Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Mkuu wa mkoa wa Dsm mh Makonda amewataka wananchi kutoitafsiri vibaya hotuba ya Rais Magufuli na kuacha kula mapapai.

Makonda amesema Rais Magufuli kama mkemia kitaaluma alihisi kuna tatizo kwenye matokeo yanayotangazwa hivyo akaamua kufanya utafiti wa ubora wa kipimo.
Sampuli zilizotumika ni kwa ajili ya kupima ubora wa kipimo na siyo virusi....
huyu nae atulie kamati imeshateuliwa kuchunguza sasa yeye anacoclude vipimo ndio tatizo anauakika...
 
Hili jambo linapaswa kujibiwa Na wataalamu kiuhalisia.Huu Ni wakati wa waandishi Wa habari kuuliza maswali ya msingi kwa wataalamu Wa Afya.
Sitaki kuamini kuwa hujui kuwa waandishi wa Tanzania wanapangiwa maswali ya kuuliza,,
 
Wanabodi,

Kwa mujibu wa Rais Magufuli wametuma sample za mimea na wanyama kwa kuzipa majina ya binadamu kwenye maabara kuu ya Taifa Dar es Salaam kwa siri bila wapimaji kufahamu baada ya kupimwa zimetest positive yaani zina corona

Hapa ndipo Magufuli ameprove uwana-science wake...
Hapa kazi tu
 
Wanabodi,

Kwa mujibu wa Rais Magufuli wametuma sample za mimea na wanyama kwa kuzipa majina ya binadamu kwenye maabara kuu ya Taifa Dar es Salaam kwa siri bila wapimaji kufahamu baada ya kupimwa zimetest positive yaani zina corona

Hapa ndipo Magufuli ameprove uwana-science wake...
Wakati mtoto anasubili Baba afe ili arithi Mali baba nae anasubili mtoto afe ili apangishe chumba anachokaa anachokaa mwanae Hatari sana
 
Watanzania tulishalogwa siku nyingi sana,kila bada ya miaka mitano tunafanya makosa halafu mwisho tunabaki kulalamika kama hatuna akili nzuri.
 
" Baadhi ya watu wanatumia hotuba ya JPM kutengeneza mkanganyiko ikiwemo kusema ukila papai au fenesi una corona, Wengine wakienda dukani badala ya oil wanaomba jabir lita 2, badala ya papai wanaomba Anne papai, Supu ya mbuzi kuleni havina corona" MAKONDA
 
Wanabodi,

Kwa mujibu wa Rais Magufuli wametuma sample za mimea na wanyama kwa kuzipa majina ya binadamu kwenye maabara kuu ya Taifa Dar es Salaam kwa siri bila wapimaji kufahamu baada ya kupimwa zimetest positive yaani zina corona

Hapa ndipo Magufuli ameprove uwana-science wake...
Huyo si ndio dokta majibu basi si aende huko maabara akatumbue maana kwa vyovyote tu kosa ni lao km mashine mbovu walishindwaje kujua afu pia kisayansi mashine zoOte kabla haijanunuliwa lazima ifanyiwe test sasa imekuaje hz ni propaganda tu
 
Hotuba ya Mh Rais jana imepokelewa kwa namna tofauti katika ngazi totauti haoa nchini. Tayari Mh. Waziri ameanza utekelezaji, na wananchi bado wana maswali.
Kwa upande wa wananchi. Nilichoona kwa ufupi.

1. Pongezi kwa Mh Rais kuweka bayana hali ya maabara ya taifa.
2. Maswali ambayo hayajajibika kutokana na hotuba
Hoja kuu

Tatizo hasa liko wapi? Je, mashine ni mbovu au watumishi ni wabovu?
Ikiwa mashine ni mbovu.

1. Je, tuliinunua hii mashine au tulipewa zawadi? (a) Kama tulipewa zawadi tuliijaribisha kuhakiki ubora wake KABLA ya kuitumia? Je, mtoa zawadi ALITUZUIA kuijaribisha mashine?
Hata kama ni zawadi ya condom umepewa, huwezi kuitumia bila kuitazama expire date, au imetoboka, maana aliyekupa anaweza kuwa amenuia mabaya, lakini ni UZEMBE wako kuamini bila kuichunguza

(b) Ikiwa tulinunua. Nani aliiagiza? Je, manunuzi yalizingatia ulinganishi wa mashine toka nchi nyingine? Ni kweli kabisa CHINA inajulikana kwa kuwa na vifaa visivyo na viwango. Hili si jambo la leo au mwaka huu. Ni miaka yote. Je, kwa nini tulinunua kwao? Kwa nini hatukununua kwenye nchi zenye mashine zenye viwango bora?

(c) Imekuwaje mashine IRUHUSIWE kutumika bila kuhakikiwa ubora? Nani aliyeamuru itumike? Je, kuna beberu alilazimisha tutumie mashine hii? Walioidhinisha matumizi ya mashine isiyohakikiwa wamechukuliwa hatua gani?

(d) Ikiwa tatizo ni mashine, serikali inakwepaje lawama za kuruhusu mashine zitumike bila uhakiki? Miezi miwili sasa, mashine isiyohakikiwa inachapa kazi. Je, watalaumiwa wachina waliouza mashine mbovu au uzembe wa wizara kutoijaribisha mashine kabla?

(e) Je, nani atalipa fidia waathirika? Waliotoka positive kumbe ni negative? Je, vipi kuhusu waliotoka negative kumbe ni positive na wakaingia mtaani kuambukiza wengine? Nani analipa fidia? Je, hakuna namna ya kumdai fidia beberu aliyeuza mashine mbovu? Je, hatuwezi kuwarudishia watubadilishie?

2. Ikiwa tatizo ni wataalam
(a). Je, Wataalam walipewa elimu ya kutosha kabla ya kuanza kazi?
(b) Je, waliotoa elimu kwa hawa wataalam walikuwa wana uelewa wa kutosha?
(c) Je wataalam walioelimishwa walipimwa kujua ufanisi wao?
(d)Je, wataalam hawa wanatumiwa na akina nani? Je, ni kwa maslahi ya akina nani?
(e) Je, ikiwa wanahusika kucheza na majibu, serikali iko tayari kuwashitaki walipe waathirika fidia?

3. Tatizo ni sampuli?
(a) Je, sampuli zilizopelekwa zinaweza kupimwa na mashine husika?
(b) Je tumejidhihirisha kwamba matokeo yatakuwa sahihi kwa sample ambazo sio? Yaani utumie magazijuto kwenye kutafuta kipenyo cha mduara, hivi inafaa?
Hayo ndiyo niliyokusanya huku na huko

Mtazamo wangu.

Ikiwa mashine ni mbovu, hakika kuna uzembe mkubwa sana, na hauhusu mabeberu. Miezi miwili, unatumia kifaa kibovu kisa zawadi/au vinginevyo.

Ni kama ununue simu kariakoo, kisha ukaitumie weeeeee, baada ya miezi miwili unaona ukipiga picha unaona picha kadhaa zina kivuli, nyingine hazina, unalalamika kariakoo kuna matapeli... Kuna aliyekulazimisha ukanunue KKOO? Kwa nini hukuhakiki kabla?

Matapeli wapo na hawaishi. Umakini ndio unatakiwa. Na wakati mwingine kupendapenda kupokea, au kununua vitu vya bei rahisi kuna madhara yake. Cheap is always expensive
 
Unadhani ni kwanini hasa wanafanya uchunguzi?
 
Back
Top Bottom