Rais Magufuli kuondoa sherehe za Uhuru ili fedha zikajenge hospitali Dodoma si jambo la sifa, ni kuonesha Serikali haina mipango hususan ya maendeleo

Rais Magufuli kuondoa sherehe za Uhuru ili fedha zikajenge hospitali Dodoma si jambo la sifa, ni kuonesha Serikali haina mipango hususan ya maendeleo

Kiukweli hizi ni dalili za kujichanganya unapokosa fedha. Hata majumbani pesa za christmass tunazipeleka kulipia ada watoto hasa tunaoijali elimu ya watoto wetu kwa kuepuka ile bure mbovu kutokana na ukata.

Unaweza kushinda uchaguzi kibabe lakini huwezi kushinda uchumi kibabe... ndani ya muda mfupi utaonekana kama umepatia lakini punde utatiisha aibu kwa kuvuruga uchumi uliojengwa nakulindwa miaka mingi iliyopita.

- mabenki yanaanguka, mahoteli na maduka makubwa yanakufa, viwanda na makampuni yanafilisika, kilimo kinazorota, bidhaa zinaadimika, ajira zinakosekana, gharama ya maisha inakuwa kubwa nk.

Kufuatia hayo makusanyo ya kodi yatashuka vibaya,misaada toka nje hamna,ushirikiano kimataifa kwenye kiteknolojia,kibiashara,utafiti nk. vinaanguka na taifa litajikuta kwenye dhiki mbaya sana.

Ma mp hawakosoi wanasifu tuu maana wamesaidiwa kufika walipo kwa ubabe wa mkuu wao.
 
hata mimi nampango kuifuta sherehe chrismas pesa tununue tofali sijui wataafiki familia 🤣





iterms
1: mbuzi 2
2: mkungu mmoja wa ndizi
3:stake (mishikaki) 10 kg
4: kuku (15)
5:viungo (nyanya,vitunguu,kabichi,vitunguu swaum, tangawizi,mamasita,giligilani,chumvi,n:k
6:Mkaa
7:gharama ya mchomaji
8:foil
9:mafuta ya kula kg 5 (kwa ajili ya kukangia ndizi)
 
Kanuni ni ileile tengeneza tatizo halafu ibuka useme utalitatua! Mitano 5
 
Sherehe za Uhuru zinamaliza hela tu. Hongera Rais Magufuli kwa kuliona hilo. Hii nchi imepigwa sana enzi za Kikwete kupitia visherehe vya ajabuajabu.
Hata pesa ya uchaguzi ingekwenda kwenye ujenzi wa maendeleo.
Maendeleo hayana chama.
 
Mleta maada na wenzako wa kupinga kila kitu. Saa nyingine mpunguze ujuaji. Umeanza kwa kuita akili ndogo wale watakao unga mkono uamuzi huu. Wahenga walipatia kusema "werevu mwingi mbele kiza".

Kuna kitu kinaitwa intuition. Kiongozi mzuri pamoja na kufuata taratibu zilizopo anapaswa pia kuwa na utashi wake binafsi umwongoze kuchukua hatua za hapa na pale hata ikiwa hakuagizwa kufanya hivyo.
Wewe ndio umepotea hujui ulikotoka wala unaoenda.

Miradi ya kujenga hospitali inafanywa kwa intuition?
 
Aliyetuletea hili jiwe ipo siku atalipa alichotufanyia watz. Haya Mambo Kuna siku tutaambiwa mshahara wa mwezi wa 2 wafanyakazi hawatapewa. Pesa ziende kujenga barabara. Nini maana ya bajeti sasa.
 
Kiongozi yoyote lazima awe na MADARAKA NA MAMLAKA! Hivyo viwili vinatoka kwa MUNGU na hunavyo, basi huwezi kuwa kiongozi. Mfano mzuri ni Lissu hakuwa na vyote viwili, yaani hakupewa na Mungu bali alikuwa anataka kuvilazimisha kupitia rhetorics na noise huko majukwaani na "nyomi" bandia alizoona zikamuaminisha kuwa anaweza kuwa kiongozi - subutu au thubutu!
Kukua umri kuendane na akili pia msikariri maneno hasa ya vitabu vitakatifu mtamkufuru Muumba wenu kwa kukosa hekima. Kwahivyo marais wauaji na madikteta walipata madaraka na mamlaka toka kwa ulomtaja??
Wapo wanaoenda kwa waganga kutafuta uongozi nao unawaelezeaje??
 
Sherehe za Uhuru zinamaliza hela tu. Hongera Rais Magufuli kwa kuliona hilo. Hii nchi imepigwa sana enzi za Kikwete kupitia visherehe vya ajabuajabu.
Mawazo ya chini kabisa haya, hizo pesa zimepelekwa bank??
 
Huyu vipi!? Ndio wale wale wanaosema wanataka maendeleo ya watu siyo vitu! Hivi ni kipi kitendo cha maendeleo - watu kutumia Tshs. 834,742,000/= kwa ajili ya sherehe za uhuru za siku moja au kutumia hizo pesa kujenga miundombinu ya maendeleo kama hiyo hospitalini? Jamani mbona mmevurugikiwa sana hasa baada ya kupigwa kwenye GE ya juzi kiasi hata hamjui nini ni maendeleo na nini ni STAREHE!?
Tatizo ni kwamba watu kama wewe hamna uwezo wa kufikiri. Unasoma lakini huelewi.

Hatukatai kuokoa fedha, tunachokataa ni kutokuwa na mipango. Tunachosema hapa ni kwamba serikali haina mipango na budget ya kujenga hospitali ndio maana inaokoteza. Haya, hospitali ya Dodoma mmeokoteza fedha za Uhuru, na ya Morogoro je, tutauza magari ya Ikulu au ndege ya raisi?
 
Hata pesa ya uchaguzi ingekwenda kwenye ujenzi wa maendeleo.
Maendeleo hayana chama.
Hiyo pesa ya uchaguzi imeleta MAENDELEO makubwa sana kwa kuuonesha ulimwengu kuwa Watanzania wanao utashi wa kutaka maendeleo ya kweli kwa kuchagua viongozi wenye nia na kiu ya kuwaletea maendeleo. Hivyo ni kweli Tshs. 265.34/= bilioni walizopewa NEC na Serikali yetu zimeleta chanzo kikubwa cha maendeleo kwa kutuletea Rais, Wabunge na Madiwani wataka maendeleo.
 
Umeelewa uzi lakini?
Shida sio sherehe kuahirishwa shida ni mipango ya kujenga hospital ilikuwa hakuna mpk isubiri fedha za emergence zilizotengwa kwa ajiri ya sherehe za uhuru.?
Mkuu umetoa jibu ambali limefupisha thread yangu katika sentensi moja. Wewe ni kipanga sana.

Yaani kuna watu yeboyebo humu hawaelewi kabisa thread lakini wanakuwa kimbelembele kujibu utafikiri kuachia round ya kwanza baada ya kukaa jela miaka mitano!
 
Aliyetuletea hili jiwe ipo siku atalipa alichotufanyia watz. Haya Mambo Kuna siku tutaambiwa mshahara wa mwezi wa 2 wafanyakazi hawatapewa. Pesa ziende kujenga barabara. Nini maana ya bajeti sasa.
Huyu naye vipi!? Umetokea kwenye njozi na kuingilia mada au unataka useme kwa kusema tu? Bajeti ni dira tu ya namna ya kupata fedha na namna ya kuzitumia; bajeti inaweza kupangwa Ikulu au Hazina au BOT au Bungeni na ikatumika popote na vyovyote ili mradi inafaidia watu wa Tanzania.
 
Ni kweli jambo hili halijakaa sawa!

Vilvile ni lazima ieleweke kuwa kila mradi una wizara yake, na kila wizara ina fungu lake la bajeti, hivyo suala la bajet ya sherehe za Uhuru haliingiliani kwa namna yoyote na bajet ya wizara ya afya!

Kama vipi tungerekebisha mfumo wa kuzisherekea sherehe hizo ikiwezekana zisheherekewe kitaifa kila mahali lakini kila taasis isherekee sherehe hizo mahala walipo, Mikoani na halmashauri ziadhimishe sherehe hizo palepale walipo bila kuingia gharama kubwa!

Hili suala la kuadhimisha kitaifa kwenye mkoa flani kubebelea viongozi na makundi ya watu kupeleka huko ndiyo yanaongeza gharama kiasi cha kufikia hatua ya kuilazimisha serikali kuanza kukuna kichwa kuhusu fedha itagharamia sherehe hizo.
 
Uhuru tulishaupata 1961.
Na sintashangaa hata wazazi wako walikuwa hajazaliwa. Kwa hiyo si muhimu kwako

Lakini issue ya thread sio fedha za Uhuru, issue ni kwamba fedha za vitu kama kujenga hospitali zinapaswa kuwa na mipango maalum, sio kuokoteza. Nisingemkosoa Magufuli kama angesema tunatumia fedha za Uhuru kwa jambo la emergency, labda mafuriko, nk. Lakini kujenga hospitali?

Nyie dotcom hamna uwezo wa kuelewa maandishi. Akili imeshikilia uhuru uhuru. Hamna uwezo wa kusoma na kuelewa hata paragraph moja mnarukia rukia tu kujibu, mmezowea computer games kuwahi kuua adui!
 
Kukua umri kuendane na akili pia msikariri maneno hasa ya vitabu vitakatifu mtamkufuru Muumba wenu kwa kukosa hekima. Kwahivyo marais wauaji na madikteta walipata madaraka na mamlaka toka kwa ulomtaja??
Wapo wanaoenda kwa waganga kutafuta uongozi nao unawaelezeaje??
Waisraeli walimlilia Mungu awape WAAMUZI na WAFALME. Akawapa akina SAULI,yule Mfalme aliyetaka kumuua Daudi! Sijui unajua kisa hicho!? Mamlaka na Madaraka ya SAULI yalitoka kwa Mungu! Si unajua aliwafanyaje Waisraeli au Wayahudi!? Kimsingi, ndiyo mamlaka na madaraka YOTE yanatoka kwa Mungu kwa nia na makusudi mbalimbali kwa muda na wakati apendao Yeye, Mungu wetu. Hili suala ni pana tena la kiimani, siwezi kuliendeleza humu zaidi ya hayo machache hapo juu. Ila kila mtu anayo haki ya kutoa tafsiri yake kwa kila kiongozi, ikiwa na wewe kusema chochote juu ya Rais wetu Dr.John Magufuli. Hakuna wa kukuzuia, hiyo ni haki yako!
 
Wewe ndio umepotea hujui ulikotoka wala unaoenda.

Miradi ya kujenga hospitali inafanywa kwa intuition?
Intuition sharti itumike wapi na wapi? Dodoma tayari mpango wa serikali ulikuwa kwenye hospitali ya BWM. Yeye rais kaona iongezwe nyingine tena kwa pesa ambayo ingetumika siku mbili au tatu tu! Sasa hapo aliyepotea nani kati yetu.
 
Back
Top Bottom