo Naibu waziri wa afya, Katibu tawala mkoa wa Pwani Mkurugenzi wa Takukuru na mabalozi.

Rais Magufuli ameshaingia ukumbini tayari kuanza kuwaapisha wateule wake.



=====
Baadhi ya mambo yaliyozungumzwa

Prof. Kabudi - Canada yaipongeza Tanzania kwa hatua ilizochukua dhidi ya CoronaVirus na wameahidi kusaidia kusaidia kwenye swala la elimu

Waziri Wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Canada. Canada imetupongeza kwa namna ambavyo tumepambana na Covid19. Wameahidi watatisaidia katika maeneo ya elimu na afya kwa kadiri mahitaji yetu yatakavyokuwa.

Nilimsisitizia Waziri yule kuwa sisi watupe pesa na tutajua ni maeneo gani katika nchi hii tutazipeleka, katika kuimarisha uchumi na katika kupambana na maradhi haya.

Juzi pia niliongea na Balozi wa Umoja wa Ulaya. Umoja wa Ulaya umeamua kutoa Dola milioni 38 ambazo zitakuja Tanzania kutusaidia katika maeneo mbalimbali baada ya hili janga la Coronavirus.

Pia niliongea na Balozi wa Sweden kwa njia hii hii ya mtandao. Sweden wataongeza Dola milioni 20 katika bajeti ya elimu na Dola milioni 10 kwenda TASAF

Ummy Mwalimu - Tulijiandaa kuchukua uwanja wa sabasaba ili kuwaweka wagonjwa wa corona lakini sasa wagonjwa wamepungua kwa hiyo uwanja umerudishwa

Suleiman Jaffo - Nyungu season two inaanza Jumatatu... pia tuwaambie watalii kuwa, wanakaribishwa Tanzania wakifika wanapewa zawadi ya nyungu

Magufuli - Corona bado ipo, imepungua ni kweli lakini tuendelee kuchukua tahadhari

- Msikubali vifaa vya corona vinavyogawiwa na taasisi mbalimbali, kama ni kupokea kifaa cha kupambana na corona, kipitie Wizara ya Afya na kiwe checked.

- Katika michango hii unaweza kuletewa hata barakoa zenye corona kwa kuwa trend yetu iko vizuri, vya bure ni vibaya

- Mtu akileta kifaa kikichunguzwa kikakutwa na korona apewe kesi ya jinai hata ya kuua kabisa

- Vyuo vikuu vyote vitafunguliwa tarehe 1/6/2020

Vijana wa kidato cha sita watarudi shuleni 1/6/2020, pia iandaliwe crash program ili isiharibu utaratibu wa wao kuingia chuo kikuu,

Sekondari na shule za msingi zinapewa muda wa kujitazama ila chuo kikuu wanajitambua

Michezo
- Kuanzia tarehe 1/6/2020 michezo yote ianze rasmi kuanzia ligi daraja la kwanza, taratibu za kushangilia na kushabikia zitatolewa muongozo na Wizara ya Afya

Immunity inaongezeka mtu akiwa anainteract, ukimfungia immunity inaweza kushuka kwa 30%

--
Kuanzia tar 27/28 Mei 2020 itaanza kuruhusu ndege kuingia nchini, na watalii hawatafungiwa kwa siku 14, atamuikwa na kama joto lake litakuwa chini ya ile jotoridi linalotakiwa,

Miti ya kujifukiza itolewe kama Complementary kwa watalii

Magufuli: Mungu amejibu maombi yetu.

Watakaoguswa kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili tutumie siku hizo kumshukuru Mwenyezi Mungu


Hakika Mungu amejibu maombi yetu.
 
Hongera Magufuli kwa uamuzi huu kufungua vyuo, michezo na kuwaruhusu form six kuendelea kuendelea na masomo ili kujiandaa na mitihani. Huu Ni uamuzi wa kujiamini baada ya kuona maambukizi kupungua. Tuombe Mungu Mambo yaende vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanao mhusu wako safe, peleka wa kwako
 
mkuu kuwa serious, jamaa amesema kuwa hao viongozi hawajavaa barakoa kwasababu wamepiga nyungu,
inamaana mtu akipiga nyungu ndiyo inakua kinga means nyungu ni chanjo ya korona??
Mmh ni Nani alisema nyungu ni chanjo? Kwani magonjwa yote Yana njanjo? Hivi Chlorowuin ni njanjo? After a second thought uliwahi kusikia kitu kinaitwa Sauna bath?? Kwa maoni yangu wazungu nao wana aina Fulani ya nyungu...haya ni maoni yangu binafsi..
 
Mmh ni Nani alisema nyungu ni chanjo? Kwani magonjwa yote Yana njanjo? Hivi Chlorowuin ni njanjo? After a second thought uliwahi kusikia kitu kinaitwa Sauna bath??
narudia tena kukuuliza, Nyungu ni kinga ya korona???
maana mtu anavyosema kuwa hao kina kabudi hawajavaa barakoa kwasababu walipiga nyungu anakua anamaanisha kuwa nyungu ni kinga ya korona.

hivi ukimeza dawa ya malaria ndiyo hutumii chandarua tena???
dawa ya malaria ni kinga ya malaria??
 
Wewe endelea kumfuata askofu tena ikiwezekana nenda na familia yako mkajifungie kwake kabisa mkisubiri corona iishe duniani.

Yani mkisikia hakuna kisa cha corona hata kimoja dunia nzima ndio mnatoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nasubiri kushika beleshi siku ya kuchimba kaburi lako. Nyambafu wewe usiyeweza kutumia akili zako
 
narudia tena kukuuliza, Nyungu ni kinga ya korona???
maana mtu anavyosema kuwa hao kina kabudi hawajavaa barakoa kwasababu walipiga nyungu anakua anamaanisha kuwa nyungu ni kinga ya korona.

hivi ukimeza dawa ya malaria ndiyo hutumii chandarua tena???
dawa ya malaria ni kinga ya malaria??
Nyungu ni miongoni mwa tiba ya corona
 
unabii unaelekea timia

darasa halitimii bila wapiga kelele hivo msiwashangae hawa oya oya wamitandaoni
 
Basi kumbe wanachuo Wana raha Sana,Ina maana hata nikikacha kipindi mwalimu haji bwenini kusaka waluojongo vipindi?,mwalimu wa zamu hafanyi patrol bwenini?.
Nisivyopenda kusoma,ningeota kitambi asee😆😆
Haha kwani Wewe haukufanikiwa kufika chuo kikuu
 
Kuna baadhi ya wanafunzi walisha sign boom likaingizwa kwa a/c mtaani walikuwa wanaonesha kuwa wanasoma elimu yakulipwa kamahawakujua kunakurudi chuo
 
Mimi nasubiri kushika beleshi siku ya kuchimba kaburi lako. Nyambafu wewe usiyeweza kutumia akili zako
Angalia nisije kuchimba mimi lako kwanza!

Mimi nakushauri endelea kujifungi ndani na askofu wako hadi siku mtakapo sikia hakuna kabisa corona duniani ndio mnatoka sawa ee?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom