Rais Magufuli: Mshahara wangu kwa Mwezi ni Sh. Milioni 9.5. Nitatoa salary slip...

Rais Magufuli: Mshahara wangu kwa Mwezi ni Sh. Milioni 9.5. Nitatoa salary slip...

Rais Magufuli analipwa Tshs. Milioni 43 kwa mwezi, na mshahara huu ni nyongeza ya Tshs. Milioni 7 ambapo mwaka 2014 mshahara wa rais ulikuwa Tshs. Milioni 36! Marais wastaafu yaani Mwinyi, Mkapa na Kikwete wao wanakula Tshs. Milioni 34 kila mmoja kwa mwezi iwe walale, watembee, wakae kuchwe jua, mvua. Wao ikifika mwisho wa mwezi account zinasoma hadi siku wanaingia ndani ya futi 6.

Kilichotokea jana ni kituo cha clouds kwa kujua fika kuwa ni siku ya wajinga duniani basi wakavamia kuifanya siku hiyo kufana zaidi kwa Tanzania.

Kwa kweli kwa sasa watanzania wamebadilika na au kubadiloshwa sana! Hawahoji tena mambo muhimu kama haya bali wanayapokea tu juu juu. Kila kitakachosemwa kumsifia Magufuli wao huitika "HAPA KAZI TU" Sasa wengi wamekuwa walemavu wa kufikiri.

MCC wametoa sababu za msingi za kuinyima Tanzania Tshs. Trilioni 1. 05 za miradi ya maendeleo Magufuli akatoa matamshi ambayo kimsingi ni kujipa faraja huku wakijua fika kuwa tumekosea wao wakaitika "HAPA KAZI TU"

Kama mshahara wa rais umepunguzwa hayo yangejulikana na vyombo husika tena kwa mujibu wa sheria na siyo kusemwa kwenye kipindi cha soga kwenye kituo cha TV kisha wakaita "official statement" hivi hatuoni kuwa tunajidharau wenyewe?
Magazeti yametoa Rais analipwa mil 9.5, sasa tumuamin nan kati yako na vyanzo vya ikulu kupitia magazeti

Hii vita ya mshahara mshashindwa tafuteni nyingine , na hapo atarudi bungeni sijui itakuaje huko naomba tumuunge mkono mh Rais

Naona anataka watu wajali taaluma na siasa soon siasa itakuwa hailipi
 
Kuna mitanzania mipumbafu sana, yaani yanaamini kabisa Rais anapokea 9.5mil. kwa mwezi, na ndio mshahara aliyoukuta!!! Hii inamaana kwamba mzee wa Msoga nae alikuwa anakunja kiasi hicho hicho. Huu usanii sijui ni kwa faida ya nani.

Naipenda sana Tanzania yangu, ila wananchi wake ni wa hovyo sana.
 
Exactly.. ndio matokeo ya makosa ya Uchaguzi Mkuu 2015. Utawalaumu wakitumia wingi wao; si ndiyo demokrasia ile ile.

..YES.

..mimi nawa-encourage watumie wingi wao kuleta positive changes nchini petu.

..katika mukthadha huo, nawachagiza wakabadili katiba ili wa-Tz wasiendelee kubeba mzigo/msalaba wa kuwatunza viongozi wakuu.

..according to william lukuvi, gharama za kumtunza Raisi ni sawa na bajeti ya mikoa mitano. je, huo siyo unyonyaji kweli?

..hivi kuna ulazima wa kuendelea kuwatunza viongozi wakuu kwa viwango hivi vya sasa hivi hata miaka 20++ tangu wastaafu?
 
Kuna mitanzania mipumbafu sana, yaani yanaamini kabisa Rais anapokea 9.5mil. kwa mwezi, na ndio mshahara aliyoukuta!!! Hii inamaana kwamba mzee wa Msoga nae alikuwa anakunja kiasi hicho hicho. Huu usanii sijui ni kwa faida ya nani.

Naipenda sana Tanzania yangu, ila wananchi wake ni wa hovyo sana.
Hapa ndugu umetumia kauli yenye ukakasi issue sio kuwa tunaamini issue ni kuwa taarifa ni za uhakika na je, Ikulu iko tayari kuweka wazi kiwango anacholipwa Rais mimi mwenyewe nataka kujua lakini nahitaji taarifa sahihi kabla ya hiyo jana nilikuwa najua mzee wa msoga alikuwa anakunja milioni 36
 
Ataje na masurufu mengine, usikute allowance mil 30 mshara ndio M 9.5 hii Nchi hii, Ngoja tuone hii tamthiliya itaishia wapi.
Mzee inaonesha upeo wako haujatulia. Nini maana ya neno masurufu mil 30. Kwa taarifa yako masurufu ni pesa ya jambo fulani maalumu na haiwezi kuwa na kiwango km ulivyosema bila kutaja ya kufanyia nini. Na kumbuka masurufu lengo lange ni kuwezesha mfanyakazi kutenda majukumu yake kwa ufasaha. Wakati mshahara ni malipo ya utumishi kwa ujumla. Hivyo wanaosema sijui ulinzi, magari, chakula hayo ni ya kumfanya afanye kazi tuliyomtuma kwa ufasaha. yaani asiwaze atakula nini yeye akomae na majipu na kujenga nchi tu.
 
Hivi kweli kunamtz anaona 9.5m ni kubwa kwa kazi ambayo JPM anaifanya unadhani hii nchi ni Consultant gani na tungemlipa kiasi gani atufanyie hata robo tu ya mambo JPM anatufanyia? We should learn to appreciate and be thankful. Binafsi nimeona haitoshi kama kuna mtu analipwa 40m kwenye mashirika ya umma mengi yasiyo namanufaa kwa umma yaani yanajiendesha kwa hasara.
 
..YES.

..mimi nawa-encourage watumie wingi wao kuleta positive changes nchini petu.

..katika mukthadha huo, nawachagiza wakabadili katiba ili wa-Tz wasiendelee kubeba mzigo/msalaba wa kuwatunza viongozi wakuu.

..according to william lukuvi, gharama za kumtunza Raisi ni sawa na bajeti ya mikoa mitano. je, huo siyo unyonyaji kweli?

..hivi kuna ulazima wa kuendelea kuwatunza viongozi wakuu kwa viwango hivi vya sasa hivi hata miaka 20++ tangu wastaafu?

Tunaposema 'kuwatunza viongozi wetu" tunamaanisha nini?. What is the scope ya kuwatunza hao viongozi?. Is there data so that we can do a comparative analysis ya gharama za kuwatunza viongozi. This will shed light and enable suggestions on ways to balance actual need and associated cost.
 
Kampeni tuliyoianza tarehe 1 mwezi Julai 2007 mwishowe itafanikiwa tu.
 
Kampeni tuliyoianza tarehe 1 mwezi Julai 2007 mwishowe itafanikiwa tu.

NN, I thought I promised you something on this thing.. kampeni itakuwa na matokeo mkuu.. na itakuwa na matokeo ya kushtua kweli kweli. Hongera kwa kutolegeza kamba, unaitwa "msimamo"
 
NN, I thought I promised you something on this thing.. kampeni itakuwa na matokeo mkuu.. na itakuwa na matokeo ya kushtua kweli kweli. Hongera kwa kutolegeza kamba, unaitwa "msimamo"

Yes you did my man! You told me that.

Kwa kweli nimefurahi sana na nitafurahi zaidi pale atakapotimiza ile ahadi yake akitoka mapumzikoni.

Ni jambo zuri sana.
 
Hiyo ni nzuri ya kusoma

http://s07.jamiiforums.com/mini/uyE8/bg_000000/txt_000000/border_000000/flags_0/

http://s09.jamiiforums.com/mini/h96A/bg_000000/txt_000000/border_000000/flags_0/
 
Ataje na masurufu mengine, usikute allowance mil 30 mshara ndio M 9.5 hii Nchi hii, Ngoja tuone hii tamthiliya itaishia wapi.
HAJAFANYA KOSA KUTANAZA MSHAHARA WAKE KWA MWEZI.JE WAKATI WA UKWELI NA UHAKIKA MLIYAFAHAMU YOTE HAYO ! NI VIGUMU KUWARIZISHA WATU OTE.TENDA WEMA WENDE ZAKO USINGOJE SHUKRANI KUMBE NI KWELI !
 
Tunaposema 'kuwatunza viongozi wetu" tunamaanisha nini. What is the scope ya kuwatunza hao viongozi? Is there data so that we can do a comparative analysis ya gharama za kuwatunza viongozi. This is shed light and enable suggestions on ways to balance actual need and associated cost.

..kuwatunza viongozi namaanisha mshahara,posho, marupurupu, pamoja na huduma nyingine ikiwemo matibabu ndani na nje ya nchi.

..some of the data zinapatikana wakati wa bunge la budget. lakini kwa ujumla kuna usiri mkubwa katika suala hili.
 
Asante ndugu. Hivyo basi inakuwa ngumu kujadidli suala la kuwatunza viongozi kwa vile hatuna data za kutosha. Ninaamini awamu ya tano imejikita kwenye transparency. Tumeona Rais kataja mshahara wake, kinachofuatia rais atataja marupurupu yake, kiasi cha fedha kinachotumika 'kuitunza ikulu kwa ujumla', may be with breakdown of each expense category.
 
Eti analipwa 9 milioni huyuhuyu aa huyu jamaa ameamua kutudanganya tu.
Rais wa nchi alipwe milioni 9 tu haiwezekani
Vipi mkurugenzi wa TANESCO analipwa shilingi ngapi
 
Back
Top Bottom