Hotuba ya Mh Rais jana imepokelewa kwa namna tofauti katika ngazi totauti haoa nchini. Tayari Mh. Waziri ameanza utekelezaji, na wananchi bado wana maswali.
Kwa upande wa wananchi. Nilichoona kwa ufupi.
1. Pongezi kwa Mh Rais kuweka bayana hali ya maabara ya taifa.
2. Maswali ambayo hayajajibika kutokana na hotuba
Hoja kuu
Tatizo hasa liko wapi? Je, mashine ni mbovu au watumishi ni wabovu?
Ikiwa mashine ni mbovu.
1. Je, tuliinunua hii mashine au tulipewa zawadi? (a) Kama tulipewa zawadi tuliijaribisha kuhakiki ubora wake KABLA ya kuitumia? Je, mtoa zawadi ALITUZUIA kuijaribisha mashine?
Hata kama ni zawadi ya condom umepewa, huwezi kuitumia bila kuitazama expire date, au imetoboka, maana aliyekupa anaweza kuwa amenuia mabaya, lakini ni UZEMBE wako kuamini bila kuichunguza
(b) Ikiwa tulinunua. Nani aliiagiza? Je, manunuzi yalizingatia ulinganishi wa mashine toka nchi nyingine? Ni kweli kabisa CHINA inajulikana kwa kuwa na vifaa visivyo na viwango. Hili si jambo la leo au mwaka huu. Ni miaka yote. Je, kwa nini tulinunua kwao? Kwa nini hatukununua kwenye nchi zenye mashine zenye viwango bora?
(c) Imekuwaje mashine IRUHUSIWE kutumika bila kuhakikiwa ubora? Nani aliyeamuru itumike? Je, kuna beberu alilazimisha tutumie mashine hii? Walioidhinisha matumizi ya mashine isiyohakikiwa wamechukuliwa hatua gani?
(d) Ikiwa tatizo ni mashine, serikali inakwepaje lawama za kuruhusu mashine zitumike bila uhakiki? Miezi miwili sasa, mashine isiyohakikiwa inachapa kazi. Je, watalaumiwa wachina waliouza mashine mbovu au uzembe wa wizara kutoijaribisha mashine kabla?
(e) Je, nani atalipa fidia waathirika? Waliotoka positive kumbe ni negative? Je, vipi kuhusu waliotoka negative kumbe ni positive na wakaingia mtaani kuambukiza wengine? Nani analipa fidia? Je, hakuna namna ya kumdai fidia beberu aliyeuza mashine mbovu? Je, hatuwezi kuwarudishia watubadilishie?
2. Ikiwa tatizo ni wataalam
(a). Je, Wataalam walipewa elimu ya kutosha kabla ya kuanza kazi?
(b) Je, waliotoa elimu kwa hawa wataalam walikuwa wana uelewa wa kutosha?
(c) Je wataalam walioelimishwa walipimwa kujua ufanisi wao?
(d)Je, wataalam hawa wanatumiwa na akina nani? Je, ni kwa maslahi ya akina nani?
(e) Je, ikiwa wanahusika kucheza na majibu, serikali iko tayari kuwashitaki walipe waathirika fidia?
3. Tatizo ni sampuli?
(a) Je, sampuli zilizopelekwa zinaweza kupimwa na mashine husika?
(b) Je tumejidhihirisha kwamba matokeo yatakuwa sahihi kwa sample ambazo sio? Yaani utumie magazijuto kwenye kutafuta kipenyo cha mduara, hivi inafaa?
Hayo ndiyo niliyokusanya huku na huko
Mtazamo wangu.
Ikiwa mashine ni mbovu, hakika kuna uzembe mkubwa sana, na hauhusu mabeberu. Miezi miwili, unatumia kifaa kibovu kisa zawadi/au vinginevyo.
Ni kama ununue simu kariakoo, kisha ukaitumie weeeeee, baada ya miezi miwili unaona ukipiga picha unaona picha kadhaa zina kivuli, nyingine hazina, unalalamika kariakoo kuna matapeli... Kuna aliyekulazimisha ukanunue KKOO? Kwa nini hukuhakiki kabla?
Matapeli wapo na hawaishi. Umakini ndio unatakiwa. Na wakati mwingine kupendapenda kupokea, au kununua vitu vya bei rahisi kuna madhara yake. Cheap is always expensive