Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,710
- 9,063
Tukisema Magufuli hafai kuongoza hata kijiji mafisi wa Lumumba wanabisha!Kwa mtu mwenye akili za chini, atamsifia Rais Magufuli kwa kutangaza kwamba mwaka huu hatutakuwa na sherehe za uhuru ili kuokoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Dodoma. Kwa mtu mwenye akili ya kufikiria, atajiuliza, hivi inakuwaje tunakuwa hatuna mipango hususa inayotia ndani kutengwa kwa fedha kwa ajii ya ujenzi wa miundo mbinu muhimu kama hospitali Dodoma?
Naingia sana wasiwasi, kwamba inafikia mahali mambo muhimu kwa ajili ya miundo mbinu na miradi ya nchini hayapangwi kwa kufuata uratatibu maalum, bali inakuwa ni uamuzi kutokana na hisia za Rais Magufuli. Kuamua kujenga barabara ndefu ya kiwango cha lami kwa ghafla na kumpigia simu mkurugenzi wa TANROAD, au kuamua ghafla kwamba fedha za uhuru ndio zikajenge hospitali, ni wonyesho dhahiri wa udhaifu mkubwa sana katika uongozi wa Magufuli katika kuwa na mipango hususa ya miradi ya maendeleo nchini. Magufuli asifikiri hiyo inamfanya kuwa raisi bora au mzalendo. Ni udhaifu katika uongozi.
Hautuwezi kufanikiwa kufanya mambo haya kwa kutegemea Rais Magufuli siku hiyo kawaza nini kichwani, au kasukumwa na nini kabla hajachukua simu na kutoa agizo mradi fulani mkubwa nchini utekelezwe fedha atajua kwa kuzipata kwa kuwa yeye ndio raisi. Huko ni kuendesha nchi kama duka la baniani. Hayo ni mambo ya kichifu, siyo nchi iliyo jamhuri.
Hivi huyu Magufuli anaposema NCHI NI TAJIRI SANA huwa anamdanganya nani?FEDHA ZIKO WAPI? Maana kama nchi ina fedha ni Tajiri sana inakuweje Rais anahamisha Fedha iliyopangwa kwa kazi maalumu na kuipeleka kwengine. What is Budget???
Nini maana ya BAJETI KUU YA SERIKALI inayopangwa na Serikali kupitia Bunge lake??
Huu utawala ni wa hovyo sana kuwai kutokea Tanzania......!!!!!!