Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Mkuu hujajibu swali langu nikikuletea hizo utashindwa kuzitofautisha hata kwa macho?

Sent using Jamii Forums mobile app


Wewe unaweza kutofautisha majimaji ya papai na maji maji ya Koo la mwanadamu?

Jambo la kujua kabla n vipi Yale majimaji yanachukuliwa, pili yanahifadhiwa kwenye nn mpaka yafike maabara.

Sijui Tanzania tunatumia njia gan Ila naona huko Asia wanakwambia fungua mdomo/Puan wanaingiza kidude kirefu chenye pamba Zen wanaenda kupima.

Sasa wewe sijui ulikuwa unafikiri wanapondaponda papai alafu wanaweka kwenye test tube ndo wakapime au?
 
Mkuu andika habari kwa kumnukuu kama alivyosema.
Ulichofanya hapa ni kupotosha mengi kwa kujaribu kutafsiri alichosema.
Angalia unaweza kujikuta matatizoni ikitokea ukaandika hivi sehemu nyingine ambazo wanaweza kukupata.

Hapa kwa uandishi kama huu hauchomoki ukifikishwa kwenye mahakama yoyote ya kisheria duniani.
Nakushauri mnukuu neno kwa neno na siyo hivi.
Jenga hoja acha kutisha watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atangaze tu hakuna corona Tanzania.Kuvaa barakoa marufuku maana zinaleta hofu tu kwa watu.Sanitizer zimwagwe na maji ya kunawa marufuku.watu waishi maisha yao waliozoea, Shule na vyuo vifuguliwe,maisha yaendelee kama zamani.
 
Sijajua ni nani aliyemshauri Rais kuyatamka haya hadharani.

Matamshi yake yanatoa picha mbaya zaidi na yanazidisha taharuki badala ya ahueni kwa watu wenye kufuatilia muenendo wa janga hili.

Kuwana majibu feki ya kitu kama virusi inatoa tafsiri kuu tatu.
1. Huna vifaa vya uhakika
2. Huna wataalamu wanaoweza tafsiri matokeo sahihi ya vipimo
3. Unao wataalam na unavyo vifaa lakini unapindisha ukweli wa matokeo

Sasa katika yote haya, ina hadi sasa hatuna uhakika kwa kiwango gani COVID-19 imeathiri watu.

Wengi wa Watanzania kwa kadiri ninavyofahamu tabia zetu za kupuuzia, wataanza kujiachia wakiamini janga si kubwa hivyo.

Lakini kwa upande mwingine kuna mambo ya kujiuliza zaidi, je wale Watanzania na wasio Watanzania waliopimwa nchi jirani wakitokea Tanzania, majibu ya vipimo vyao nayo ni ya kutilia shaka?
Hiki ndicho nilichowaza na kuandika mod. Wakafuta Kama watu wasipochukua tahadhari stahiki hali itaenda kuwa mbaya sana huko nchini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila nyie watu wakatili wa nafsi aiseee...
Kuangalia tuu TBC inahitaji roho ngumu,
Sasa kumwangalia Huyo jamaa TBC inahitaji uwe bandidu na nusu.

Nilienda ugenini, wanaangalia TBC mda wote, Maisha yangu ile jioni yalikua magumu sanaaa, nje kuna mvua, chumbn hakwendeki maana unasubr mwongozo wa wenyeji, kuvaa earphones utaonekana wa ajabu, kuchezea simu mda wote nako hakuleti picha nzuri,
Bahat nzuri mtoto akawa anakuja kuniongelesha kila mambo yakiwa magumu, na mtoto wa mzee ambaye ndie mwenyeji wangu ndie alikua anamtuma dogo aje maana alijua.

Yaani yule Mzee mwenye nyumb anashangilia kila kitu asee, half anakuongelesha u comment...

Nilijitahd kuonesha unafk wa hali ya juu ile siku huku unajichekesha la sivyo naharibu hata kilichonipeleka,
Mpk nikahisi ana ni challenge kuona how deep i can handle pressure.
Baadae Mwanaye akanipa pole maana alijua ninavyoteseka.

Ila asikwambie mtu unafk wa nafsi yako unachoma moyoo aisee, naondoka huku najishangaa, hv kweli n mm wa kumshangilia yule jamaa... Nilitamani nikatubu.

Na huwezi ukanishangaa,
Maana haya sasa wewe umesikiliza, ulichoambulia ndio hicho, umefurahia?
Ha ha ha ha ha ha ha h h h h h h

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ameyasema hayo leo wakati wa kumuapisha Waziri wa Sheria na katiba kuwa vyombo vya usalama vilipenyeza sampuli kutoka kwenye mananasi, mafenesi, mbuzi, kondoo, nk kwa siri na kuzifanya ni za binadamu. Jambo la kushangaza matokeo ya baadhi ya sampuli hizo au yalionyesha yana maambukizi ya corona.

"...tunawasiliana na Madagascar na wamehaidi kututumia dawa inayotibu covid 19...." JPM
Mambo ni mengi ngoja niweke clip ya video!

Chanzo ITV....
Uongo mwingine hata watoto wa chekechea watazimia kwa kukucheka. Wa tz tuna bahati mbaya sana
 
Nashangaa anawalaumu waliokuwa wanapima kule maabara ya kitaifa kuwa wanamhujumu, kwa kutoa matokeo positive Ya corona, anadai kuwa walionekana ni positive ni uongo, eti alipeleka sample Ya Mbuzi, papai, na vitunguu eti wale watu Wa maaabara ya taifa walimuhujumu, eti na hizo sample hao wa maaabara Walisema ni positive aiseee anaone kuwa hakuna corona anasema hata ligi ya mpira atairuhusu iendelee aisee huyu mzeee akishindwa Jambo anasingizia mabeberu na kuwa anazungukwa, yani hahahahaha, Halafu nashangaaa anaenda anasema corona kweli ipo halafu anasema vipimo ni vya uongo watu waliokuwa wanapima wachunguzwe yani mmmmh simwelewi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama yeye haogopi corona kwanini hakuna ule mlolongo wa viongozi wakati wa kuapisha waziri mpya kama ilivyo kawaida yake??

Kwa kifupi ni kwamba alikuwa akijaribu kujitetea na kuzijibu baadhi ya hoja za Mh Mbowe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basi kama anaongea ukweli afungue shule na ligi kuu ,/ Sio anakunywa supu ya Mavv alafu anabwatuka.
 
Jenga hoja acha kutisha watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe umekurupuka, simtishi namuelimisha.
Hujona nimemuambia akiandika hivyo kwenye mitandao ambayo wanaweza kumpata kirahisi (mfano Facebook, n.k.) anaweza kujikuta matatizoni kwa vile humu najuwa hawatamkamata, kwa hivyo simtishi namtahadharisha.

Acha mihemko, mwenye kushauriwa ana uhuru wa kupokea ushauri wangu au kuupuzia.
 
Wewe unaweza kutofautisha majimaji ya papai na maji maji ya Koo la mwanadamu?

Jambo la kujua kabla n vipi Yale majimaji yanachukuliwa, pili yanahifadhiwa kwenye nn mpaka yafike maabara.

Sijui Tanzania tunatumia njia gan Ila naona huko Asia wanakwambia fungua mdomo/Puan wanaingiza kidude kirefu chenye pamba Zen wanaenda kupima.

Sasa wewe sijui ulikuwa unafikiri wanapondaponda papai alafu wanaweka kwenye test tube ndo wakapime au?
What if hayo mapapai yalikuwa contaminated na mtu aliyechukua sample ?Sidhani kama alifuata sheria zote za kuchukua vipimo kama inavyotakiwa. Alivaa gloves n.k. Ikute alichukua sample huku mwenyewe akiwa positive na akaliambukiza papai.
 
Wakuu, someni hiyo mada hapo juu kisha nenda kamsikilize rais wewe mwenyewe kwa masikio yako, tafakari aliyo yasema, alafu njoo hapa uje kusoma comments za watu hapa hakika utagundua kitu cha ajabu sana hapa.

Kama sio mvivu soma comments za uzi mzima kuna kitu utaikiona cha muhimu mno.
Elimu ya TZ inahitaji maboresho makubwa.

"We have schools and we're mis-educated in those schools" Prof Lumumba uko sahihi hukukosea leo nimeamini.
 
Back
Top Bottom