Rais Magufuli: Mshahara wangu kwa Mwezi ni Sh. Milioni 9.5. Nitatoa salary slip...

Rais Magufuli: Mshahara wangu kwa Mwezi ni Sh. Milioni 9.5. Nitatoa salary slip...

Nga'choka mie.....[emoji134] [emoji134] [emoji134]
 
Kalipe sh 500000/= maadili ya viongozi utaona. Ukae ofisi ukisoma majalada ya JPM. Utakuta sh 9000000/=
 
Kwa hiyo hamtaki kuamini?
Hata tukiamini bado ni pesa kubwa mnoo maana mpaka chupi yake sasa hivi tunaigharamia watanzania, kila Kitu anapata bure na ndio maana ana jeuri ya kuwajeurikia watumishi wenye mishahara ya laki 2 mbili hadi 5
 
Huyu ng.ombe anapenda kiki za kijinga sana
 
Hili kuangalia file la kiongozi unatakiwa kulipia pesa upewe hili file. Ofisi za maadili. Na uape na pesa utoe.
 
Ngazi za mishahara ya watumishi wa serikali (civil servants), Rais akiwa mmoja wao na ndiye mwenye ngazi ya juu kuliko watumishi wote wa serikali inaanzia TGS A hadi TGS Z (TGS = Tanzania Government Salary). Rais ndiye mwenye TGS Z peke yake, wengine wa serikali hawawezi kuvuka hapo, wanajikanyaga chini ya hapo. Ili watumishi wengine waweze kupanda mishahara lazima TGS Z ipandishwe kwani ndiyo ina set ceiling ya mishahara hii.

Nyerere hadi anaondoka madarakani TGS Z yake ilikuwa Sh 4,000 kwa mwezi. Hakuwa anapenda ipande kwani itasababisha na ya walio chini yake kupanda na hivyo wage bill kukua na kusababisha ongezeko la inflation na kupunguza thamani ya shillingi. Huko Kenya kumekuwa na mtikisiko wa utumishi serikalini kutokana na Rais na wasaidizi wake wa kisiasa kujitengenezea mfumo wao wa mishahara, mishahara ambayo ni mikubwa sana ukilinganisha na civil servant wengine. Kwa mfano mshahara wa rais ni KSh 22 milion kwa mwezi wakati mshahara wa very senior civil servant kama Daktari bingwa ni KSh 200,000/.
 
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametaja mshahara wake kuwa ni Tsh mil 9.5, huku akiahidi atatoa Salary slip zake punde akitoka mapumzikoni Chato.

Hiyo imetokea wakati wa kipindi cha magazeti leo tarehe 01/04/2016 ambapo watangazaji walisoma habari iliyoandikwa na gazeti la nipashe kuwa Zitto na Lissu waomba ataje Mshahara wake na ukatwe kodi.

Wakiwa katika mjadala huo, walipokea taarifa kuwa Rais kawasikia na katuma taarifa ofisi za Clouds kujuza mshahara wake kuwa ni mil 9.5 na atatoa stakabadhi zake akirudi Dar.

Chanzo: Clouds 360 Asubuhi hii

==========
Kutoka Gazeti la Mwananchi:
Heheeeeeeee mnamlipa MIRIONI TISA TU harafu mnategemea yeye ataishije???????
 
Back
Top Bottom