Ila nyie watu wakatili wa nafsi aiseee...
Kuangalia tuu TBC inahitaji roho ngumu,
Sasa kumwangalia Huyo jamaa TBC inahitaji uwe bandidu na nusu.
Nilienda ugenini, wanaangalia TBC mda wote, Maisha yangu ile jioni yalikua magumu sanaaa, nje kuna mvua, chumbn hakwendeki maana unasubr mwongozo wa wenyeji, kuvaa earphones utaonekana wa ajabu, kuchezea simu mda wote nako hakuleti picha nzuri,
Bahat nzuri mtoto akawa anakuja kuniongelesha kila mambo yakiwa magumu, na mtoto wa mzee ambaye ndie mwenyeji wangu ndie alikua anamtuma dogo aje maana alijua.
Yaani yule Mzee mwenye nyumb anashangilia kila kitu asee, half anakuongelesha u comment...
Nilijitahd kuonesha unafk wa hali ya juu ile siku huku unajichekesha la sivyo naharibu hata kilichonipeleka,
Mpk nikahisi ana ni challenge kuona how deep i can handle pressure.
Baadae Mwanaye akanipa pole maana alijua ninavyoteseka.
Ila asikwambie mtu unafk wa nafsi yako unachoma moyoo aisee, naondoka huku najishangaa, hv kweli n mm wa kumshangilia yule jamaa... Nilitamani nikatubu.
Na huwezi ukanishangaa,
Maana haya sasa wewe umesikiliza, ulichoambulia ndio hicho, umefurahia?