Rais Magufuli kuondoa sherehe za Uhuru ili fedha zikajenge hospitali Dodoma si jambo la sifa, ni kuonesha Serikali haina mipango hususan ya maendeleo

Rais Magufuli kuondoa sherehe za Uhuru ili fedha zikajenge hospitali Dodoma si jambo la sifa, ni kuonesha Serikali haina mipango hususan ya maendeleo

Hivi hawa watoto wanaokua sasahivi wajifunze nini juu ya Sherehe za Uhuru?

Ikiwa Uhuru hawakuuona na Sherehe zake wasizione?

Inchi inayoghairi Sherehe za kitaifa kwa Mujibu wa Katiba ni Nchi mfu.
Nyie ndio wapiga hela mnaotaka kupewa tenda za t-shirts mapambo chakula no

Magu amewashtukia
 
Hakuna mtu mwizi kama jiwe in this country since 09th December 1961.
 
Ajabu sana.halafu kumbe hata ile hospital ya uhuru bado haijakamilika mpka sasa (wanasema ujenzi umefikia asilimia 94).

Ni wajinga tu ndio watakaoshangilia .
Yaani walitenga fedha za kutosha za sherehe za uhuru wakaacha kutenga fedha za kutosha za ujenzi wa hospitali Dodoma hadi Rais aje kuamuru fedha za uhuru zikajenge hospitali; ajabu sana hii!

Halafu kama ni uhitaji wa mahospitali na huduma nyingine za kijamii mahitaji ni mengi; ni bora sasa kama kinachokausha hazina ya taifa ni sherehe za uhuru imefika wakati sasa sherehe hizo zifutwe kabisa ili kupata fedha za kujenga na kuboresha huduma zote za jamii.
 
Kwa mtu mwenye akili za chini, atamsifia Rais Magufuli kwa kutangaza kwamba mwaka huu hatutakuwa na sherehe za uhuru ili kuokoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Dodoma. Kwa mtu mwenye akili ya kufikiria, atajiuliza, hivi inakuwaje tunakuwa hatuna mipango hususa inayotia ndani kutengwa kwa fedha kwa ajii ya ujenzi wa miundo mbinu muhimu kama hospitali Dodoma?

Naingia sana wasiwasi, kwamba inafikia mahali mambo muhimu kwa ajili ya miundo mbinu na miradi ya nchini hayapangwi kwa kufuata uratatibu maalum, bali inakuwa ni uamuzi kutokana na hisia za Rais Magufuli. Kuamua kujenga barabara ndefu ya kiwango cha lami kwa ghafla na kumpigia simu mkurugenzi wa TANROAD, au kuamua ghafla kwamba fedha za uhuru ndio zikajenge hospitali, ni wonyesho dhahiri wa udhaifu mkubwa sana katika uongozi wa Magufuli katika kuwa na mipango hususa ya miradi ya maendeleo nchini. Magufuli asifikiri hiyo inamfanya kuwa raisi bora au mzalendo. Ni udhaifu katika uongozi.

Labda tungemuelewa Magufuli ikiwa angesema fedha za sherehe za Uhuru zinaenda kusaidia emergency fulani, kama mafuriko, kipindupindu kimezuka mahali, nk. Lakini kupeleka fedha za sherehe kwenye kujenga hospitali, kitu ambacho kinapaswa kupangwa na kutengewa fedha toka mapema, ni udhaifu mkubwa katika kupanga. Kwa namna hii kuna siku tutauza Ikulu ili tumalizie SGR!

Hautuwezi kufanikiwa kufanya mambo haya kwa kutegemea Rais Magufuli siku hiyo kawaza nini kichwani, au kasukumwa na nini kabla hajachukua simu na kutoa agizo mradi fulani mkubwa nchini utekelezwe fedha atajua kwa kuzipata kwa kuwa yeye ndio raisi. Huko ni kuendesha nchi kama duka la baniani. Hayo ni mambo ya kichifu, siyo nchi iliyo jamhuri.
Ni kweli hii ni hatari,kama mkuu wa Nchi anapindua aprovals za Bunge bila wao kuhusika.Hiv budget si huwa inatungiwa sheria ndiyo inaanza kutumika?.ama nakosea,kuna kitu kinaitwa "apropriation act" Hii huwa ni nini?
 
Sherehe za Uhuru zinamaliza hela tu. Hongera Rais Magufuli kwa kuliona hilo. Hii nchi imepigwa sana enzi za Kikwete kupitia visherehe vya ajabu ajabu.
Huyo mwanaume uliyenaye anapata taabu sana kukuelewesha mambo madogo, Kikwete ndiye aliyeanzisha hzo sherehe?
 
Mleta maada na wenzako wa kupinga kila kitu. Saa nyingine mpunguze ujuaji. Umeanza kwa kuita akili ndogo wale watakao unga mkono uamuzi huu. Wahenga walipatia kusema "werevu mwingi mbele kiza".

Kuna kitu kinaitwa intuition. Kiongozi mzuri pamoja na kufuata taratibu zilizopo anapaswa pia kuwa na utashi wake binafsi umwongoze kuchukua hatua za hapa na pale hata ikiwa hakuagizwa kufanya hivyo.

Uamuzi wa kujenga hospitali hiyo ulikuwa utashi binafsi. Kuna wale Bharti Airtel nao waliunga mkono kwa kuchangia huo ujenzi. Sasa rais kuamua pia kufuta hizo sherehe ili kupata pesa za kununulia vifaa tiba hizo ni akili zake binafsi ambazo kupinga lazima uwe na kawendawazimu flani kichwani.

Miradi inayopangwa iko mingi sana kiasi kwamba kudai kuwa hii miradi miwili mitatu ya utashi binafsi inaakisi mwelekeo wa jamii nzima kuwa mambo yetu hayako planned ni zaidi ya ujuha! Labda kama mnaigiza.

Natambua namna vichwa vyenu viko brainwashed na mfumo wa maisha wa kiliberali ambao mamlaka pekee makubwa kiongozi wa nchi anapaswa kuwa nayo ni kutangaza vita au kuitangazia vikwazo nchi flani. Hapo ndio roho zenu husuuzika nyie watumwa.
Hizo Akili binafsi angezitumia Wakati bajeti inapangwa, siyo hivi.
 
Sherehe za Uhuru zinamaliza hela tu. Hongera Rais Magufuli kwa kuliona hilo. Hii nchi imepigwa sana enzi za Kikwete kupitia visherehe vya ajabu ajabu.
Kumbukumbu ya UHURU WA TANGANYIKA ni Sherehe za AJABUAJABU?

Unataka VIZAZI VIJAVYO VISIIJUE HISTORIA JUU YA TANGANYIKA?
 
Comments za watu kwenye huu uzi zinasikitisha sana.
Sijui kwa nini baadhi yetu hatujifunzi haya mambo! Yaani watu wanaandika mi comments mirefu as jadili jambo la maana.
Hivi zaidi ya kutaka misifa na populism kuna lipi la ajabu?
 
kwaio Mh Rais hataki watu wake tushuhudie kwata la kufa mtu pale jamhuri na makomandoo wakifanya yao?
 
Sherehe za Uhuru zinamaliza hela tu. Hongera Rais Magufuli kwa kuliona hilo. Hii nchi imepigwa sana enzi za Kikwete kupitia visherehe vya ajabu ajabu.
Ila wewe unakataga keki kila mwaka birthday yako na mnaalikana na mashosti kula keki na mapaja ya jimbi
 
Basi siku hizi Serikali hii ikifanya kitu cha maana namna gani lazima mtauliza - kilikuwa kwenye bajeti au kimepitishwa na Bunge na maswali mengine ya hovyo hovyo kama hayo! Kama una chanzo cha ziada na ukikitumia kwa maendeleo, kuna ubaya gani!?

Hivi ni lazima kiende Bungeni na kupangiwa bajeti, by the way budget nini, kama siyo dira tu ya kukuonyeshA wapi pa kupata pesa na namna ya kuzitumia hizo pesa!?

Kama umezipata kutoka kwenye makanikia au Barrick au Buzwagi, matumizi yoyote, as long as ni kwa maendeleo, BASI NI HALALI!
Rudi shule uweke akili na uelewa wako wa mambo vizuri.
 
Tukisema Magufuli hafai kuongoza hata kijiji mafisi wa Lumumba wanabisha!
Hivi huyu Magufuli anaposema NCHI NI TAJIRI SANA huwa anamdanganya nani?FEDHA ZIKO WAPI? Maana kama nchi ina fedha ni Tajiri sana inakuweje Rais anahamisha Fedha iliyopangwa kwa kazi maalumu na kuipeleka kwengine. What is Budget???
Nini maana ya BAJETI KUU YA SERIKALI inayopangwa na Serikali kupitia Bunge lake??
Huu ni utawala ni wa hovyo sana kuwai kutokea Tanzania......!!!!!!
Kabla ya Awamu hii isiyo na mwelekeo, siku ya Uhuru ilikuwa inaadhimishwa kwa kuwaonyesha wananchi Serikali yao, Mashirika ya Umma na hata Sekta Binafsi wamefanya nini kipindi cha mwaka husika. Wafanyakazi waliandamana na magari yao yakiwa yamepakia bidhaa zilizozalishwa au zinazouzwa wakapita mbele ya mgeni Rasmi na wageni waalikwa. Hii iliwapa nafasi wananchi kulinganisha maendeleo yaliyopigwa Kati ya mwaka uliopita na huu.
 
Kwa mtu mwenye akili za chini, atamsifia Rais Magufuli kwa kutangaza kwamba mwaka huu hatutakuwa na sherehe za uhuru ili kuokoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Dodoma. Kwa mtu mwenye akili ya kufikiria, atajiuliza, hivi inakuwaje tunakuwa hatuna mipango hususa inayotia ndani kutengwa kwa fedha kwa ajii ya ujenzi wa miundo mbinu muhimu kama hospitali Dodoma?

Naingia sana wasiwasi, kwamba inafikia mahali mambo muhimu kwa ajili ya miundo mbinu na miradi ya nchini hayapangwi kwa kufuata uratatibu maalum, bali inakuwa ni uamuzi kutokana na hisia za Rais Magufuli. Kuamua kujenga barabara ndefu ya kiwango cha lami kwa ghafla na kumpigia simu mkurugenzi wa TANROAD, au kuamua ghafla kwamba fedha za uhuru ndio zikajenge hospitali, ni wonyesho dhahiri wa udhaifu mkubwa sana katika uongozi wa Magufuli katika kuwa na mipango hususa ya miradi ya maendeleo nchini. Magufuli asifikiri hiyo inamfanya kuwa raisi bora au mzalendo. Ni udhaifu katika uongozi.

Labda tungemuelewa Magufuli ikiwa angesema fedha za sherehe za Uhuru zinaenda kusaidia emergency fulani, kama mafuriko, kipindupindu kimezuka mahali, nk. Lakini kupeleka fedha za sherehe kwenye kujenga hospitali, kitu ambacho kinapaswa kupangwa na kutengewa fedha toka mapema, ni udhaifu mkubwa katika kupanga. Kwa namna hii kuna siku tutauza Ikulu ili tumalizie SGR!

Hautuwezi kufanikiwa kufanya mambo haya kwa kutegemea Rais Magufuli siku hiyo kawaza nini kichwani, au kasukumwa na nini kabla hajachukua simu na kutoa agizo mradi fulani mkubwa nchini utekelezwe fedha atajua kwa kuzipata kwa kuwa yeye ndio raisi. Huko ni kuendesha nchi kama duka la baniani. Hayo ni mambo ya kichifu, siyo nchi iliyo jamhuri.
Mataahira ya Lumumba yatakuja hapa!
 
Naona na yeye ndivyo alivyojipambanua kuwa hapendi hayo masherehe sherehe kama lilivyo suala la demokrasia kwake pia bila kificho hapendi.

Lakini yeye kama kiongozi mkuu wa nchi anapaswa kufuata misingi ya sheria na katiba ya JMT imezitambua sherehe hizi ni muhimu katika kutunza historia ya nchi. Aliapa kuilinda na kuitunza katiba hivyo anachofanya ni kinyume na kiapo chake.

Kuendelea kufanya hivi kama kiongozi mkuu ni kuichafua taasisi ya urais. Rais anayejiamulia mambo yake anatengeneza njia ya kuifanya katiba isiginwe na ionekane si kitu cha muhimu ambacho mtu yeyote awaye na mamlaka anaweza kuisigina tu atakavyo. Hii ni dalili isiyo njema kabisa kwa uelekeo wa taifa letu.

Kama ana maono mazuri kwa taifa kupitia sherehe hizi basi ni vyema akafuata utaratibu wa kisheria wa namna ya kufuta sherehe hizi na sio kutuonesha sarakasi zake za uvunjifu wa katiba. Ni rais asiefuata misingi ya utawala bora.
 
Lakini Rais huyu siye muasisi wa kusherehekea sikukuu za kitaifa kwa utaratibu huu uliozoeleka. Ila yeye ana maoni kuwa ni ufujaji wa pesa, kwa hiyo kuzielekeza pesa hizo eneo jingine sioni kama ni jambo baya
 
Back
Top Bottom