Rais Magufuli kuvunja Jiji la Dar es Salaam

Yan akivunja maana yake kutakuwa hakuna Dar es Salaam. Au nimeelewaje! Badala yake ilala ndo itakuwa jiji kama sasa tunavosema jiji la dar es salaam. Niko sahihi au.
Anamaanisha kuvunja halmashauri ya jiji
 
He! Kwahiyo kinondoni, temeke, kigamboni ziwe manispaa alafu Ilala ndio jiji?

So jina la Dar Es Salaam ndio litakuwa kwishney?
Wale madiwani wanaokaa vikao vya jiji hawamwakilishi yeyote pale tofauti na madiwani wa manispaa.
 
'kwanza hawakuchaguliwa na wananchi' Kaanza kutoboa siri
Shetani hana rafiki , Mambosasa alipotetea kura za mabegi Kawe tulimpinga lakini watu hawakutuelewa , pembe la ng'ombe halifichiki , leo aliyewatuma karopoka mchana wa jua kali !
 
hapana amesema Dsm itabaki kuwa jiji lkn kutakuwa na halmashauri moja tuu ndiyo itakayobeba jiji haalmashauri nyingine zote zitaondolewa hadhi ya jiji
binafsi sijaelewa itafanyikaje
Nafikiri unaweza kusoma post yangu. Miji mingi duniani inakua na mambo mawili. Jambo la kwanza ni kuteua Urban proper na kuifanya ni Jiji na pembezoni wanaipa Metropilitan Areas. Nilitoa mfano wa Maputo, Maputo ni Jiji kuu la nchi ya Msumbiji lakini pia kuna Jimbo la Maputo, ambalo mji mkuu wa jimbo ni Matola, lakini ni hapo hapo Maputo pembezoni na hawaingiliani kiutawala na jiji la Maputo, na umbali kutoka Maputo kama hakuna foleni ni dk 30 tu unakua umeingia Jijini Maputo. Hii pia ipo Jiji la Kinshasa(Gombe) na jimbo la Kinshasa, vyote vikiwa mji mmoja lakini Mamlaka tofauti.

Ama aina nyingine ni ile ya kuongeza eneo ili kuipa hadhi kubwa zaidi ya Jiji, yaani Agglemeration(spelling) na Corbunation(spelling Check) kama ilivyo kwa Jiji kuu la Lagos na J'burg.

Mfumo huu mimi niliutegemea ili kukuza jiji, kwa mfano Kisemvule, Vikindu, Mapinga, Mlandizi, hadi Kibaha zote zingechukuliwa na kutengenezwa GREAT DAR ES SALAAM.
 
Huwezi kidhoofisha dar ukakuza mwanza huku ni kujifurahisha tu kwani Dar ni kila kitu
 
Napongeza uamuzi wa kulivunja Halmashauri ya Jiji maana lilikuwa redundant.

Lakini mtu anayeelewa anijuze.

Mimi nikifikiri JIJI ni Halmashauri inayo comprise madiwani wa Halmashauri za Kinondoni, Temeke, Ilala na Kigamboni.

Wote ambao wamechaguliwa na watu lakini JIJI bado sijui kama linawajibika moja kwa moja kwa wananchi.

Mwenye kuelewa ufafanuzi please.
 
Shanwe kwa rais ambae ni juzi tu hapa amesimama na kusema siku ina masaa 48! Clip inasambazwa kwa kasi mno na watu wanapata sababu ya kucheka na kufurahi!
 
is it?
 
Exactly!

New York City inside New York.

Manchester City inside (Great) Manchester.

Cairo inside (Great) Cairo.
Wakati mwingine ni vizuri kuficha ujinga badala ya kuleta hadharani kwa kuwa mnaunga mkono ujinga. New York City na New York, kama ilivyo Washington DC na Washington ni vitu viwili tofauti, mawili ni Majiji na mawili ni Majimbo Kati ya Majimbo 50 ya Marekani ndo maana ukitaja au kuulizia Jiji la New York lazima uongeze City vivyo hivyo Washington DC (District of Columbia) ni Makao Makuu ya Marekani na Majiji yote yako karibukaribu mashariki mwa Nchi. Majimbo ya Washington na New York yako karibukaribu Magharibi mpakani na Bahari ya Pacific lakini yako mbali sana na hayo Majiji yaliyopo karibu na Bahari ya Atlantic. Waunga mkono juhudi wasingekuwa vilaza wangekuwa wanajua vizuri Jimbo la New York maana ndiko yanatengenezwa madege ya Magufuli ya Dreamliner ambayo wanatuimbia na kuturingia kila siku yakiwa yamepark tu kama ya maonyesho. Greater Manchester (au Jiji lolote) ni eneo lote ndani ya mipaka iliyotengwa kwa ajili ya Jiji lililopo na upanuzi wa baadaye. Someni muachane na ujinga!
 
Hebu kumbuka Keenja alivyoteuliwa kuwa Mkurugenzi wa jiji , hiki ndicho anachokitaka jiwe , kuna mtu mmoja wa kitengo alishanivutia uzi kunidokeza .

Kumbuka kwamba mgogoro wa Meya anaousema huyu wa sasa ndio pia ulikuwa chanzo wakati wa Mkapa , ambapo mgombea wa udiwani wa kata ya Gerezani au Kariakoo wa UDP ndugu Abbas Mtemvu alimwangusha Mahakamani aliyekuwa mshindi kwenye udiwani wa kata hiyo na ambaye ndiye aliyekuwa Meya wa jiji , Kitwana Kondo na kumvua umeya ( Hadithi ni ndefu )

Wakubwa wakachukia wakaamua kuvunja halmashauri na kujitwalia ulaji
 
Tutakuwa na Dar Metropolitan. Ikiwa na jiji la Ilala, Manispaa ya Kino, Ubungo, TMK na Kiga.
 
Mimi na wewe nani wakuficha ujinga?!

Hii thread inahusu jiji la Dar es Salaam na sio siasa zenu hasa "...kwa kuwa mnaunga mkono ujinga".

Ni vyema kufahamu maana ya approx. katika uhalisia sio kuishi kwa bahati nasibu, kukalili na kuendesha maisha yako kwa siasa.

Mdau CHAZA ameeleza namna na mgawanyo wa jiji na miji/canton/eneo la kijumla linavyokuwa na kutolea mfano Maputo jiji na Maputo jimbo (Mkoa/Eneo) sawia na Kinshasa jiji na Kinshasa jimbo.

Na mimi kutolea mfano wa kijumla New York City ni jiji na New York ni jimbo, Manchester City au ikifahamika kama City of Manchester ni jiji na Great Manchester ni jimbo (Mkoa,Eneo) same kwa Cairo ni jiji ndani ya jimbo kuu la Cairo.

Wewe uliyeficha ujinga unamaanisha nini katika ujumbe wako?
 
Ila wahusika wameangalia mgogoro wa kiutawala, mapato na masilahi tu. Basi wangevunja na kulipa jiji la Dar es Salaam special status. Ila kinachoondolewa ni ile halmashauri ya jiji sio status ya jiji. Wangeondoa ile halmashauri then hizi zikaendelea kubaki kama manispaa zinazounda jiji la DSM.
 
Hawakuchaguliwa na wananchi ?Hapo sijaelewa. Au kwenye udiwani kuna viti maalum ?Pia Ilala kuwa Jiji sababu ni nini?
Madiwan wa jiji la Dar wanatoka kwenye manispaa zotë nadhan kila manispaa inachagua madiwan watano kuingia kwenye jiji hio ndo concept ya mh rais. Hawachaguliw moja kwa moja na wananchi kwenda jiji
 
Ikishakua hivyo impact yake ni ipi hasa kiujumla? Kwenye nyanja ya uchumi na social services..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…