Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Itakuwa haina haka kabaraza kanakojiita halmashauri ya jiji. Unless thinkers waliofanya master minding, hawakufikiria vizuri.Ambalo tofauti yake na hili la sasa ni nini?
Kwahiyo Ilala inakuwa Jiji ndani ya mkoa wa Dsm, right? Ilala kama Ilala pekee inayo sifa ya kuwa Jiji?Itakuwa haina haka kabaraza kanakojiita halmashauri ya jiji. Unless thinkers waliofanya master minding, hawakufikiria vizuri.
Nilichoelewa mimi ni kwamba hiyo administration inaondolewa kwa kuwa imeonekana haina kazi za msingi za kufanya.
Unaambiwa siku aliposema siku ni masaa 48 hakuna hata aliyecheka pale kanisaniShanwe kwa rais ambae ni juzi tu hapa amesimama na kusema siku ina masaa 48! Clip inasambazwa kwa kasi mno na watu wanapata sababu ya kucheka na kufurahi!
Acha utani mkuuKwa nn asipeleke chato kabisa
Hapana Dar litakuwa Jiji kibiashara na siyo kiutendaji! Alyetia uzi huu hakufafanua sana alivyoeleza Mhe Rais! Litabaki jiji la Dar lakini kihalmashauri hakutakuwa na halmashauri ya Jiji la Dar!
Kasomee LGAs, HomboloNapata tabu kuelewa hii concept
Hata mimi nimetoka kapa, najiuliza kwani Dar kuna majiji mangapi mpaka livunjwe moja litengenezwe jingine?Yan akivunja maana yake kutakuwa hakuna Dar es Salaam. Au nimeelewaje! Badala yake ilala ndo itakuwa jiji kama sasa tunavosema jiji la dar es salaam. Niko sahihi au.
Kazi ipoWalichaguliwa na madiwani wa Manispaa za Kinondoni, Ilala, Ubungo, Kigamboni, Temeke! Hawakuchaguliwa na wananchi ndiyo maana walikuwa wana-hang tu bila kuwa na Manispaa. Hata Meya wa Jiji alikuwa ana-hang tu, hakuwa na Manispaa maana kila Manispaa ina Meya wake.
Umeongea vizuri. Swali lingine ni wakazi walishirikishwa vipi kwenye hili?Sina tatizo sana na chochote kinachofanyika..., swali langu hili suala wamekaa wadau wakaangalia pro and cons au ndio kuamka asubuhi na kutoa maamuzi ?
Tusipoangalia kila siku tutakuwa tunapanga na kupanga..., badili na kubadilisha...., ingeandikwa proposal ikapitiwa kwa ufanisi na kuangalia faida na hasara alafu ndio likafanyika jambo (hata kama jambo zuri vipi ni vema kuwahusisha wote pamoja na wananchi kwa kuwafahamisha ) Maamuzi ya kiwa ni ya wote ni rahisi kupokelewa vizuri
Ficha ujinga wako wewe mchagaKatoa siri ya wizi wa kura. Si unajua Meko kuna wakati zinaruka anajisahau?
Hapana, hakusema hivyo.hapana amesema Dsm itabaki kuwa jiji lkn kutakuwa na halmashauri moja tuu ndiyo itakayobeba jiji haalmashauri nyingine zote zitaondolewa hadhi ya jiji
binafsi sijaelewa itafanyikaje
HAWAKUCHAGULIWA NA WANANCHI, YAHANI NI VITI MAALUMU!Nimependa hapo hawakuchaguliwa na wananchi.
Uzuri wa huyu Mjomba huwa hanaga siri kabisa.
Hawakuchaguliwa na wana........Ficha ujinga wako wewe mchaga
Siri imevujaaa.....Akiwa katika uzinduzi wa daraja la juu Ubungo amesema atalivunja jiji na kuipa Ilala hadhi ya jiji na wilaya zingine zibaki kuwa Manispaa.
----
Rais Magufuli ameyasema haya
Nategemea Jiji la Dar es Salaam kulivunja na hii nawaambia hapa ili tutengeneze jiji la eneo fulani, tunaweza tukaifanya Ilala ndio ikawa jiji, ita-depend na mambo yatakavyoenda lakini kuwa na madiwani ambao wanakaa hapa juu, wanachangiwa hela, hawana miradi ya maendeleo, wanakula posho na hawakuchaguliwa na watu, hili nitalikataza.
Kwa hiyo ninalizungumza hapa, wale wanaojiandaa kuwa Mameya wa jiji la Dar es Salaam na wanakaa hawana maeneo wajue hicho kimekwisha. Tunataka Manispaa moja katika jiji la Dar es Salaam ndio ipandishwe hadhi iwe jiji halafu nyingine ziwe manispaa, ni kama ilivyo katika majiji mengine.
Kwahiyo mjiandae kisaikolojia wale waliokuwa wanataka umeya wajiji la Dar es Salaam, meya atapatikana kutoka Ilala au kutoka manispaa mojawapo ya hapa, huu ndio ukweli na ukweli utabaki kuwa ukweli na draft nimeshaletewa na mheshimiwa Jafo, nafikiri nikitoka huku nitakwenda kuisaini.
Ili turahisishe mambo, bajeti ya jiji ambayo haipo, fedha zilikuwa zinapotea ndugu zangu waheshimiwa wabunge, jiji la Dar es Salaam litaendelea kuwepo lakini tutachukua eneo fulani nafikiri Ilala inafaa kuwa jiji, ndio katikati ya jiji la Dar es Salaam, wewe Ubungo utasubiri kwanza kwasababu hata barabara bado hazijatengenezwa tengenezwa lakini nafanya haya ndugu zangu kwa kuangalia matumizi mazuri ya fedha zetu. Mwiso wa Nukuu