G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Najiuliza ni nini tatizo?
Rais Magufuli alipoingia ikulu mgogoro namba moja aliouanzisha ni sukari. Sukari ghafla ikapanda bei, ikapotea mitaani.
Ilifikia hatua akatoa vitisho kuwa ataliruhusu jeshi likamate sukari iliyofichwa liigawe bure. Nakumbuka hii kauli wapiga zumari waliishangilia sana ila ilikopotelea anakujua mwenyewe.
Kwa miaka yote mitano ya utawala wake sukari haijawahi kupata suluhu na sasa imepotea tena sokoni. Nini tatizo? Mbona huu mgogoro kama una kitu nyuma ya pazia?
Sasa kama kwa miaka yote mitano sukari tu kashindwa kuipatia ufumbuzi, sijagusia sarakasi zake za makinikia? Inakuwaje hili la Corona?