Rais Magufuli kuondoa sherehe za Uhuru ili fedha zikajenge hospitali Dodoma si jambo la sifa, ni kuonesha Serikali haina mipango hususan ya maendeleo

Rais Magufuli kuondoa sherehe za Uhuru ili fedha zikajenge hospitali Dodoma si jambo la sifa, ni kuonesha Serikali haina mipango hususan ya maendeleo

Sherehe za Uhuru zinamaliza hela tu. Hongera Rais Magufuli kwa kuliona hilo. Hii nchi imepigwa sana enzi za Kikwete kupitia visherehe vya ajabu ajabu.
Kwahiyo sherehe za uhuru alianzisha Kikwete du!

Kaazi kwelikweli ... kuna wakati unaweza kuruka MKOJO ukakanyaga MAVI japo vyote uchafu ila MKOJO una nafuu kuliko MAVI
 
Haya ni maigizo tu mnapanga bajeti wenyewe mnaikamilisha na mnatangazia umma kwamba nikiasi Fulani baada ya wiki inajtokeza taasisi nyingine ndani ya serikali hiyo hiyo inasema hatuta ipeleka kule bali tunaileta huku, wakati bajeti inapangwa walikuwa wapi?
 
Waisraeli walimlilia Mungu awape WAAMUZI na WAFALME. Akawapa akina SAULI,yule Mfalme aliyetaka kumuua Daudi! Sijui unajua kisa hicho!? Mamlaka na Madaraka ya SAULI yalitoka kwa Mungu! Si unajua aliwafanyaje Waisraeli au Wayahudi!? Kimsingi, ndiyo mamlaka na madaraka YOTE yanatoka kwa Mungu kwa nia na makusudi mbalimbali kwa muda na wakati apendao Yeye, Mungu wetu. Hili suala ni pana tena la kiimani, siwezi kuliendeleza humu zaidi ya hayo machache hapo juu. Ila kila mtu anayo haki ya kutoa tafsiri yake kwa kila kiongozi, ikiwa na wewe kusema chochote juu ya Rais wetu Dr.John Magufuli. Hakuna wa kukuzuia, hiyo ni haki yako!
Wewe utakuwa unafikiria kizama za agano lakaleee BC (Before Christ) ndomana nakwambia usikariri maandiko lielewe neno! Viongozi wa dunia yaleo wengi hupitia kwa waganga na hujilinda kwamahirizi hatakama j2 unawaona viti vyambele kanisani.
 
Mleta mada uelewa wako wa mambo uko chini sana. Nenda kasome kuna kitu kinaitwa “Mid Year Review” au “Budget Reallocation” vitakusaidia kuelewa. Hivyo vitu unaweza kujisomea kwenye internet au tafuta Sheria ya Bajeti. Hayo mambo Serikali inafanya kila mwaka kama kuna uhitaji wa kuhamisha Bajeti kutoka Activity A kwenda Activity B.
Kwa hiyo kwa akili yako, Magufuli kupeleka hela za uhuru kwenda kujenga hospitali ni budget reallocation? Ambayo mlifanya wewe na Magufuli au yeye na Dotto?
 
Uhuru wa Tanganyika hautakiwi tena kukumbukwa ,kwa vile kuna Tanzania sasa. Siku muhimu hapa ni Ya Muungano tuu.
Hamujui kuwa Nchi inaelekea kwenye serikali Moja?
Sooon muswaada utapelekwa bungeni kuanzisha mchakato wa serikali moja.
Mbona hata sherehe za Muungano alishawahi kuzifutilia mbali?
Soma hiyo kamanda:
 
Kwa mtu mwenye akili za chini, atamsifia Rais Magufuli kwa kutangaza kwamba mwaka huu hatutakuwa na sherehe za uhuru ili kuokoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Dodoma. Kwa mtu mwenye akili ya kufikiria, atajiuliza, hivi inakuwaje tunakuwa hatuna mipango hususa inayotia ndani kutengwa kwa fedha kwa ajii ya ujenzi wa miundo mbinu muhimu kama hospitali Dodoma?

Naingia sana wasiwasi, kwamba inafikia mahali mambo muhimu kwa ajili ya miundo mbinu na miradi ya nchini hayapangwi kwa kufuata uratatibu maalum, bali inakuwa ni uamuzi kutokana na hisia za Rais Magufuli. Kuamua kujenga barabara ndefu ya kiwango cha lami kwa ghafla na kumpigia simu mkurugenzi wa TANROAD, au kuamua ghafla kwamba fedha za uhuru ndio zikajenge hospitali, ni wonyesho dhahiri wa udhaifu mkubwa sana katika uongozi wa Magufuli katika kuwa na mipango hususa ya miradi ya maendeleo nchini. Magufuli asifikiri hiyo inamfanya kuwa raisi bora au mzalendo. Ni udhaifu katika uongozi.

Labda tungemuelewa Magufuli ikiwa angesema fedha za sherehe za Uhuru zinaenda kusaidia emergency fulani, kama mafuriko, kipindupindu kimezuka mahali, nk. Lakini kupeleka fedha za sherehe kwenye kujenga hospitali, kitu ambacho kinapaswa kupangwa na kutengewa fedha toka mapema, ni udhaifu mkubwa katika kupanga. Kwa namna hii kuna siku tutauza Ikulu ili tumalizie SGR!

Hatuwezi kufanikiwa kufanya mambo haya kwa kutegemea Rais Magufuli siku hiyo kawaza nini kichwani, au kasukumwa na nini kabla hajachukua simu na kutoa agizo mradi fulani mkubwa nchini utekelezwe fedha atajua kwa kuzipata kwa kuwa yeye ndio raisi. Huko ni kuendesha nchi kama duka la baniani. Hayo ni mambo ya kichifu, siyo nchi iliyo jamhuri.
Pesa inaenda kutumika kudidimiza demokrasia kurejesha mfumo wa chama kimoja
 
Huyu vipi!? Ndio wale wale wanaosema wanataka maendeleo ya watu siyo vitu! Hivi ni kipi kitendo cha maendeleo - watu kutumia Tshs. 834,742,000/= kwa ajili ya sherehe za uhuru za siku moja au kutumia hizo pesa kujenga miundombinu ya maendeleo kama hiyo hospitalini? Jamani mbona mmevurugikiwa sana hasa baada ya kupigwa kwenye GE ya juzi kiasi hata hamjui nini ni maendeleo na nini ni STAREHE!?
Hujaelewa anaongelea nini! Omba watu wakufafanulie.
 
Wewe utakuwa unafikiria kizama za agano lakaleee BC (Before Christ) ndomana nakwambia usikariri maandiko lielewe neno! Viongozi wa dunia yaleo wengi hupitia kwa waganga na hujilinda kwamahirizi hatakama j2 unawaona viti vyambele kanisani.
Ndiyo maana nimesema kila mtu anayo haki yake ya kutoa mawazo, maoni na hata maamuzi on anybody. Hiyoni haki ya kila mmoja wetu. Pia tafsiri vivyo hivyo!
 
Back
Top Bottom