Rais Magufuli jitahidi uache uvunjaji wa sheria! Let justice take its natural course!

Rais Magufuli jitahidi uache uvunjaji wa sheria! Let justice take its natural course!

Rais kwa mamlaka yake ni muajiri mkuu wa Serikali hivyo ana mamlaka yote ya kumuajiri na kumfukuza yeyote ndani ya JMT kwa sababu yoyote bila kumtaarifu yoyote juu ya ukomo wako wa ajira.

Hata kama ni ngumu kuwatoa baadhi ya watumishi kama CAG na majaji lakini katiba imesema hapana kama Rais hatoweza kuwaondoa hao dhanà nzima ya muajiri mkuu inapotea ndio maana kawekewa utaratibu wa kumtoa na anaweza kumtoa.

Kwa hiyo Rais anaposema Fulani atoke hakihitajiki kingine zaidi ya kutangazwa nafasi ipo wazi na mtu anajazwa
Angeweza kufanya hivyo kimya kimya, bila 📷
 
Huyu bwana kaenda kinyume na maadili ya kazi hana sababu ya kukaa kwenye ofisi ya Umma kama analeta tabia za kuzungumzia udini kwenye ofisi za Umma
 
Muislamu kukaa Jela kwa sababu ya uonevu na udhalimu haikuanza leo, ni sunna ya manabii.

Kakaa Jela nabii Yusufu itakuwa masheikh?. kwa taarifa yako kila siku wanayokaa jela wanaandikiwa thawabu bali kila siku ipitayo wale watesi na waovu waliowaweka jela kwa dhulma wanaandikiwa dhambi, Je ni nani atakayefaulu kati ya wao na hawa madhalimu?

Huyu mlevi aliyechoma Quran, hata kama asingeichoma au kufukuzwa kazi isingewasaidia chochote wale masheikh
Na hapo ndipo mnapofeli kila siku mnakalia mnasubiria dhawabu na wale Mabikira 72 mlioahidiwa na bwana mood badala ya kuwatetea kwa kupiga kelele kuomba haki itendeke kama mahakamani wapelekwe kama kufungwa wafungwe kihalali.Hapo tu lazima kipindi cha uchaguzi mtoe tu!!!.
 
Kila mtu ana haki ya kupiga kura kuchagua anayemtaka. Sasa usilszimishe sababu zinazokufanya wewe umchague mtu fulani ziwe ndo zilezile ambazo mtu mwingine anapaswa kuzitumia kumchagua unayemtaka wewe.

Kura ya mtu ni haki yake hata akiamua kumchagua mgombea mwenye sura nzuri hilo muachie yeye.
 
Kwa hiyo Rules of procedure zinazotungwa to guide the constitution and the laws therefrom ni upuuzi! Umesoma wapi kijana. Mimi nina miaka 47 ya sheria.......siyo kijana kama ulivyosema.

Sent using Jamii Forums mobile app
katiba inasema raisi hatatakiwa kufuata sheria za bunge zinazotoa mwongozo wa kuwaondoa wafanyakazi soma sheria kijana acha siasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo ndo huwa namuelewaga magufuli,kasimama kwenye maadili,
,huyo msela yy huko mahakamani ashinde tu kesi kuchana kitabu cha imani ya mwenzio ni sahihi,tena ashinde tu ila kwenye maadili kala kibano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais kama muajiri mkuu wa Serikali na aliyechana Quran ni muajiriwa wa Serikali na serikali imeweka viwango vya nidhamu na maadili ambavyo vingine vipo nje ya sheria ila ndani ya mamlaka ya ajira, kumfukuza mtu aliyefanya hivi si kosa.

Mahakàmà itaangalia kosa kwa upànde wa kisheria na serikali imeangalia kosa kwa upànde wa maadili na si makosa yote ya kimaadili yanavunja sheria, mengine yanavunja taratibu za kazi na za kiutumishi.

Mfano mtu kaenda kazini kalewa, hilo ni kosa la kimaadili ambalo sheria haiwezi kumkuta na kosa.

Rais hajavunja sheria yeyote ila katekeleza wajibu kama muajiri mkuu na msimamzi wa maadili wa watumishi wote wa umma

Halafu Rais mimi nilimsikiliza usiku wakati wa marudio ya Hotuba yake. Rais hakusema kuwa amemfukuza kazi kwa sababu amechana Quran, hapana. Alisema kuwa amemfukuza kazi kwa sababu "HATUWEZI KUKAA NA WAFANYAKAZI WAPUMBAVU".Niliipenda sana hii
 
katiba inasema raisi hatatakiwa kufuata sheria za bunge zinazotoa mwongozo wa kuwaondoa wafanyakazi soma sheria kijana acha siasa

Sent using Jamii Forums mobile app
tatizo lako unasoma hivi vifungu in isolation! Kifungu hicho unachokimamania hakimpi Rais mamlaka ya kufanya atakavyo katika kumfukuza mfanyakazi! Nadhani tushie hapo maana tuko tofauti kabisa mimi na wewe!
 
Kwani imethitika kuwa kweli alichana kuruani? Usije kuta alichana makaratasi yenye maandishi ya lugha ya kiarabu halafu watu wanasema ni kuruani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu Rais mimi nilimsikiliza usiku wakati wa marudio ya Hotuba yake. Rais hakusema kuwa amemfukuza kazi kwa sababu amechana Quran, hapana. Alisema kuwa amemfukuza kazi kwa sababu "HATUWEZI KUKAA NA WAFANYAKAZI WAPUMBAVU".Niliipenda sana hii
Upumbavu wa huyo jamaa ni upi kama sio wa kuchana QURAN ambao kila mtu ameuona?
 
Upumbavu wa huyo jamaa ni upi kama sio wa kuchana QURAN ambao kila mtu ameuona?
Mpumbavu ni mtu ambaye hajui, na hajui kuwa hajui. Mimi ninavyoona, Rais amemfukuza kazi kwa sababu huyu mtu hajui kuwa Quran ni nini, na pia hajui kuwa hajui kuwa Quran ni nini. Kwa hiyo ni mpumbavu!
 
Dibagula alichana na kuikanyaga Biblia?

Kusema Yesu siyo Mungu siyo ishu maana imeandikwa hivyo kwenye Quran kuwa Yesu siyo Mungu.

hata Mashahidi wa Yehova wanasema Yesu siyo Mungu.
Sio mashahidi wa Yehova wanasema bali ni Biblia ndiyo inasema hivyo!
 
Back
Top Bottom