Rais Magufuli: Mshahara wangu kwa Mwezi ni Sh. Milioni 9.5. Nitatoa salary slip...

Rais Magufuli: Mshahara wangu kwa Mwezi ni Sh. Milioni 9.5. Nitatoa salary slip...

Wadau kipindi mkulu yupo mapumzikoni Chato mwaka jana aliahidi akirudi Dar angeonyesha salary slip yake ili watanzania tujue analipwa shilingi ngapi.

Sasa nadhani sababu ya majukumu mengi amesahau, nlikua nawaomba wasaidizi wake wamkumbushe mkulu ili watanzania tujue mkuu wetu analipwa shilingi ngapi. Cha kushangaza ni kwamba tunaujua mshahara wa Rais wa marekani lakini wa Rais wetu hatuujui.
Watu wengine wachimvi sana. Hivi ukiujua mshahara was Rais utapata faida gani. Frankly mambo mngine unaonekana mwenye busara ukinyamaza.
 
Watu wengine wachimvi sana. Hivi ukiujua mshahara was Rais utapata faida gani . Frankly mambo mngine unaonekana mwenye busara ukinyamaza.
Alivyosema anatuonyesha ni ili tupate faida gani? kinachozungumziwa hapa na ahadi za uongo
 
Hata hivyo mshahara siyo issue kwake!Si ninasikia katiba inamruhusu hata kuchukua pesa za ujenzi was reli,barabara hata hospital akiamua!Lamuhimu tumuombee kwa Mungu!Na muhimu zaidi tumuombee Bw. Edward afya yake iendelee kuimarika!2020 pachimbike zaidi!
 
Watu wengine wachimvi sana. Hivi ukiujua mshahara was Rais utapata faida gani . Frankly mambo mngine unaonekana mwenye busara ukinyamaza.
Yeye kama alikua na busara kwa nini alisema atonyesha salary slip yake. Muulize kwanza hilo swali bosi wako kabla hujaja humu kutupigia makelele yako
 
Yeye kama alikua na busara kwa nini alisema atonyesha salary slip yake. Muulize kwanza hilo swali bosi wako kabla hujaja humu kutupigia makelele yako
weka kwanza salary slip yako wewe, ukijua mshahara wa mtu utakusaidiaje wewe kimaisha. fanya kazi
 
Moja ya uongo wa Magufuli. Hadi leo hii zaidi ya mwaka sasa kashindwa kuthibitisha kauli yake.
 
Rais wa Tanzania John Magufuli amefichua kuwa anapokea mshahara wa kila mwezi wa shilingi milioni 9 za Tanzania.

Hii ni robo ya mshahara ambao mtangulizi wake Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa akipokea iwapo takwimu zilizonakiliwa na Afrika Review miaka mitatu iliopita ni za kweli.

Rais Magufuli alifichua hayo katika taarifa ya moja kwa moja katika runinga mapema Jumanne katika hotuba kwa muungano wa serikali za mitaani wakati ambapo alikuwa akikisisitiza kuhusu umuhimu kwa kukabiliana na rushwa.

''Baadhi ya wanachama wa bodi za mashirika ya uma walikuwa wakisafiri hadi Dubai kufanya mikutano yao huko ili wajilipe marupuru mengi.Hivi sasa hawataki kile serikali yangu inachofanya''.

bbc
 
Back
Top Bottom