Rais Magufuli mtumbue Bosi wa TTCL anaihujumu kampuni

Kuna siku niliona wametoa gawio kwa serikali kiasi kama bilioni ivi,siku ya pili yake nikaona gari lao lilipaki sehemu sasa wakati linataka kuondoka nikaona watu wanalisukuma ili liwake,kumuuliza dereva tatizo ni nini dereva akajibu betri yake mbovu,nikacheka kweli na kusema jana tu mmetoa bilioni of money leo mnasukuma gari,lakini jamani ndio changamoto izo inabidi wazikabili
 
Mm nnatumia Mtandao wao wa Internet na line ya chuo. Ila network yao haiko vizrui baadhi ya sehemu hapa Dar. Mfano, nikiwa Mjini mida ya kazi, nafaidi vzuri. Nikirudi home bunju au nikiwa Chanika huko kwenye mishemishe zangu. Siambulii chochote.

Sasa kama hapa Dar tu inawashinda kuweka full covarage, vipi huko mikoani?

Ttcl mnatakiwa mjidhatiti. Na muweze kutoa huduma iliyo na viwango hata kama haitafanana na wainzani wenu, ila basi sio kila mtu aweze kuona hizo dosari ndogo ndogo.

Sent using [Iphone XS Max]
 
Hivi Dr. Kamugisha Kazaura walimtoa pale kwa kisa gani?

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Hapo ktk kuimarisha mtandao umenena, mie nikitoka tu nje ya mji ni majanga dunia nzima
 
Hujui accounts and financing ndio.maana unaona ni ujinga
Kupata faida na kutoa gawio,hakukuzuii kuomba mkopo au capital injection toka kwa shareholder kwa ajili ya investment ya miundombino
Nenda ukasome hata book keeping KIMAwewe acha kukariri mambo ya MATAGA. Utagawaje gawio wakati Net Profit ni Negative?. Kwanza angalia hata asets zenu zilivyo chakavu, magari yenu tu ya kwenye field ni TETANUS tupu eti mnaigawia Serikali fedha||
 
Tunashukuru kwa ushauri wako.
 
Yaani watoa huduma baada ya kutufuata sisi wao ndio wanataka sisi tuwafuate
taasisi nyingi za serikali ndivyo zilivyo yaani wao wanaona wenye shida ni raia na sio wao, wao ujichukulia km special cream flani hivi kwenye jamii..
 
yaani hapo ndio hamn'goi kabisaaaaaa
 
Kila siku taasisi za serikali zinatumbuliwa lakini bado kuna taasisi hawajifunzi kwa wenzao wanaotumbuliwa mfano wa hizo taasisi na TTCL,bado wanafanya kazi kwa mazoea.
TTCL hata kupata vocha dukani ni inshu kubwa.kusajili laini tu unasumbuka kupata wakala labda mpaka uende dukani kwao.mawakala wa kwenye meza na miamvuli hawana kifaa chao cha kusajilia.
 
Naunga mkono hoja. Haiwezekani hapahapa dsm mtandao usikamate. Naishi tabata kimanga. Mtandao ni wa shida sana. Internet haikamati kabisa. Kama bosi ameshindwa kazi ni vema akae pembeni, awapishe watakaoweza kuleta ufanisi kwa kampuni hiyo ya umma
 
Bonge moja la ushauri.
 
Mimi ni mteja wa TTCL kwa miaka mingi, ninatumia simu ya mezani, natumia MI-FI na mobile
kuangalia salio kwa mobile iko standard kwa wote piga *102# kuona salio lako au kwa upande wa vifurushi piga *148*30# select number 9
Sidhani kama wewe ni mteja, bali ni sehemu ya menejementi ya TTCL maana unatetea sana humu
 
Tangu magufuli aje na utaratibu wa 1×3 yaani
Teua Mwigulu Mchemba
Tengua Mwiguli Mchemba
Teua Mwigulu Mchemba

Hakujawahi kuongezeka ufanisi wowote ule kwenye utendaji wa serikali yake.
 
Serikali ni msimamizi wa sheria za sector nzima ya mawasiliano Tanzania

Hivyo anasimamia rules of the game,kila mfanyabishara hii awe protected na kuwajibishwa kwa usawa

Cha ajabu serikali hiyo hiyo tuliyoipa madakara makubwa namna hii kusimamia rules of the game eti yeye nae anafanya biashara hiyo hiyo...

Unategemea haki among all the wafanyabiashara kwenye hii sekta?

Kindamba ni nonsense,tangu lini serikali ikajua kufanyaa biashara ya aina yoyote?

Kwanza biashara yeyote inayohusiana na serikali tu,wananchi hawapendi huduma zake to begin with!

Serikali iache kufanya biashara isimamie sekta hizi kuhakikisha rules of the game are equally adhered by all participants,otherwise tunavuruga uchumi mzima

Serikali ni dude la hovyo mno..

Na majitu yaliyomo humo tumeyapa nguvu ya kufanya maamuzi ya hovyo bila wao kupata consequences zozote wakati sisi ndio wabeba consequences 100%!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…