Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kwa mtu mwenye akili za chini, atamsifia Rais Magufuli kwa kutangaza kwamba mwaka huu hatutakuwa na sherehe za uhuru ili kuokoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Dodoma.
Kwa mtu mwenye akili ya kufikiria, atajiuliza, hivi inakuwaje tunakuwa hatuna mipango hususan inayotia ndani kutengwa kwa fedha kwa ajii ya ujenzi wa miundo mbinu muhimu kama Hospitali Dodoma?
Naingia sana wasiwasi, kwamba inafikia mahali mambo muhimu kwa ajili ya miundo mbinu na miradi ya nchini hayapangwi kwa kufuata uratatibu maalum, bali inakuwa ni uamuzi kutokana na hisia za Rais Magufuli.
Kuamua kujenga barabara ndefu ya kiwango cha lami kwa ghafla na kumpigia simu Mkurugenzi wa TANROAD, au kuamua ghafla kwamba fedha za uhuru ndio zikajenge Hospitali, ni wonyesho dhahiri wa udhaifu mkubwa sana katika uongozi wa Magufuli katika kuwa na mipango hususa ya miradi ya maendeleo nchini. Magufuli asifikiri hiyo inamfanya kuwa raisi bora au mzalendo. Ni udhaifu katika uongozi.
Labda tungemuelewa Magufuli ikiwa angesema fedha za sherehe za Uhuru zinaenda kusaidia emergency fulani, kama mafuriko, kipindupindu kimezuka mahali, nk.
Lakini kupeleka fedha za sherehe kwenye kujenga Hospitali, kitu ambacho kinapaswa kupangwa na kutengewa fedha toka mapema, ni udhaifu mkubwa katika kupanga. Kwa namna hii kuna siku tutauza Ikulu ili tumalizie SGR.
Hatuwezi kufanikiwa kufanya mambo haya kwa kutegemea Rais Magufuli siku hiyo kawaza nini kichwani, au kasukumwa na nini kabla hajachukua simu na kutoa agizo mradi fulani mkubwa nchini utekelezwe fedha atajua kwa kuzipata kwa kuwa yeye ndio raisi. Huko ni kuendesha nchi kama duka la baniani. Hayo ni mambo ya kichifu, siyo nchi iliyo Jamhuri.