Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Umeuliza maswali mazuri sana ila mpaka leo hujui kuwa usahihi ni MAABARA NA SIO MAHABARA.

Kwa nini una maswali mazuri alafu unakuwa hujui usahihi wa kuandika baadhi ya maneno mkuu ?

Umerudia zaidi ya mara moja kosa lile lile kuonesha kuwa unajua usahihi ndio huo,ilikuwaje, hili neno hukuwahi kuliona au shida nini mkuu ?

Baada ya kuandika "uko wapi" unaandika "huko wapi " kweli wewe unataka africa ibadilike wakati wewe haujabadili hata namna ya uandishi ?
Nashukuru mkuu nimebadilisha.
 
Ni nini logic ya raisi leo ni kwamba corona imetapakaa sana mitaani hadi katika mapapai na mafenesi?

Au

Corona hakuna nchini kwetu Tanzania isipokuwa hivi vipimo vya kichina ndio vinatudanganya?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe itakuwa una damu ya kizungu ndio maana humuelewi

Raisi aliposema haya yote wazungu pia hawakuelewa

No lockdown

Corona kagonjwa kadogo

Tufanye maombi siku 3 kujikinga na corona

Tuwe tunajifusha ili kujikinga na corona

Na sasa ameitangazia dunia kuwa maabara yake inatoa majibu faki ya corona

Ila sisi wenye damu ya kiswahili tunamuelewa sana bila ya shida yoyote na ndio maana kila alipoongea katika hayo watu waliandika nyuzi nyingi kumpongeza raisi

Usihofu taratibu na wewe utamuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuuu, hiii kitu naona inazungumzia na nchi mbalimbali duniani na inazungumziwa kwa namna mbaya sana, wanaozungumza wanaonesha kuwa nchini Tanzania kuna vituko vinaendelea katika namna tunavyokabiliana na Covid -19, watu wanaijadili huko nchi za nje kwa dharau kubwa na kutuona kama sisi ni majinga sana.

Huenda Rais alilisema akiwa na maana nzuri lakini akakosa kuona madhara ya upande wa pili. Kauli ya Rais huwa ni kubwa sana na huwa kila mtu anaichukua na kutembea nayo, Rais anapaswa kushauriwa juuu ya maneno ya kuongea, ndio maaana kuna wahariri wa hotuba za marais. Washauri wasimuogope wamshauri na kumwelekeza wasimuache anaongea kila kitu, rais wetu anazidi kudhalilika ktk nchi za kimataifa.

Nina Uhakika hata hao marafiki zake akina Museveni, Kenyatta na wengne wanamsema vibaya ila yeye hawezi jua ajitahid kusikiliza washauri wake, anazid kudhalilika.

Unaweza ukaongea Jambo ukiwa na maaana nzuri lakini kwa upande mwingne Jambo hilo lina maaana mbaya kwa asilimia kubwa, maana kumbuka kuwa watu walioko huko Japan au Uholanz au hata hapo Kenya hawawezi kumpata mtu wa kufafanua ulichokisema ulikuwa unamaaanisha nini.

Pia rais aache kuongea kwa hasira awe mtulivu; aongeee kwa ustaarabu, anaonesha ana hasira kubwa hadi anajikuta anakohoa kohoa ktk kuongea; zile ni hasira zinazopelekea hadi anakohoa sio kuwa ana umwa, hapana. Zile ni hasira ambazo kila mtu anajiuliza kwanini ana hasira?

Huuu ugonjwa haujaletwa na mtu, lakini yeye anaonesha kama COVID -19 kaletewa na wabaya wake. Rais aache hasira aongee kama Rais wa nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma vyanzo mbali mbali vya dunia, hili suala limetembea sana. Na waandishi wa habari wao huchukua key points na kuandika, na waasomaji hu base hapo hapo, yaani ni aibu sana kwa nchi. Tz saiv ni maarufu sana
 
Boss wewe umezungumzia wahariri wa Hotuba lakini yeye haya maneno huwa hayatoi kwenye hotuba🤣 huwa ni papo kwa papo, kuna member walidai huwa anaandaliwa hotuba afu anakataa kuzisoma.
 
Hii hotuba ya raisi ya jana ni kwaajili ya Watanzania na sio Wakenya wala hao uliowataja!!!! Watz tumemuelewa maana lugha aliyotumia ni ya Taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma vyanzo mbali mbali vya dunia, hili suala limetembea sana. Na waandishi wa habari wao huchukua key points na kuandika, na waasomaji hu base hapo hapo, yaani ni aibu sana kwa nchi. Tz saiv ni maarufu sana
ngoja niende google nione wazungu wamejiskiaje kusikia maiti zivikwe PEP
 
Hii hotuba ya raisi ya jana ni kwaajili ya watanzania na sio wakenya wala hao uliowataja!!!! Watz tumemuelewa maana lugha aliyotumia niya Taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili gonjwa ni la wote, ndiyo maana lilianzia china ila leo liko kuwa mahali... Kusema kwamba sisi tumejitenga na dunia siyo kweli ikitokea wengine measures zimewavusha sisi bado hatujavuka ina maana tutakuwa tunawahatarisha na wao.
 
Hivi tunaonekana majinga kivipi?
Anayetuona sisi wajinga huwenda
ndiyo pumbafu sana

Rais kaongea kwa lugha rahisi tu haihitaji wewe uwe na elimu yoyote ili
uweze kumuelewa rais alichoongea
Uwe tu na uwezo wa kusikia utamuele
Hao waandishi walioandika hizo habari kuna shida mahali ama ni propaganda ama ni lugha tatizo

Kauli ya rais ni simpo tu
Kwamba :Vipimo vya corona katika maabara kuu Tanzania ni feki

Sasa ujinga ni nini hapo
Vipimo vimenunuliwa kutoka nchi gani?
Na hizo habari mbaya mmezisikia kutoka nchi gani?
Propaganda:huwenda watengeneza vipimo wamebadili story na nyie wajinga wachache mmeshatekwa akili na kuwaona wao ndiyo wako sahihi
Kwani pia mmewahi kusikia India ikikataa vipimo vya corona kutoka China kuwa havina ufanisi? Ni feki kwa kifupi
Majuzi tu India walikataa vipimo vya China
Nchi zetu haziko makini kinachokuja huwa tunaona ni bora wakati wote bila kuchunguza Leo watu sameshtuka kuchunguza na imebainika
Manakuja hapa kutetea shudu
Sasa nendeni mkapimwe tuwaweke Quarantine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mtu nimeongea naye akaniambia point ya msingi sana...

Maabara huwa kuna msemo wa "gabbage in, gabbage out".

Kama sample inapaswa kuwa mkojo, wewe ukaweka damu; ujue tu majibu pia yatakuwa ya ajabu.

Ndio maana kabla ya tests huwa wanafanya quality control.

Sasa sio mara zote siasa itakuambia facts hizi.
 
Ilikuwaje hii mkuu? Hahahaha

Sent using iphone pro max
Hahahaah!! Ilikua wakati mzee Kigoda anaumwa yupo India watu wakawa wanamuulizia sana hawamuoni na hawajui anaendeleaje ndo mzee baba akasema ameongea akiwa ICU na kamwambia anaendelea viruzi.

Umesahau na alivomtuma katibu mkuu mstaafu Kinana kwenda kutibiwa India?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yalipimwa mapapai mangapi..?? Mbuzi ngapi..?? Mafenesi mangapi..??

Yote yalileta majibu sawa.? JPM nae Visa
 
Mkuu wa mkoa wa Dsm mh Makonda amewataka wananchi kutoitafsiri vibaya hotuba ya Rais Magufuli na kuacha kula mapapai.

Makonda amesema Rais Magufuli kama mkemia kitaaluma alihisi kuna tatizo kwenye matokeo yanayotangazwa hivyo akaamua kufanya utafiti wa ubora wa kipimo.
Sampuli zilizotumika ni kwa ajili ya kupima ubora wa kipimo na siyo virusi.

Makonda amesisitiza kuwa matokeo yaliyotoka yameonyesha kuna walakini kwenye kipimo na hiyo haina maana kuwa papai lina Corona hata kama lilibatizwa na kuitwa Anna.
Makonda amewataka wananchi wsendelee kula mapapai na amesikitishwa na picha zilizozagaa mitandaoni zikionyesha watu wakiikata miti ya papai kwa sababu ya hofu ya Corona.

Source Ayo tv!
 
Mkuu wa mkoa wa Dsm mh Makonda amewataka wananchi kutoitafsiri vibaya hotuba ya Rais Magufuli na kuacha kula mapapai.

Makonda amesema Rais Magufuli kama mkemia kitaaluma alihisi kuna tatizo kwenye matokeo yanayotangazwa hivyo akaamua kufanya utafiti wa ubora wa kipimo.
Sampuli zilizotumika ni kwa ajili ya kupima ubora wa kipimo na siyo virusi...
What if aliyepeleka sample ya papai ana Corona? Huyo mbona hawamzungumzii?
 
Utawala uliofitinika
IMG-20200503-WA0071.jpg
IMG-20200503-WA0126.jpg
IMG-20200503-WA0093.jpg
IMG-20200504-WA0016.jpg
IMG-20200504-WA0006.jpg
IMG-20200503-WA0072.jpg
IMG-20200503-WA0131.jpg
IMG-20200503-WA0132.jpg
 
Back
Top Bottom