Uchaguzi 2020 Rais Magufuli muombe Rais Mstaafu Kikwete akusaidie kupiga kampeni

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli muombe Rais Mstaafu Kikwete akusaidie kupiga kampeni

Kuna watu sita (6) ambao Mheshimiwa anapaswa kuwaomba kwa njia ya kipekee wamsaidie katika kampeni zake za uchaguzi mwaka huu;
1. Mzee Kikwete
2. Kamarade Kinana
3. Mzee Warioba
4. Mzee Butiku
5. Mzee Msekwa
6. Mzee Makamba

Hii ndiyo think tank ya CCM, kwa kuzidi kujimwambafai kwake, na kuwaweka kando wazee hawa, kura zake zinakwenda kuwagawanyika na za Membe.
Tatizo mnapenda kukariri
Magu hata bila kampeni ameshinda amefanya makubwaaaa
Sie wananchi tunamkubali
Kama Ana makosa yake NI madogo madogo Kama binadamu
 
Kwanza naona Km Magufuli anajichosha izo pesa za kampeni bora angewaongezea mishahara watumishi yeye akaendelea kufanya kazi za nchi kwa aliyoyafanya miaka5 haitaji kusumbuka sioni mpinzani wakupambana nae.Wapinzani badala ya kutwambia watatufanyia nn wao wanabaki kutueleza upigwaji wao wa lisasi watanzania ndotunakita sisi icho??Acheni Magufuli akaongoze nchi na Wapinzani wangekua wazalendo ndowangekua wakwanza kupinginga uchaguzi wa Rais sana tungefanya wa wabunge na madiwani.
 
Nimemsikia Mwenyekiti akiwa Singida na akiwa Shinyanga anayo yaongea hayana tofauti na hotuba yake ya kuvunja bunge......"vijiji elfu mbili vilivyobaki havia nishinda"....wanaomshauri inabidi wamweleze ukweli......kampeni ni zaidi yakusema mafanikio
Ulitaka aseme Nini Kama sio mafanikio
Wewe kweli unachekesha
Kwa hiyo kampeni nini ?yaan watu mnapenda kujifanya mnajua kukosoa!!!wakati hamjawahi kufanya kampeni hata ya uongozi was chuo
 
Amuache mjuaji apambane na hali yake kibebeo mkapa hayupo tena
Amelaaniwa mtu Yule amtegemeaye mwanadamu
Magu songa mbele Mungu Yuko na wewe
Hao wanaowategemea wastaafu ndio washinde achana na
Wewe NI jeshi
 
Kifo cha Rais mstaafu Benjamin W Mkapa ni Pengo kubwa sana katika uchaguzi wa mwaka huu.

Kwa mwenendo wa uchaguzi wa mwaka huu, hali sio ya kuchukulia poa kama CCM ilivyokuwa ikifikiria. Ukimya wa watu miaka 5 usiwadanganye wana CCM kuwa uchaguzi huu ni mwepesi. Watu wamebeba mengi kwenye Nafsi zao. Waatu wanataka kutumua sanduku la kura kuonesha hisia zao.

Rais Magufuli unatakiwa utambue kuwa,
huu uchaguzi ni mgumu sana haijawai tokea hapa Tanzania na ukiudharau utakushangaza.

Rais Mstaafu J. Kikwete ni mmoja wa viongozi wenye upawa mkubwa wa kuvuta hisia za watu.

Rais Magufuli, Jisushe na Muombe Mh Kikwete aje akusaidia kufanya kampeni. Hutaweza wewe peke yako. Kumbuka bado siku 50+. Uliyekuwa ukimtegemea sana ndiyo hivyo Mungu kampenda zaidi. Sasa mtumie aliyebaki anaweza kuwa msaada mkubwa kwako zaidi ya hata uliyekuwa ukimtegemea.

Aliyekudanganya kuwa wasanii ndiyo watakupa kura, mchunguze kwa umakini sana. Anawezakuwa anafaidika kupitia posho za ao wasanii. Ila ukweli ukiangalia mikutano yako imejaa watoto na wanawake tu ambao wanavutiwa na wasanii tu.
1599123861565.png
 
JPM 2015 alishinda uchaguzi na Wala siyo kwa msaada wa hao uliowata, hao wanajifagilia kwamba walimsaidia ni njia za kutaka kupewa ulaji nauhakika, Kinana hakuwepo nchi mbona CCM imeendelea chini ya Bashir na hao wengine kina Nape wamebaki kujipitisha bila kupingwa Kama kweli walimsaidia Magufuli mbona wameshindwa kujishindisha wao kwenye sanduku la kura?
 
Halaf leo nimemcheki pale Nzega kachoka mnoooo, na hii ni siku ya 3 ya kampeni zake....si ajabu huyu Jamaa kutokupenda Uchaguzi, anateseka jamani!
alitoboa lowassa kipindi kile sembuse magufuli mwenye kucheza singeli[emoji38][emoji38][emoji38].

mnatafuta tone la maji kupooza makoo yenu lakini waaapi.
magu rais 05 tena.
 
Anawapelekea Wanyamwezi waliopinda stori za Ndege na Daraja la Mfugale wanamcheekii akiondoka wanarudi kwenye vijiwe vyao vya kahawa huku wakimsubiri Lissu walugaluga hawataniii wanamnyoa Mhutu alfajiri na mapema
waluga luga wanashangaa magari.
 
Kifo cha Rais mstaafu Benjamin W Mkapa ni Pengo kubwa sana katika uchaguzi wa mwaka huu.

Kwa mwenendo wa uchaguzi wa mwaka huu, hali sio ya kuchukulia poa kama CCM ilivyokuwa ikifikiria. Ukimya wa watu miaka 5 usiwadanganye wana CCM kuwa uchaguzi huu ni mwepesi. Watu wamebeba mengi kwenye Nafsi zao. Waatu wanataka kutumua sanduku la kura kuonesha hisia zao.

Rais Magufuli unatakiwa utambue kuwa,
huu uchaguzi ni mgumu sana haijawai tokea hapa Tanzania na ukiudharau utakushangaza.

Rais Mstaafu J. Kikwete ni mmoja wa viongozi wenye upawa mkubwa wa kuvuta hisia za watu.

Rais Magufuli, Jisushe na Muombe Mh Kikwete aje akusaidia kufanya kampeni. Hutaweza wewe peke yako. Kumbuka bado siku 50+. Uliyekuwa ukimtegemea sana ndiyo hivyo Mungu kampenda zaidi. Sasa mtumie aliyebaki anaweza kuwa msaada mkubwa kwako zaidi ya hata uliyekuwa ukimtegemea.

Aliyekudanganya kuwa wasanii ndiyo watakupa kura, mchunguze kwa umakini sana. Anawezakuwa anafaidika kupitia posho za ao wasanii. Ila ukweli ukiangalia mikutano yako imejaa watoto na wanawake tu ambao wanavutiwa na wasanii tu.
Awamu ya nne waliishaambiwa nchi ilikuwa shamba la bibi (musib)
 
Magufuri hata asipopiga kampeni atashinda tu... Hamna mtu anayeweza kuwapa chadema nchi. Mbona haitaji hata elimu ya chuo kikuu kuelewa hilo. Watu wengine vichwa vyenu vina nini? Mbona hamuelewi?

(Hamna mtu anaeweza kuwapa chadema nchi) ebu tohoa hiyo sentesi tumjue huyo mtu anayeweza kumpa mtu nchi
 
alitoboa lowassa kipindi kile sembuse magufuli mwenye kucheza singeli[emoji38][emoji38][emoji38].

mnatafuta tone la maji kupooza makoo yenu lakini waaapi.
magu rais 05 tena.
Kwani hujasikia waliokuwa Wazima wazima wa afya tele wakifa kabla ya Lowassa? Yule Mzee wa Lupaso aliyetuita malofa yuko Wapi, Samweli 6 yuko wapi? Kwa hiyo usipime afya ya mgombea wenu kwa kutazama afya ya Mtu mwingine...kwani Kwanza yeye mwenyewe si alikusudia Lissu afe? Sasa si anatokwa jasho?
 
ndio maana nakushanga wewe unayejaji mtu kwa sura yake iliyochoka na utu uzima.

mkikosa hoja mnakuwa viumbe wa hovyo hovyo sana.
 
Mkuu makada wa CCM mpya na team Magufuli walikuwa wanategemea sana mbeleko ya Benjamin Mkapa ktk kupangua hoja kutoka kwa wapinzani, kiasi kwamba hawakuona umuhimu wa Jakaya. Sasa imefika wakati anakubali kufa na tai shingoni.

Hoja jadidu za ushindani kutoka CDM za team Lissu na za ACT Wazalendo za team Membe na Maalim Seif zinamtia kiwewe.
 
Magufuri hana haja ya kufanya kampeni na kuanza kutoa ahadi mpya
Anachokisimamia yeye hivi sasa miradi yake aliyoianzisha ifikie ukomo
Kazi kubwa hivi sasa ni ya wapinzani kuibua hoja mpya
Hoja za zamani za wapinzani
Tume huru ya uchaguzi
Katiba mpya
Nchi aina ndege hata 1 ni aibu hii
Elimu bure kuanzia awali mbaka seco
Vifaa tiba hospital zetu hakuna
Madawa hospital zetu hakuna
Madini yanaibiwa na mabeberu
Ndani ya ccm kuna mapapa wa ufisadi
Miradi ya umeme tunapigwa
Mikataba feki
Mali asili za taifa ikiwemo twiga wanapindwa kwenye ndege
Rushwa serikalini
Nidhamu mbovu ya watumishi serikalini

Baada ya miaka mitano ya magufuri
Leo wapinzani wamepindua meza
Wamekuja na hoja mpya
Kazi ya magufuri na ccm yake ni kuzisikiliza hoja za wapinzani na kisha kuzifanyia kazi ili 2021 2022 mbaka 2025
Mtakuwa tayari mmeshamalizana nazo
Ifikapo 2025 wapinzani waje tena na hoja zingine hapo ndio tutakuwa tunajenga taifa la tanzania..
Nimesoma nikajiuliza ni mtanzania gani chizi hivi, kurudi juu na kuta ni wewe ikabidi nikusamehe bure
 
Back
Top Bottom