Rais Magufuli kuvunja Jiji la Dar es Salaam

Rais Magufuli kuvunja Jiji la Dar es Salaam

Geografia haibadilishwi. Kinachobadilishwa ni kabaraza kalikokuwa kanaitwa halmashauri ya Jiji. Yaani ile Administration inaondolewa.
 
I will be the last person to understand what it means by his statement.
labda Nguruvi3 mtueleweshe concept ya mkoa wa Dsm kuwa jiji na vipi manispaa zake ndio iwe jiji
Heri ya mwaka mpya mwalimu wangu...

Hope all is well with you...

Ok ok ok....
 
Ambalo tofauti yake na hili la sasa ni nini?
Itakuwa haina haka kabaraza kanakojiita halmashauri ya jiji. Unless thinkers waliofanya master minding, hawakufikiria vizuri.
Nilichoelewa mimi ni kwamba hiyo administration inaondolewa kwa kuwa imeonekana haina kazi za msingi za kufanya.
 
Basi ni baba mzuri anazuia mali zisitapanyike kwa kukaa chini nakuona wapi zinapotelea alafu anazuia na kuleta maendeleo. Na wabunge wa viti maalumu pia aangalie jinsi ya kuwapunguza maana hawakuchaguliwa na wananchi.
 
Hapa kuna mchanganyo wa "Halmashuri ya jiji(administration, authority, government, instutution" VS Jiji(jiografia, miundo mbinu, population).
 
Itakuwa haina haka kabaraza kanakojiita halmashauri ya jiji. Unless thinkers waliofanya master minding, hawakufikiria vizuri.
Nilichoelewa mimi ni kwamba hiyo administration inaondolewa kwa kuwa imeonekana haina kazi za msingi za kufanya.
Kwahiyo Ilala inakuwa Jiji ndani ya mkoa wa Dsm, right? Ilala kama Ilala pekee inayo sifa ya kuwa Jiji?
 
Shanwe kwa rais ambae ni juzi tu hapa amesimama na kusema siku ina masaa 48! Clip inasambazwa kwa kasi mno na watu wanapata sababu ya kucheka na kufurahi!
Unaambiwa siku aliposema siku ni masaa 48 hakuna hata aliyecheka pale kanisani
 
Hapana Dar litakuwa Jiji kibiashara na siyo kiutendaji! Alyetia uzi huu hakufafanua sana alivyoeleza Mhe Rais! Litabaki jiji la Dar lakini kihalmashauri hakutakuwa na halmashauri ya Jiji la Dar!

..Inawezekana anayelengwa ni Makonda arudishwe ktk uongozi wa D'Salaam.
 
Yan akivunja maana yake kutakuwa hakuna Dar es Salaam. Au nimeelewaje! Badala yake ilala ndo itakuwa jiji kama sasa tunavosema jiji la dar es salaam. Niko sahihi au.
Hata mimi nimetoka kapa, najiuliza kwani Dar kuna majiji mangapi mpaka livunjwe moja litengenezwe jingine?
 
Walichaguliwa na madiwani wa Manispaa za Kinondoni, Ilala, Ubungo, Kigamboni, Temeke! Hawakuchaguliwa na wananchi ndiyo maana walikuwa wana-hang tu bila kuwa na Manispaa. Hata Meya wa Jiji alikuwa ana-hang tu, hakuwa na Manispaa maana kila Manispaa ina Meya wake.
Kazi ipo
 
Sina tatizo sana na chochote kinachofanyika..., swali langu hili suala wamekaa wadau wakaangalia pro and cons au ndio kuamka asubuhi na kutoa maamuzi ?

Tusipoangalia kila siku tutakuwa tunapanga na kupanga..., badili na kubadilisha...., ingeandikwa proposal ikapitiwa kwa ufanisi na kuangalia faida na hasara alafu ndio likafanyika jambo (hata kama jambo zuri vipi ni vema kuwahusisha wote pamoja na wananchi kwa kuwafahamisha ) Maamuzi ya kiwa ni ya wote ni rahisi kupokelewa vizuri
Umeongea vizuri. Swali lingine ni wakazi walishirikishwa vipi kwenye hili?

Amandla...
 
hapana amesema Dsm itabaki kuwa jiji lkn kutakuwa na halmashauri moja tuu ndiyo itakayobeba jiji haalmashauri nyingine zote zitaondolewa hadhi ya jiji
binafsi sijaelewa itafanyikaje
Hapana, hakusema hivyo.
Magufuli amesema atalivunja jiji la Dar (ambalo kwa sasa linabebwa na manispaa za Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kigamboni) ili kuunda jiji la Ilala (ambalo litabebwa na manispaa ya ilala). Kifupi sana Jiji la Dar litakufa rasmi na manispaa ya Ilala itabadilika na kuwa jiji.
 
Akiwa katika uzinduzi wa daraja la juu Ubungo amesema atalivunja jiji na kuipa Ilala hadhi ya jiji na wilaya zingine zibaki kuwa Manispaa.
----
Rais Magufuli ameyasema haya

Nategemea Jiji la Dar es Salaam kulivunja na hii nawaambia hapa ili tutengeneze jiji la eneo fulani, tunaweza tukaifanya Ilala ndio ikawa jiji, ita-depend na mambo yatakavyoenda lakini kuwa na madiwani ambao wanakaa hapa juu, wanachangiwa hela, hawana miradi ya maendeleo, wanakula posho na hawakuchaguliwa na watu, hili nitalikataza.

Kwa hiyo ninalizungumza hapa, wale wanaojiandaa kuwa Mameya wa jiji la Dar es Salaam na wanakaa hawana maeneo wajue hicho kimekwisha. Tunataka Manispaa moja katika jiji la Dar es Salaam ndio ipandishwe hadhi iwe jiji halafu nyingine ziwe manispaa, ni kama ilivyo katika majiji mengine.

Kwahiyo mjiandae kisaikolojia wale waliokuwa wanataka umeya wajiji la Dar es Salaam, meya atapatikana kutoka Ilala au kutoka manispaa mojawapo ya hapa, huu ndio ukweli na ukweli utabaki kuwa ukweli na draft nimeshaletewa na mheshimiwa Jafo, nafikiri nikitoka huku nitakwenda kuisaini.

Ili turahisishe mambo, bajeti ya jiji ambayo haipo, fedha zilikuwa zinapotea ndugu zangu waheshimiwa wabunge, jiji la Dar es Salaam litaendelea kuwepo lakini tutachukua eneo fulani nafikiri Ilala inafaa kuwa jiji, ndio katikati ya jiji la Dar es Salaam, wewe Ubungo utasubiri kwanza kwasababu hata barabara bado hazijatengenezwa tengenezwa lakini nafanya haya ndugu zangu kwa kuangalia matumizi mazuri ya fedha zetu.
Mwiso wa Nukuu
Siri imevujaaa.....
 
Hakuna namna ya kuliacha jiji liendelee kua kama lilivyo ila kufutafuta mavyeo mengine yasiyokua na tija...
 
Back
Top Bottom